The House of Favourite Newspapers

JB: King Majuto atacheza filamu yangu

0

JBStaa wa filamu Bongo Jacob Stephen maarufu kama JB.

Na Mayasa Mariwata
STAA wa filamu Bongo Jacob Stephen maarufu kama JB, amesema licha ya muigizaji mkongwe Amri Athumani ‘King Majuto’ kudai kuiweka kando sanaa ili afanye mambo ya kumpendeza Mungu baada ya kurejea kutoka hija huko Makka, atafanya hivyo baada ya kucheza kazi atakayoiandaa.

Akizungumza na gazeti hili, alisema yeye ni kama mtoto kipenzi wa Mzee Majuto, hivyo hawezi kukataa ombi lake kwa kuwa hata yeye anataka kustaafu kuigiza baada ya kufanya filamu moja na muigizaji huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa uchekeshaji.

maxresdefaultMzee Majuto.

“Kama kuacha rasmi ataacha kupitia filamu yangu ambayo itakuwa kama kanizawadia mwanaye kipenzi na nimejaribu kumshawishi kakubali, sababu hata mimi baada ya hiyo filamu mwakani sitarajii tena kuigiza, nitakuwa mtayarishaji tu kupitia kampuni yangu ya Jerusalem maana nakaribia miaka 50 sasa,” alisema.

Leave A Reply