Je Unajua Usingizi Unaweza Kukusababishia Kifo?
“IWAPO una hamu ya kutaka kuishi maisha marefu basi utalazimika kuwekeza katika kujipatia usingizi mzuri, hii ni kulingana na mtaalamu wa usingizi, Matthew Walker.
Matthew ambaye ni profesa wa sayansi ya neva (mishipa ya fahamu) na ile ya saikolojia, katika Chuo Kikuu cha California, Marekani, amefanya uchunguzi kutoka kwa mamilioni ya watu ambao wamehusika katika utafiti wa tawi la sayansi inayoangazia visa, usambazaji na udhibiti wa magonjwa na sababu nyengine zinazohusiana na afya.
“Usingizi ni kiungo muhimu cha kidemokrasia na mfumo wa afya ambao unapatikana bure,” ameainisha.
Na jamii ya kisayansi inaamini kwamba baada ya miaka 50, wataalamu wa usingizi kote duniani hawatafanya tafiti za kuangazia kile ambacho kinasababishwa na usingizi, lakini, je, kuna kitu chochote ambacho usingizi hautupatii?
Kufikia sasa wataalam hawawezi kupata kitu chochote ambacho hakikuzwi na usingizi ama kile ambacho hukosekana wakati usingizi unapokuwa mfupi. Sayansi imebaini kwamba ukosefu wa usingizi husababisha athari mbaya kwa miili yetu na ubongo.
Kila ugonjwa unaowaua watu katika mataifa yalioendelea kama vile ugonjwa wa kusahau, saratani, magonjwa ya moyo, unene wa kupita kiasi, kisukari, unyongo’nyevu, wasiwasi na hata mtu kutaka kujiua, unahusishwa na ukosefu wa usingizi.
Mifumo yote ya kisaikolojia katika mwili wa binadamu ama hata oparesheni ya akili, huimarishwa wakati mtu anapolala.
Viungo hivyo vyote huathirika iwapo unakosa usingizi wa kutosha. Na ni sharti uwe na usingizi halisi ili viungo hiyyo viweze kuimarishwa. Hata hivyo, ni lazima kufahamu kwamba dawa za kumfanya mtu apate usingizi zinahusishwa na kiwango cha juu cha hatari ya saratani, maambukizi na vifo.
Comments are closed.