JELA MAISHA KWA KUKIRI KUUA, KULA NYAMA YA BINADAMU

WANAUME wawili nchini Afrika Kusini wamefungwa maisha baada ya kutiwa hatiani kwamba walimuua na kumla mtu mmoja.

Watu hao waliotiwa hatiani na kuhukumiwa na Jaji Peter Olsen wiki hii Jumatano, ni Nino Mbatha (33) na Lungisani Magubane (32) waliomuua na kumla Zanele Hlatshwayo, limeandika gazeti la  Witness.

Mbatha, ambaye ni mganga wa kienyeji alikamatwa baada ya kujisalimisha kituo kimoja cha polisi huko  Estcourt, mji ulio katika jimbo la KwaZulu-Natal ambapo akiwa amebeba mfuko uliokuwa na mguu na mkono wa mtu, aliwaambia maofisa wa polisi kwamba  “nimechoka kula nyama ya binadamu”.

Hata hivyo, polisi hawakuamini madai yake hayo mpaka alipowapeleka kwenye nyumba moja ambako walikuta mabaki ya mwili wa binadamu.

Mwanzoni mwa kesi hiyo jumla ya watu saba walikuwa wamekamatwa.

Watu waliokuwa wamefurika katika mahakama hiyo walitaka kuwashambulia washitakiwa hao.

Kosa la kula nyama ya mtu liliondolewa katika mashtaka hayo, kwani nchini Afrika Kusini hakuna sheria ya moja kwa moja dhidi ya watu kula nyama ya watu, lakini kuna sheria dhidi ya kuharibu maiti na kukutwa na sehemu au vipande vya mwili wa binadamu.

Loading...

Toa comment