The House of Favourite Newspapers

Jembe la Kaze Larejea Kikosini Yanga

0

RASMI sasa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mburkinabe Yacouba Songne, atakuwa sehemu ya kikosi cha keshokutwa kitakachocheza na Coastal Union ya mkoani Tanga.

 

Hiyo ni baada ya kukosekana muda mrefu uwanjani katika michezo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, kutokana na majeraha ya misuli aliyoyapata katika Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

 

Mburkinabe huyo kesho saa kumi kamili atakuwepo kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kucheza na Coastal mchezo unaotarajiwa kujaa upinzani mkubwa.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Kocha Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, alisema kuwa kiungo huyo amepona kwa asilimia mia moja, hivyo atakuwa sehemu ya kikosi cha timu kama siyo kuanza basi kutokea benchi.

Kaze alisema kuwa katika mazoezi ya mwishoni kuelekea mchezo huo, kiungo huyo alifanya vizuri katika mazoezi yake na kumpa matumaini ya kumtumia katika michezo ijayo.

 

Aliongeza kuwa kurejea kwa kiungo huyo kumempa matumaini ya kufanya vizuri kwa kuanzia mchezo huo dhidi ya Coastal na mingine inayofuatia ya ligi na FA.

 

“Yacouba amepona, yuko fiti kucheza mchezo ujao dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo wa ligi tutakaocheza keshokutwa Alhamisi.“

Anarejea uwanjani baada ya kukosa michezo sita ya mashindano baada ya kupata maumivu ya misuli akiwa kwenye Kombe la Mapinduzi huko Zanzibar,” alisema Kaze.

Leave A Reply