The House of Favourite Newspapers

Jenerali wa Jeshi Burundi na mkewe wauawa

0

Jenerali Burundi

Jenerali Athanase Kararuza.

OFISA Mkuu wa Jeshi la Burundi, Jenerali Athanase Kararuza ameuawa pamoja na mkewe baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mjini Bujumbura leo asubuhi.

Jenerali Kararuzana na mkewe wameuawa katika Tarafa ya Mutanga wakiwapeleka watoto wao shuleni, ofisa mmoja wa usalama ambaye hakutaka jina lake litajwe ameliambia shirika la habari la AFP.

Wizara ya ulinzi pia imethibitisha kifo cha jenerali huyo.

Athanase Kararuza alikuwa mshauri wa masuala ya ulinzi katika ikulu ya rais na kamanda wa pili katika kikosi cha kimataifa cha kulinda amani Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Leave A Reply