Jengo la shule laanguka, laua wanafunzi wanane

 WATOTO zaidi ya wanane wamefariki na wengi kujeruhiwa na kunasa katika mabaki ya jengo la shule lililoanguka jijini Lagos, Nigeria.

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la utangazaji la Uingereza (BBC) kikosi cha uokoaji kilisema shule hiyo ambayo ilikuwa katika jengo la ghorofa tatu eneo la Ita Faji katika Kisiwa cha Lagos, ilikuwa na wanafunzi zaidi ya 100

Habari kutoka eneo hilo ambapo chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana, wanafunzi wapatao 40 waliokolewa wakiwa hai na waokoaji bado wanatafuta wengine.

 

Sehemu ya jengo hili lililoanguka ilikuwa pia na sehemu za makazi na shule. Pamoja na wanafunzi kadhaa kuokolewa kutoka katika vifusi, wazazi wengi walikuwa na wasiwasi kwa kutowapata watoto wao ambapo wengine walilazimika kwenda hospitali ambako majeruhi wengi walipelekwa.

Ni kawaida ka majengo kuanguka nchini Nigeria kutokana na kujengwa chini ya viwango.

Mwaka 2016, zaidi ya watu 100 walifariki wakati paa la kanisa moja huko Uyo, Kusini mwa Nigeria, lilipoanguka.


Loading...

Toa comment