The House of Favourite Newspapers

Jerry Muro Atoa Ushuhuda wa Maisha Yake – Video

MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amewataka vijana kujitambua na kuachana na wale wanaowabeza kwani ni Mungu pekee ndiye anajua hatima ya maisha ya kila mwanadamu hapa duniani.

 

Muro ametoa kauli hiyo usiku wa kuamkia leo wakati akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini waliokusanyika katika Kongamano la Victory Campus Night 2019 lililofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar.

Amezungumza mengi huku akianika baadhi ya mapito na changamoto alizopitia mpaka kufika alipo huku akiwataka wanafunzi hao kutokata tamaa na badala yake wasome kwa bidii na  wakimtegemea Mungu.

“Wakati nasoma pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hakuna hata mwenzangu mmoja aliyejua kama ningekuwa mwanahabari, ama ningekuja kuwa Msemaji wa Yanga… Lakini leo mimi ni mkuu wa wilaya. Mungu anao uwezo wa kukuinua na kukutoa shimoni…. ”

 

Comments are closed.