The House of Favourite Newspapers

Jerry Muro kupandishwa ‘kizimbani’

0

DSC03160 (1)Msemaji wa Yanga, Jerry Muro.

Nicodemus Jonas, Dar es Salaam
KAMA ulidhani ile kesi inayomkabili msemaji wa Yanga, Jerry Muro imepotezewa kiaina, unajidanganya, maana Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema bado iko hai na muda wowote ataitwa kwenye Kamati ya Maadili kusomewa kesi yake.

Muro alikumbana na kadhia hiyo miezi miwili iliyopita kutokana na kutoa lugha ya kibaguzi dhidi ya msemaji wa Simba, Haji Manara ambapo TFF ilitangaza kumfikisha katika kamati hiyo.

Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, ameliambia gazeti hili kuwa, ataitwa kwa kuwa siyo mara yake ya kwanza kwani aliwahi kutozwa faini na Kamati ya Nidhamu kwa kosa jingine.

Leave A Reply