The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Burkina Faso Lakiri kuwaua Raia Katika Uvamizi wa Anga

0
Wanajeshi wa Burkina Faso

JESHI la Burkina Faso limesema liliwaua Raia kwa bahati mbaya wakati wa Oparesheni ya Kijeshi Kusini Mashariki mwa nchi hiyo mapema wiki hii.

 

Nchi hiyo imekuwa ikipambana na uasi wa kutumia Silaa unaofanywa na Makundi ya Waasi, baadhi ya hao waasi hao wanahusishwa na kundi la Al-Qaeda.

Jeshi hilo limekiri kuwaua raia kwa bahati mbaya

Jeshi la Nchi hiyo limekiri kuwaua Raia katika Oparesheni yake ya kudhibiti Makundi hayo.

 

“Wakati wa oparesheni ambazo zilifanywa ili kuwazima magaidi kadhaa kwa bahati mbaya ilisababisha madhara ya Raia”

 

Jeshi ilo lilisema katika taarifa yake siku ya Jumatano, lakini halijasema ni raia wangapi waliuawa.

 

Waathirika walipigwa na makombora katika eneo kati ya Kompiengo na Pognoa karibu na mpaka wa nchi ya Togo siku ya Jumatatu.

 

Togo imekuwa ikikabiliana na uvamizi wa Wanamgambo kutoka Burkina Faso, ambapo iliuwa watoto saba mwezi uliopita katika mpaka huohuo.

Leave A Reply