The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Nigeria Lalipua Kimakosa Kambi ya Wakimbizi na Madaktari, 6 Wauawa

c2zmc4exuaanxch Ndege ya Jeshi la Nigeria imelipua kimakosa kambi ya wakimbizi na madaktari wasio na mipaka wakidhani ni wanamgambo wa kundi la Boko Haram katika eneo la Rann kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, linasema kuwa takriban watu 50 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa

Wafanyakazi wa kutoa misaada ni baadhi ya wale waliouawa huku shirika la msalaba mwekundu likisema kuwa 6 kati ya wafanyakazi wake waliuawa.bomu

Shambulizi hilo lilitokea karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon ambapo jeshi la Nigeria limekuwa likipigana na kundi la Boko Haram.

Msemaji wa jeshi Meja Jenerali Lucky Irabor, anasema kwa rubani wa ndege kimakosa aliamini kuwa alikuwa akiwashambulia wapiganaji.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, ametuma rambi rambi akisema kuwa amehusunishwa na kupotea kwa maisha na kuomba kuwepo utulivu.

MSF inasema kuwa watu wengi waliouawa ni wale waliohama maeneo ambapo Boko Haram walikuwa wemeendesha mashambulizi.

Comments are closed.