Jeshi la Polisi Latembelea Ofisi za Vodacom Kukagua Usalama Sehemu za Kazi
Jeshi la Polisi Tanzania, limefanya ziara kwenye ofisi za Kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom kukagua usalama wa ofisi na magari yanayotumiwa na kampuni hiyo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi inayosherehekewa April 28, kila mwaka.