Polisi Arusha Washiriki Mazoezi ya Pamoja na Vyombo vingine vya Ulinzi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo leo Februari 01, 2025 wamefanya mazoezi ya pamoja (Route March) kwa kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini Arusha na badaye kufanya mazoezi ya viungo.
Matembezi hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano baina ya Majeshi ya ulinzi na Usalama, kuongeza uimara na utimamu wa mwili miongoni mwao pamoja na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika kulinda amani na usalama wa Nchi.