The House of Favourite Newspapers
gunners X

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Songwe Katika Doria Maalumu Ya Kuimarisha Usalama

0

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe Septembe 22, 2024 limefanya zoezi la kujaribu vitendea kazi vyake vyote vya kulinda raia na mali zao ili kujiweka tayari kwa lolote litakalojitokeza.

Vitendea kazi hivyo ikiwemo magari ya doria, kikosi cha mbwa na farasi na kikosi vya Usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kikosi cha kuzuia ghasia vilionekana katika doria mitaa mbali mbali ya Mji wa Mpemba, Tunduma Wilaya ya Momba na Vwawa na Mlowo Wilaya ya Mbozi ili kuwaondoa hofu raia wema wanaofuata sheria na taratibu za nchi na kuwahakikishia kuwa ulinzi na usalama wao umeimarika.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe SACP Augustino Senga amefanya ukaguzi wa vitendea kazi hivyo pamoja na ukakamavu wa askari kuhakikisha wepesi wao katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupongeza uimara wao uluotokana na mazoezi ya Utayari ya mara kwa mara na yanayoendelea nchini kote.

Sambamba na hilo Kamanda Senga amesema kuwa doria za namna hiyo zitaendelea kufanyika katika maeneo tofauti tafouti ya Mkoani Songwe.

Leave A Reply