The House of Favourite Newspapers

Jeshi La Polisi Zanzibar: Hatutambui Uwepo wa Mazombi

0

1 (3)Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, Salum Msangi.

Jeshi la Polisi Zanzibar limewataka madaktari kuacha kuwahudumia watu wanaokwenda hospitali baada ya kupigwa na kikundi cha watu wasiojulikana cha mazombi bila ya kuwa na fomu ya matibabu (PF3).

Akizungumza na wanahabari mjini Unguja jana, Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar, Salum Msangi alisema matukio ya watu kujeruhiwa na kutopeleka taarifa polisi yanachangia kuendeleza uhalifu.

Alisema taswira ya haraka wanayoipata ni kwamba inawezekana watu wanaotendewa vitendo hivyo ni wahalifu ambao wamekutana na wahalifu wenzao hivyo kuhofia kutoa taarifa ili uhalifu wao usibainike hali inayosababisha kunung’unika pembeni bila ya kufikisha taarifa maeneo sahihi ili zifanyiwe kazi.

“Kwa mujibu wa taratibu zilizopo ni kwamba mtu yeyote anayefanyiwa kitendo cha kihalifu anapaswa kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi ili uchunguzi au upelelezi ufanyike kubaini wahalifu hao,” alisema Msangi.

Alisema iwapo polisi itambaini daktari atakayetoa tiba kwa watu hao bila PF3 itamchukulia hatua.

Alisisitiza polisi kutowatambua mazombi hao ambao huvaa soksi nyeusi usoni, wakiwa na silaha wanazotumia kuwashambulia watu kwa vile wanaofanyiwa vitendo hivyo hawatoi taarifa.

Alisema kumejitokeza mambo matatu; vipeperushi vyenye vitisho, mazombi na kuwekwa alama za X kwenye baadhi ya nyumba hasa Pemba na kutoa tahadhari kwa mtu yeyote anayehusika, kikundi au jumuiya inayojihusisha na utoaji wa vitisho hivyo kuacha mara moja kabla ya jeshi hilo kuchukua hatua kali dhidi.

Akivisoma vipeperushi hivyo, Msangi alisema kuna vikaratasi vimesambazwa vyenye ujumbe usemao ipo siku itakuwa kweli ‘One Day Yes’ kingine “Kutangazwa uchaguzi siyo kufanyika uchaguzi.”

Leave A Reply