The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Yanga Limekamilika, Kesho Kukiwasha Uwanja wa Mkapa

0

JESHI limekamilika, hivi ndivyo unaweza kusema baada ya uongozi wa Yanga, jana kumtangaza Mserbia Zlatko Krmpotić kuwa ndiye kocha mkuu wa kikosi hicho akichukua nafasi ya Mbelgiji, Luc Eymael aliyetimuliwa.

 

Yanga imemchukua kocha huyo akitokea Polokwane City ya nchini Afrika Kusini huku klabu baadhi nyingine alizopita ni APR (Rwanda), Zesco United (Zambia) na TP Mazembe (DR Congo).

 

Timu hiyo imemchukua kocha huyo baada ya Mrundi, Cedric Kaze aliyekuwa anafundisha Academy ya Barcelona kupata matatizo ya kifamilia.

 

Akizungumza jijini Dar jana, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Injinia Hersi Said alisema kuwa kocha huyo anatarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam leo Jumamosi akitokea Serbia.


Hersi alisema kuwa, kocha huyo mara baada ya kutua atasaini mkataba wa miaka miwili alioandaliwa baada ya kufanya naye mazungumzo na kufi kia muafaka mzuri wa kuifundisha timu hiyo iliyopania kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao.

“Tulipokea CV 21 za makocha mbalimbali kati ya hizo za wazawa ilikuwa moja pekee ambayo iliomba kuwa msaidizi, lakini hao wakuu wote kutoka nje ya nchi na katika CV hizo makocha wote walistahili kuifundisha Yanga.“Lakini kamati ilipe ndekeza makocha wawili ambao ni Kaze tuliyefi kia makubaliano mazuri ya kuja nchini kuifundisha Yanga lakini matatizo ya kifamilia ndiyo yakakwamisha mipango hiyo.


“Baada ya dili kufeli, haraka tukahamia kwa Zlatko ambaye yeye alikuwa chaguo letu la pili kati ya makocha hao walioleta CV zao Yanga, hivyo kamati ikachukua maamuzi ya kumpitisha Mserbia huyo kuja kuifundisha Yanga ambaye atatua nchini kesho (leo) asubuhi akitokea kwao Serbia“Uzoefu wa Zlatko wa kufundisha timu za Afrika ndiyo imetushawishi sisi viongozi kumpa nafasi ya kuja kuifundisha Yanga, kwani aliwahi kuzifundisha klabu za TP Mazembe, Zesco na Polokwane, kocha huyo tumemuachia nafasi mbili za usajili za wachezaji wa kigeni ambazo kama akihitaji mchezaji wake atakayetaka kufanya naye kazi tumsajili,” alisema Hersi.

 

MAFANIKIO YA ZLATKO

Amewahi kuwa kocha bora kule DR Congo msimu wa 2016-2017, msimu uliofuata pia akawa kocha bora kwenye ligi ya Zambia akiwa na Klabu ya Zesco pia akawa kocha bora Afrika. Mwaka 2018 baada ya kutua Botswana kuinoa Jwaneng Galaxy aliibuka pia kocha bora wa msimu.

 

BENCHI JIPYA LA UFUNDI LATANGAZWA

“Nichukue nafasi hii kumtangaza Mwambusi (Juma) ndiye kocha wetu msaidizi tuliyeingia naye makubaliano ya mwaka mmoja kuifundisha Yanga ambaye tayari ameanza kazi, tumemchukua kocha huyu baada ya kupokea mapendekezo ya Zlatko ambaye ameomba kocha mzawa.

 

“Pia, kocha wetu mpya wa makipa ni Niyonkuru (Vladimir) ambaye ni raia wa Burundi yupo tayari nchini kwa kufanya kazi yake hiyo, tumeliboresha benchi letu la ufundi kwa ajili ya kufi kia malengo yetu,” alisema Hersi.

 

KAZE AFUNGUKA MAZITO AKIWA BURUNDI

Kwa upande wake aliyetarajiwa kuwa kocha wa Yanga, Cedric Kaze alifafanua kwa nini hajatua ndani ya kikosi hicho: “Sababu kubwa iliyonifanya nishindwe kujiunga na Yanga ni matatizo niliyoyapata ya kifamilia, masuala ya kifamilia hayawezi kunifanya niondoke hapa nyumbani. Siyo sawa kufanya kazi huku roho yangu ikiwa haipo hapo ninapofanya kazi.

 

“Nilihofi a kuja Yanga kwa hofu ya kuharibu kazi kwani ni kati ya timu kubwa katika Ukanda wa Afrika, hivyo nitakuja huko baadaye nitakapokuwa tayari kuja kufundisha Yanga.

 

“Siyo presha iliyonifanya nishindwe kuja Yanga, kwani matatizo makubwa nimeyapata ya mtu kufanyiwa upasuaji ndani ya siku hizi chache na mimi ndiyo kila kitu katika familia.“Presha nishaizoea hasa kwenye kazi yetu ni kitu cha kawaida, ni kweli presha ipo Yanga lakini hiyo ndiyo inanifanya mimi nifanye kazi kwa nguvu kwa kuwapa morali wachezaji na kufanya vizuri.

 

Niliwahi kufundisha klabu kubwa nyingi zenye presha hivyo hiyo siyo sababu.“Nimemaliza mkataba Barcelona tangu Machi, mwaka huu na nilikuwa hapo kwa miaka mitatu. Nilikuwa natamani kuja kufundisha Afrika.” Soma jeshi kamili la Yanga la msimu ujao Uk 12&13.

 

KUHUSU JEZI MPYA “Jezi mpya zimechelewa kufi ka nchini kutokana na changamoto ya usafi ri iliyopo kwenye baadhi ya nchi, hiyo ni baada ya Corona hivyo usafi ri tulioutumia ni meli ambayo bado haijafi ka.“Tumefi kia hatua ya kuleta mzigo kwa njia ya meli kutokana na changamoto ya anga za nchi nyingi kufungwa, na kama unavyofahamu njia ya meli inachelewa, lakini niwatoe hofu kuwa jezi mpya tutazitambulisha kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Taifa, Dar

Leave A Reply