The House of Favourite Newspapers

Jeshi Lakabiliana na Waasi Sudan

0

Jeshi la Sudan linayashikilia makao makuu ya kikosi cha usalama wa taifa cha nchi hiyo ambacho awali kilikuwa kitiifu kwa rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir kwa makosa ya uasi.

 

Mapambano yalianza Jumanne katika jiji la Khartoum ambapo milio ya milipuko ilisikika na  kupelekea Kitengo hicho cha usalama wa taifa kwa sasa kuvunjwa.

Serikali inadai kuwa uasi huo umechochewa na malipo ya mafao, lakini pia kuna mashaka juu ya tukio hilo kulenga kuchelewesha mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

 

Kiongozi mwandamizi wa baraza huru linaloongoza Sudan kwa sasa, Jenerali Mohammed Hamdan Dagalo, amemtuhumu mkuu wa zamani wa usalama wa taifa Salah Gosh kuwa yupo nyuma ya uasi huo.

 

Leave A Reply