The House of Favourite Newspapers

Jesus Moloko Ajazwa Upepo Yanga

0
Mkongomani, Jesus Moloko.

MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, amemjaza upepo na kumpa sifa nyingi winga mpya wa timu hiyo, Mkongomani, Jesus Moloko akisema anaamini ataliziba pengo la Tuisila Kisinda.

Yanga imemsajili Moloko akitokea AS Vita ya DR Congo kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Kisinda aliyeuzwa hivi karibuni kwenda RS Berkane ya nchini Morocco.

Akizungumza naSpoti Xtra, Mwakalebela alisema kuwa kati ya mawingabora Congo, basi Moloko yupo, hivyo hawana hofu katika msimu ujao.


Mwakalebela alisema kuwa hawajakosea kumsajili winga huyo huku akiamini kuisaidia timu hiyo katika msimu
ujao ambao wamepanga kubeba makombe yote watakayoshiriki.

“Hatujakosea kumsajili Moloko, kwani tukiwa kambini Morocco nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu kwa ajili ya kujua uwezo wake.

“Kati ya usajili bora ambao tumeufanya katika msimu huu, basi huu wa Moloko ni mmoja wapo kutokana na kiwango
kikubwa alichonacho.

“Kikubwa anachotakiwa ni kutimiza majukumu yake ya uwanjani kufunga na kutengeneza nafasi kwa wake ili timu ipate matokeo mazuri,” alisema Mwakalebela.

Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga na Mkurugenzi wa Uwekezajiwa GSM, Injinia Hersi Said ambaye alifanikisha usajili wa winga huyo, alisema:

 

“Kwa hakika Moloko ni mchezaji ‘potential’ ni mbadala sahihi wa Kisinda ambaye tumemuuza, kwangu namuona Moloko anakwenda kuwa mara tatu zaidi ya Kisinda kutokana na uwezo alionao.

 

“Jambo la kusubiri ni yeye afanye vizuri akiwa uwanjani, kwa sababu hilo ndiyo jambo la muhimu zaidi ambalo mashabiki wanatakiwa kumuombea.

Leave A Reply