Jesus Moloko Akabidhiwa Majukumu Maalum Yanga SC

WINGA mpya wa Yanga Mkongomani, Jesus Moloko ameidhinishwa na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ya kupiga mipira yote ya kona katika mechi za timu hiyo.

 

Moloko ameonekana akianza kupiga mipira hiyo katika mchezo wake wa kwanza wa Wiki ya Mwananchi dhidi ya Zanaco ya Zambia uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar. Mchezo mwingine ni wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba ambao walishinda bao 1-0 uliochezwa uwanjani hapo.

 

Mwingine ni ule wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar ambao Yanga walishinda bao 1-0 uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba dhidi ya Kagera Sugar.

 

Winga huyo huyo hadi hivi sasa hajafunga bao tangu ajiunge na timu hiyo katika msimu huu akitokea AS Vita ya Congo Kinshasa kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Tuisila Kisinda aliyeuzwa RS Berkane.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam


Toa comment