The House of Favourite Newspapers

Jeuri ya Yanga SC ipo hapa

0

MTENDAJI Mkuu wa Yanga, Senzo Mbatha Mazingisa, amesema kuwa jeuri ya wao kufanya vizuri msimu huu inatokana na kuwa na kikosi kipana ambacho anaamini kinatosha kuwapa mafanikio tofauti na msimu uliopita.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Senzo alisema: “Msimu uliopita tulikuwa tuna kikosi kimoja cha kukiamini pekee, yaani akiumia mchezaji tegemeo mmoja basi  inakuwa tabu kubwa, lakini msimu  huu naamini kidogo tupo tofauti,  hivyo tunatarajia kupata mafanikio  kama kutwaa ubingwa wa ligi kuu.

 

“Najua haitakuwa kazi nyepesi  bila kupambana, lakini tayari kama  viongozi tumejitoa kuhakikisha  mafanikio yanakuja ndani ya timu,  hivyo tunahitaji kupewa ushirikiano  mkubwa kutoka kwa mashabiki  wetu na mambo mazuri yatakuja.” Tayari Yanga imeanza msimu huu  wa 2021/22 kwa ubingwa wa Ngao  ya Jamii baada ya kuifunga Simba  bao 1-0, wikiendi iliyopita.

STORI: MARCO MZUMBE

Leave A Reply