The House of Favourite Newspapers

Jezi Nyekundu ya Zahera Yaacha Maswali

KOCHA ambaye jina lake likitajwa tu mashabiki wa Yanga wanashtuka, Mwinyi Zahera ametua nchini usiku wa kuamkia jana Jumatano. Zahera tofauti na alivyozoeleka juzi alikuwa amepiga uzi mwekundu wa timu ya Taifa ya DR Congo na baadhi ya mashabiki waliokuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere aliwagawia.

 

Yanga wamekuwa hawataki kumsikia Zahera kwa madai kwamba anavujisha siri zao kwenye vyombo vya habari. Spoti Xtra linajua kwamba kocha huyo ana ofa tatu mezani kwake ingawa amegoma kuweka wazi majina ya timu mpaka atakapomalizana na Yanga wiki ijayo.

 

Lakini habari zingine zimekuwa zikimhusisha na Simba na inadaiwa kwamba walimhamisha kutoka kwenye jumba alilokuwa akiishi maeneo ya ufukwe wa Kawe na kumpangishia katika hoteli ya kifahari ya  YANGA wamelielekeza benchi la ufundi na wachezaji kuwashukia Alliance kwelikweli jijini hapa kesho Ijumaa. Viongozi wamepania kipigo hicho cha sapraizi ili kuwashtua watani wao Simba wanaokutana nao Januari 4 mwakani.

 

 

Lakini vilevile kocha amewaahidi kutopoteza mchezo huo pamoja na kuwafanyia sapraizi Simba watakapokutana nao mwakani licha ya gharama ya vikosi hivyo kutofautiana. Baada ya mchezo wa kesho Ijumaa, Yanga haitacheza tena mpaka itakapokutana na mwenyeji wao Simba kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa chini ya kocha mpya kwani Patrick Aussems anasepa.

Mmoja wa vigogo wa ufundi wa Yanga, ameliambia Spoti Xtra kwamba kwenye mechi ya kesho wanaanzia kutafuta mzuka wa kuwavaa Simba na mambo mengi watafanya kimyakimya. Boniface Mkwasa ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, amewasisitiza mashabiki waje uwanjani kwa kujiamini kwani Kirumba wameizoea na wanajua jinsi ya kuitumia kushinda mechi.

 

Kocha huyo ambaye akishinda atatimiza pointi tisa tangu akabidhiwe timu, amesema ataivaa Alliance kwa tahadhari kubwa kwa vile anajua watapania baada ya kipigo dhidi ya Azam. “Alliance wametoka kufungwa bao 5-0 na Azam katika hali ya kawaida lazima watukamie ili kupoza machungu yao na mimi nimejiandaa kuingia kwa tahadhari ili tuweze kupata matokeo katika mchezo huo, tuna kila sababu ya kushinda wala hatuhofii,” alisisitiza kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars ambaye ni mwanachama wa Yanga.

 

“Wote ni mashahidi kwamba tangu nipewe timu hii timu kiujumla imebadilika kiuchezaji hivyo nimejipanga kupambana ili pointi za Mwanza tusizipoteze, naamini tutapambana,” alisema na kuongeza kuwa CCM Kirumba hakumpi wasiwasi wowote.

 

“Kirumba hakutupi wasiwasi kwa kuwa naujua tangu nacheza hivyo mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutusapoti tukiamini kwamba tutapata matokeo mbele ya Alliance,” alisema Mkwasa ambaye habari za ndani zinasema kwamba huenda akamaliza msimu Yanga.

 

Habari zinasema kwamba viongozi hawana mpango wa kubadili benchi la ufundi licha ya kupokea maombi kadhaa ya makocha kutoka ndani na nje ya nchi, Yanga wanaamini Mkwasa anatosha kwa ligi na FA. 3-0 Katika mechi za Ligi, Yanga imekutana na Alliance mara mbili na kushinda zote. Dar mabao 3-0, huku Mwanza wakishinda bao 1-0.

 

Ramada iliyoko ufukweni. Zahera alitua juzi saa nane usiku akitokea kwao DR Congo, huku akidaiwa amekuja kukamilisha dili la Simba ambayo imempiga chini, Mbelgiji Patrick Aussems ambaye jana alikuwa amenuna na akasusa kabisa kuzungumza na Spoti Xtra hotelini kwake kwa madai kwamba amevurugwa.

 

Tayari Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Denis Kitambi ameweka wazi kwamba; “Nimeambiwa na mtendaji mkuu wa klabu kwamba kocha amesimamishwa na mimi nishikilie timu kwa wiki moja.”

 

 

Katika mahojiano maalum na Spoti Xtra jana hotelini kwake, Zahera hakutamka moja kwa moja kwamba amezungumza na Simba lakini akasema ukweli utafichuka baada ya kumalizana na Yanga watakapotoka Mwanza.

 

“Hizo za Simba ni tetesi tu na nisingependa kuzungumzia hilo kwa sasa, lakini kama kocha niseme tu nina haki ya kujiunga na timu yoyote iwe Simba, Ndanda FC au Ruvu Shooting kumbuka mimi ni profeshno.

 

“Kwa sasa ninaangalia maslahi pekee yatakayoniwezesha mimi kubaki kwenye timu nitakayoifundisha, timu itakayonilipa mshahara mzuri nitakuwa tayari kujiunga nayo,”alisema Zahera ambaye amechukua uraia wa Ufaransa.

 

OFA TATU “Mara baada ya kuachana na Yanga nimepata ofa tatu kati ya hizo ipo moja pekee ambayo imeonekana kutokuwa na fedha za kunilipa mimi, lakini hizo mbili zimeonyesha nia kubwa.

 

“Kwa hivi sasa sitaweza kuzitaja ni timu zipi au kutoka nchi zipi hadi pale nitakapokutana na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kunipatia barua rasmi ya kuchana na mimi, pia watakaponilipa madai yangu yote ninayodai. “Subirieni mara baada ya kumalizana na Yanga, basi nitaweka wazi kila kitu changu. Hapa ninapokwambia tayari nimetumiwa tiketi za ndege kati ya hizo moja yangu

na nyingine ya aliyekuwa msaidizi wangu, Mwandila (Noel) ambaye nitakuwa nae. “Nimeshawaonya viongozi tangu nikiwa njiani nikijiandaa kurejea kuwa nataka baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Alliance tumalizane,wakichelewa basi watakuwa wamejiweka katika wakati mgumu wao wenyewe Fifa, kwa sababu jinsi wanavyochelewa kunilipa fedha zangu ndiyo wananicheleweshea ofa zangu nilizozipata. “Sheria za Fifa zipo wazi, endapo klabu itasitisha mkataba wa kocha basi ni lazima malipo yake yalipwe kwa wakati,” alisisitiza. AUSSEMS ANUNA Gazeti hili jana asubuhi lilimtafuta Aussems kwa kuzungumzia hatma yake ndani ya Simba lakini akagoma kabisa kwa madai kwamba hayuko sawa. “Sijisikii vizuri na siwezi kuzungumza chochote, labda siku nyingine mnitafute nitakuwa katika sehemu ya kuzungumza,” alisema Aussems.

 

Comments are closed.