The House of Favourite Newspapers

#CelebrityUpdates: Jiandae Kumuona Vanessa Mdee Kwenye Season 5 Ya MTV Shuga ‘Down South’ Mwezi Huu – (Video)

Msimu wa tano wa MTV Shuga (MTV Shuga ‘Down South’) upo njiani na msanii kutoka Bongo Flevani Vanessa Mdee ni miongoni mwa sura mpya za kuzitegemea kwenye series hiyo.

Kama ulidhani kuwa kipaji pekee cha Vanessa Mdee ni kuimba basi jiandae kwa ma-surprise kwani msimu wa tano wa series ya MTV Shuga ‘Down South’ itakuacha mdomo wazi ukijiuliza maswali mengi sana juu ya uwezo wake wa kuigiza.

Vanessa Mdee atauvaa uhusika wa mwanadada aitwaye ‘Storm’, na hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Watanzania kumuona Vanessa Mdee akiigiza na itawapa chance mashabiki wake wengi wa ndani na nje ya nchi kuujua uwezo wake mwingine tofauti na uimbaji. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Vanessa alishwahi kuandika:

Nina furaha sana kuwatangazia kuwa nitakuwa kwenye msimu mpya wa #MTVShuga. Itakuwa kazi yangu ya kwanza kabisa ya kuigiza na haitokuwa ya mwisho Inshallah.“. – Vanessa Mdee.

Storm ni nani?

“Storm ni kipenzi cha kila mtu, mrembo mwenye mvuto wa kumpagawisha mtu yoyote akatizae mbele yake. Mbali na uzuri wake Storm ameolewa na Rakeem, lakini maisha ya ndoa yanaonekana kutokompendeza sana mrembo huyo kutoka Tanzania. Uwezo wa Rakeem kushindwa kuonyesha mapenzi ya kutosha yanamuacha Storm akitafuta mapenzi hayo sehemu nyingine. Ujio wa Femi unakuja kwa wakati sahihi kwa Storm. Je, Storm na Rakeem wataweza kuiokoa ndoa yao? Au ujio wa Femi utavuruga kila kitu.”

MTV Shuga ‘Down South’ itaanza kuonekana kuanzia tarehe 08 March 2017 exclusively kupitia chanel ya MTV Base (DSTV Channel 322) na BET (DSTV Channel 129).

Itazame promo ya MTV Shuga ‘Down South’ na Vanessa Mdee hapa chini.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasia, michezo, comedy, burudani, muziki na mengineyo zikufikie kwa wakati.

 

 

Comments are closed.