The House of Favourite Newspapers

Jicho Lenye Uwezo wa Kuona Gizani Lavumbuliwa

0

Fish-lenses-2Mfumo wa jicho la samaki.

WASHINGTON: Wanasayansi nchini Marekani wamevumbua jicho la kitaalam lenye uwezo wa kuona hata kama ni gizani (sehemu ambayo hakuna mwanga). Wamefanikiwa hilo baada ya kuunganisha vipande vya jicho la samaki aina ya kambamti, jicho ambalo litaweza kutumika kufanyia upasuaji, kutafuta kitu na kulinda maroboti pamoja na kutumika kama darubini wakati wa utafiti wa sayari angani.

Mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Wisconsin, Madison wamesema wameweza kupanua wigo wa tafiti za mifumo ya picha (kuona) kwa kutumia mfumo wa lenzi zaidi kuliko sensor. Roboti za kutegua mabomu, roboti za kufanyia upasuaji na kuchunguza sayari zote zinahitaji mfumo utakaoziruhusu kuona picha au kitu hata kama kuna giza kali.

Fish-lenses-1Crystals zilizopo kwenye jicho hilo

Wataalam waliovumbua jicho hilo wameeleza kuwa, kazi kubwa iliyofanyika ni kuboresha uwezekano wa kuona wakati wa giza. Retina ya jicho sasa imebadilishwa kuwa ya kidigitali zaidi ili iweze kupokea miale mingi au michache ya mwaga na kutengeneza taswira ya picha.

Tofauti na kuongeza uwezo wa kuona, watafiti wamejikita zaidi kwenye kuboresha mwanga unaoingia kwenye sensor. Walipata hamasa kutokana na macho ya viumbe wawili wa majini hasa kamba mti, ambaye wanauwezo wa kuona mbali hata kama kama maji yana top.

51863325Kama walivyo tembo kuwa na sifa za kunusa kitu kilicho mbali zaidi, hata baadhi ya samakai wana macho yasiyo ya kawaida yanaweza kuona kitu kikiwa mbali sana, yana maelfu ya vipande vilaini vya crystals ambavyo havipo kwenye wanyama wengine. Crystals hizo hukusanaya mwanga kutoka maeneo tofauti na kuuboresha uwezo wa kuona ili kumuwezesha kuwinda vitoeo vyake.

Uvumbuzi wa jicho la kitaalam umefanyika kwa kuunganisha maelfu ya magrupu ya crystals za samaki huyo na kuunda kioo ambacho kinalingana ukubwa na poleni. Wataalam hao walikusanya mwanga kutoka kwenye miale inayounda kutokana na kioo hicho. Mwanga ule ulipitishwa kwenye jicho la kambamti (lobster) na kutengeneza picha iliyoboreshwa.

Jicho hilo la kitaalam ni rahisi kufanya kazi kwenye mifumo ya picha iliyopo sasa (kwenye maroboti, ultra sound na kamera) kwa ubora zaidi hata kama kutakuwa na mwanga kidogo au hakuna kabisa.

Kwa bianadamu, jicho hilo litasaidia watu wenye matatizo ya kuona mbali au kuona nyakati za usiku.

CHANZO NA JARIDA LA PNAS

VIDEO YA UTAFITI HUO

Leave A Reply