The House of Favourite Newspapers

Jide Atoboa Siri Ya Kutochuja!

Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ akiwa na mpenzi wake.

MKONGWE wa Muziki wa Afro Pop Afrika Mashariki, Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’ anamaliza mwaka kwa kuachia video ya kibao chake kipya na cha kwanza kufanya na Taurus Musik, Baby.

 

 

Jide amesaini mkataba na lebo hiyo ya Kenya kwa miaka mitatu, ambayo ndani yake, atatengeneza albamu mbili, ikiwemo pia albamu yake ya kwanza ya video. Katika video yake mpya, mwanamuziki huyo amemshirikisha mpenzi wake, Spicy ambaye ni raia wa Nigeria. Hii ni video ya pili kucheza pamoja na Spicy ambaye pia ni mwanamuziki, ya kwanza ikiwa ile ya ngoma yao waliyofanya pamoja, Together Remix.

 

“Ni mkataba mzuri kwangu kwa sababu umezingatia masilahi ya pande zote mbili, ile lebo pia ni kubwa hapa Afrika Mashariki, wanafahamu nini cha kufanya ili msanii atimize malengo yao na yake pia, kwa hiyo ni suala la kujivunia,” anasema Jaydee katika mazungumzo kupitia mtandao wa WhatsApp. “Nimemshirikisha Spicy kwa sababu anafit kwenye nafasi ile, ni msanii lakini kumbuka pia ni mwenza wangu, nadhani nitafanya video nyingi pamoja naye, hata kumi ikibidi, kwani kuna ubaya wowote?”

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M

Ni msanii pekee wa kike aliyeanza kufanya muziki miaka ile ya 2000 ambaye bado yupo katika fani, tena akitesa na kuwashinda hata wadogo zake wenye miaka michache kwenye Bongo Fleva. Wenzake aliopigana nao pamoja ni akina Stara Thomas, Ray C, Unique Sisters, Zay B na baadaye wakaongezeka Raha P, Dataz, Sister P na wengineo, ambao wote wamepotea katika anga la muziki.

 

Ingawa Ray C anaweza kuwa afadhali kuliko wenzake, lakini hawezi tena kurejea levo zile, kwa sababu maisha yake kimuziki yamekutana na changamoto nyingi ambazo zilihitaji muda na maarifa kuweza kuzishinda. “Ni kujitambua tu na kuweka malengo na bidii, hakuna uchawi. Mimi muziki ndiyo kazi yangu, naenda nao kulingana na mahitaji ya soko, siwezi kujua kwa nini wenzangu walikwama, inawezekana hii siyo kazi yao namba moja, tuna tofautiana maisha, kila mtu ana kipaumbele chake.

 

“Mimi nimechagua kazi ya muziki, kila kitu napata kutokana na muziki, kwa hiyo lazima niwe makini na kazi, kimuziki najiona ndiyo kwanza naanza, ninafurahi vile wasanii wachanga wanakuja na kukua kimuziki, napenda changamoto kutoka kwao,” anasema Jide.

Comments are closed.