JIDE, MAI MARTHA WACHONGANISHWA

Judith Wambu­ra ‘Jide’

MWANA­MUZIKI Judith Wambu­ra ‘Jide’ na mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ juzikati walichongan­ishwa baada ya mashabiki kudai kuwa, eti Mai ni mnafiki kwa kuwa kipindi cha msiba wa bosi wa Clouds, Ruge Mutahaba alimnanga mwen­ziye kwa kutohudhuria msiba wake kisha baadaye kuanza kumsifia.  

 

Sakata hilo lilianza hivi; juzikati Maimartha alikomenti kwenye peji ya Insta ya Jide akimsifia, kitendo ambacho kilionesha kuwakera wafuasi wa Jide ambao walimwita Mai mnafiki na kumtaka Jide ‘amblok’

Baada ya baadhi ya mashabiki kushadadia hilo, Jide alikomenti kuwa hata watu wanafiki yeye anawablok kwani hajali; akaandika; ‘I don’t care’ maneno yaliyobeba jina la wimbo wake mpya.

Mwandishi wetu hakuweza kumpata Jide kuzungumzia ishu hiyo lakini Mai alipopigi­wa simu na kuulizwa anach­ukuliaje hilo la kuitwa mnafiki alisema: “Namheshimu Jide, ni dada yangu kabisa wakati mwingine ni hizi kazi tu, wala siwezi kugombana na Jide kabisa, wanaotuchonganisha wana­fanya vibaya sana.”


Loading...

Toa comment