JIFUNZE NJIA YA KUPATA WATOTO MAPACHA

Uzazi ni suala ambalo kila mtu aliye katika umri wa kuzaa analizungumzia. Mwanaume anaweza kuwa na tatizo la uzazi na mwanamke pia. Watu wawili, mke na mume pia wanaenda kuwa na watoto. Kiu ya kupata watoto mapacha inakuwa kubwa zaidi endapo mtu amekaa muda mrefu akitafuta mtoto bila mafanikio huku umri ukienda. Wanawake wengi huwa wana kiu au hamu hii ya kupata mapacha hasa baada ya kutafuta mtoto kwa muda mrefu na wanapofika kutuona madaktari wa uzazi huulizia sana uwezekano wa kupata mapacha.

MATATIZO YA UGUMBA’

Tunasema mtu ana matatizo ya uzazi au mgumba pale mume na mke wanapokuwa wamekaa miezi 12 bila mafanikio na tendo la ndoa linafanyika mara kwa mara na hapa endapo mwanaume huyu ana umri wa chini ya miaka 35. Ugumba pia unatafsiriwa endapo mume na mke wapo pamoja kwa miezi sita na tendo la ndoa linafanyika kama kawaida na mke ana umri wa zaidi ya miaka 35.

Kwa hiyo wewe hapa unaweza kuangalia unaangukia wapi. Ugumba pia ni pale ambapo mwanamke anapata mimba halafu zinatoka chini ya miezi mitatu na zimetoka mbili zenyewe katika vipindi tofauti ndani ya mwaka mmoja. Hebu

jichunguze hapo upo wapi. Ugumba tunauelezea kwa undani kwamba mtu anaweza kuwa na historia au la, kama mwanamke alishawahi kupata mimba au mwanaume alishawahi kumpa mimba mwanamke hapo nyuma inawezekana haya yametokea kwa uliye naye au mtu mwingine. Mwanaume au mwanamke anaweza kuwa mgumba, jambo la msingi ni kufanyiwa uchunguzi kwa daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama na afya ya uzazi.

DALILI ZA UGUMBA

Pamoja na kutopata watoto au kutopata ujauzito katika kipindi muafaka, mwanaume mgumba hukabiliwa na changamoto za upungufu wa nguvu kiume, kuwahi kumaliza tendo la ndoa, kutoa manii nyepesi, maumivu ya korodani na yutiai za mara kwa mara. Mwanamke mgumba hulalamika maumivu ya chango yaani kuumwa na tumbo la uzazi mara kwa

mara, maumivu ya hedhi, maumivu ya tendo la ndoa, kutosikia raha ya tendo la ndoa, kutokwa na uchafu na muwasho ukeni. Pamoja na yote haya mwanamke anaweza kuwa na historia ya matumizi yasiyo sahihi ya dawa za kuzuia mimba au utoaji au kuharibikiwa na mimba.

UCHUNGUZI NA TIBA YA UGUMBA

Tuone madaktari bingwa wa magonjwa ya kina mama kwa uchunguzi wa kina katika kliniki maalum zilizopo sehemu mbalimbali nchini. Uchunguzi utazingatia historia ya tatizo na mahusiano na tiba za awali. Baada ya kukamilisha hayo tiba itatolewa, matokeo ya tiba ni kupata ujauzito ambao unaweza kuwa wa mtoto mmoja, mapacha au zaidi.

NJIA KUU MBILI ZA KUPATA MAPACHA

Zipo njia kuu mbili zinazokuwezesha kupata mapacha, kwanza ni jinsi ya kupata mapacha bila  dawa au tiba yoyote na pili ni jinsi ya kupata mapacha kwa kutumia dawa au tiba maalum.

itaendelea wiki ijayo.


Loading...

Toa comment