Jifunze Zaidi

 

students.jpgNatumaini mpo salama na mnaendelea vyema na masomo yenu kwa kipindi hiki cha mwanzo wa muhula wa masomo. Nafahamu kuwa kipindi hiki ndiyo wanafunzi wengi wanaanza kuona ugumu wa baadhi ya masomo ambayo kwa mwaka uliopita waliona masomo yakiwa na ahueni kuliko hivi sasa.

Kuna wale ambao wameanza kujiweka sawa kwa kuendana na ugumu huo kwa kujisomea kwa bidii na kuojiongezea mazoea ya kujifunza zaidi, lakini pia kuna wale ambao wameanza kukata tamaa na masomo yao, hawa ndiyo hasa ningependa niwahusie kupitia makala haya.

Kimsingi mwanadamu ameumbwa na maamuzi binafsi anapokutana na jambo gumu au changamoto fulani, kwa  mwanafunzi changamoto hizi zinaweza kuwa nyingi sana lakini kwenye kujifunza, changamoto kubwa huwa ni hii ya ugumu wa masomo fulani na hofu ya kufeli.

Mwanafunzi anapokutana na somo gumu huweza kuamua kupambana nalo mpaka aliweze au kuachana nalo japo kuwa uamuzi huu unaweza ukawa na unafuu kwa wale ambao wamefikia levo ya kuchagua kombinesheni ambapo huweza kuyaacha masomo fulani yanayowasumbua na kujichagulia yale waliyoyamudu, mfano mwanafunzi aliyeshindwa masomo ya sayansi na kufaulu masomo ya sanaa huweza kuchagua kombinesheni ya sanaa kama atafikia levo fulani ya masomo.

Hata hivyo, kwa wale ambao hawajafikia hatua hiyo au wameipita hawawezi kuchagua chochote na hawana njia nyingine zaidi ya kupambana na masomo hayo magumu na kuhakikisha wanafaulu la sivyo watafeli na mwishowe kukata tamaa kabisa na masomo yao.

Hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa wanafunzi ambao licha ya kuchagua masomo ambayo waliamini angalau wanayaweza, wanapojikuta masomo hayo yanakuwa magumu kila kukicha na hivyo kujikatia tamaa na kufeli.

Hali hiyo huwakuta wanafunzi wengi lakini kitu cha msingi cha kufanya kama mwanafunzi ukiwa katika changamoto hii, kwanza kabisa ni kujipanga taratibu kwenye masomo yako na kuweka mikakati madhubuti ya kujifunza upya kuanzia kitu ambacho hauelewi hata kama kidogo vipi.

Pili, unapokuwa katika hali kama hii ni hatari kama utatumia njia tofauti za kujisomea nilizowahi kuziandika kwenye makala yaliyopita, pia unatakiwa kujitoa kwa moyo wote kwenye somo unaloliona linakutatiza kwa kutumia muda mwingi kujenga mazingira ya urafiki nalo na siyo kulichukia kama ambavyo wanafunzi wengi hufanya na kujikuta wakichukia kuanzia somo na mwalimu wake jambo ambalo ni hatari kwa mwanafunzi mwenyewe.

 

Loading...

Toa comment