The House of Favourite Newspapers

Jimmy Mafufu: Hata afe Ray sitamzika

0

jimmyymafufucut.jpgMkongwe wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu.

Imelda Mtema

HATARI! Mkongwe wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu ameonesha hisia kali baada ya kutoa kiapo kuwa hatahudhuria msiba wa msanii yeyote, hata afe Vincent Kigosi ‘Ray’ kufuatia wasanii kutompa ushirikiano wakati wa kifo na mazishi ya marehemu baba yake mzazi, Mchungaji Mafufu.

RAY65Staa wa filamu nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’.

Akizungumza na gazeti hili kwa uchungu, Mafufu alisema hivi karibuni alifiwa na baba yake mzazi lakini aliumizwa sana baada ya kupigiwa simu ya pole na wasanii wawili tu, wakati yeye muda wote alijitoa kwenye misiba ya wenzake.

“Jamani sikuwa najua wanadamu ndivyo tulivyo, mimi ikitokea kuna msiba kapata msanii mwenzangu, ni rahisi kuwakusanya wasanii wenzangu Leaders na hata kuchangishana lakini kwangu kumekuwa kama hakuna kitu kilichotokea kabisa, nimepigiwa simu na JB na Wolper peke yao,” alisema Mafufu.

Kutokana na hali hiyo, Mafufu alisema hatakanyaga kwenye msiba wa msanii yeyote, awe Steve Nyerere, Aunt Ezekiel, Johari au wengine kwa kuwa amejifunza kwa alivyofanyiwa.

“Yaani hili ni tamko rasmi, sitakanyaga kabisa kwenye msiba wa msanii yeyote, afe Ray, Aunt, Johari na yeyote yule sitokanyaga kabisa” alimalizia Mafufu.

Leave A Reply