The House of Favourite Newspapers
gunners X

Jini Mauti-19

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

“Tulikubaliana vipi?”
“Nimezidiwa mpenzi, naomba unionee huruma.”
Wakati akiniambia hayo, hakuwa ameacha kufanya alichokuwa akikifanya, aliendelea kuudadisi mwili wangu.

Hali iliyoniweka katika hali mbaya na mimi kuanza kutoa miguno.Nilishindwa kumzuia, alionekana kuwa na nguvu, baada ya dakika chache, wote wawili tulikuwa watupu na yeye kuanza kufanya alichotaka kukifanya. Nikaanza kuyasikia maumivu makali chini ya kitovu, mchezo ule sikuuzoea, lakini ghafla huku akiendelea kufanya mchezo huo, nikaanza kumuona akianza kutetemeka huku akigugumia kwa maumivu makali.
“Mudi…” niliita.

Hakunijibu, aliendelea kutetemeka na kugugumia kwa maumivu, mara nikaanza kuyaona macho yake yakibadilika na kuwa mekundu, kwa kweli nilishtuka, sikuamini kile kilichokuwa kikiendelea.

Nikamsukuma pembeni, alizidi kutetemeka zaidi. Niliogopa kile kilichokuwa kimetokea, nikamshika na kuanza kumuita lakini hakuitikia zaidi ya kutetemeka kama mtu aliyekuwa na kifafa, hapohapo akaanza kutokwa na mapovu yaliyochanganyikana na damu mdomoni.

“Mudi…Mudi….” nilimuita lakini hakuitikia, macho yake yakabadilika, yakatoka katika rangi nyekundu na kuwa meupe kabisa, mwili ukakakamaa na wala hakuchukua muda mrefu, akatulia tuli, akawa amekwishafariki dunia.

Nilichanganyikiwa mno, kile kilichokuwa kimetokea kwa Mudi ndicho kilichotokea kwa Thomas kipindi cha nyuma. Sikujua ningefanya nini, nje ya chumba kile kulikuwa na watu wengine, kulikuwa na ndugu zake ambao waliniona wakati nikiingia naye.

Sikujua ningetoka vipi pasipo kugundulika. Kiukweli nilichanganyikiwa kupita kawaida. Nilichokifanya ni kuvaa nguo zangu, ndani hakukuonekana kuwa salama tena, ili niweze kuepuka kesi ya mauaji ilikuwa ni lazima niondokemle chumbani.

Sikutaka kujiuliza sana, nilichokifanya ni kutoka chumbani humo. Kitu kilichonishangaza, niliwaangalia ndugu zake wale, hawakuonekana kama watu waliokuwa wakiniona, nilisogea mpaka pale walipokuwa, nikawaaga lakini wakawa kama watu wasionisikia au kuniona kabisa, nilichokifanya ni kuondoka, tena nikikimbia kwa mwendo wa kasi.

“Nimeua,” nilisema huku nikikimbia, jasho lilikuwa likinitoka.
Nilipofika nyumbani, nikaingia moja kwa moja ndani. Nilikuwa nikilia mno, mama ambaye alikuwa nje akaingia ndani na kunijulia hali kwani alishangazwa na kile kilichokuwa kimetokea, kufika nyumbani usiku tena huku nikikimbia, hakika aliogopa.
“Davina…kuna nini?” aliniuliza huku akionekana kushangaa.

“Niache mama, niache…”
“Niambie kuna nini.”
Sikutaka kumjibu, nililia mno, sikuamini kile kilichokuwa kimetokea kwamba Mudi alikuwa mtu wa pili kufa katika mikono yangu. Hapo ndipo nilipopata picha kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.

Haikuwezekana watu wawili wafe kipindi walichokuwa wakifanya mapenzi na mimi, nilihisi kulikuwa na kitu ambacho bibi yangu alikuwa akikifahamu.
Usiku wa siku hiyo sikulala, nilibaki nikilia tu. Sikutaka kwenda uwanjani kukutana na wachawi wenzangu zaidi ya kukaa tu nyumbani. Ilipofika usiku bibi na wachawi wengine wawili wakafika chumbani kwangu.

Kitu cha kwanza kabisa kukifanya ni kuviinamisha vichwa vyao mbele yangu kisha kunipongeza kwa kazi niliyokuwa nimeifanya ya kumchukua mtu wa pili na kumpeleka kule kulipokuwa na kundi kubwa la misukule.

“Kwa nini mimi?” niliuliza huku nikilia.
“Wewe ni kiongozi wetu.”
“Ndiyo niue? Sitaki kuua.”

Nilisema huku nikilia mno. Hawakuniambia kitu chochote kile zaidi ya kuondoka. Katika kipindi chote hicho sikuwa nikijua kwamba bibi yangu aliniwekea jini mauti mwilini mwangu.
Je, kilifuatia nini? Usikose mwendelezo wake wiki ijayo.

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO, BOFYA HAPA ===>https://www.facebook.com/shigongotz/

Leave A Reply