JINI MTU-03
Kwa mbali kabisa nikiwa sielewi A wala B fahamu zangu zikiwa zimepotea, lakini kama nukta kumi ama kumi na moja nikawa huru katika mikono ya yule kiumbe, nikawa nahema kwa tabu, nukta nyingine za kuhesabika nilihisi kama nashikwa mkono wangu wa kulia kwa kiganja kipana na kikubwa, halafu nanyanyuliwa kwa juu kwa nguvu nyingi, nilihisi naning’inia angani, huku mkono wangu wa kulia ukiwa umekamtwa kwa nguvu hadi mbavu zikawa zinauma..
Nilifumbua macho..
lahaula lakwata!. nilikuwa nimebebwa na kile kiumbe umbali wa mita takribani elfu tano angani.!
Hata macho yangu nilipotizama tena chini, niliona mji wa Kigoma kama kakijiji tu kadogo huku mataa ya umeme ya mji yakionekana kama mwanga wa vimuli muli ama vibatari vya wavuvi wanao onekana wakiwa maili nyingi nyakati za usiku katika bahali..
“Mungu uko wapi wewe mungu wewe!. ona sasa hii nini sasa aaagh?” nililalama kibwege, nikajaribu kufurukuta lakini nikajikuta najisababishia maumivu mwenyewe kwani ule mkono wa yule kiumbe mwenye kupaa ulionekana kama sumaku, vile vile kuendelea kuleta usumbufu kwa kile kiumbe ni kujihatarishia maisha pengine hata kwa kuniachia ambapo nikianguka huko ardhini na kujibamiza, ni wazi, nitapasuka vipande vipande.
Kiumbe alizidi kwenda angani zaidi huku akienda kwa spidi kali mvumo wa upepo ukazidi kunitesa japo kule hapakuwa na mvua, kila lilokuwa linajili mbele yangu kwa kila wasaa ilikuwa ni kama zile hadithi za Aladini na taa ya ajabu ama hadithi za mazimwi nimilzowahi kusimuliwa na babu yangu angali mdogo.
Na mpaka wakati huo, sikujua nini maana ya matukio yale. ****
Sijui ni muda gani ulitumika nikiwa naningi’inzwa angani mithili ya kifaranga cha kuku kilichobebwa na mwewe.
Ninacho kikumbuka nilijikuta nipo katika eneo fulani lenye joto kali na giza totoro bila shaka ilikuwa ni katika chumba kidogo, nasema ilikuwa ni katika chumba, kwa sababu hewa ya eneo hilo ilikuwa nzito na ndogo, katika papasa papasa yangu ya huku na kule kuna wakati niligusa kitu kama geti la chuma lililoKuwa limefungwa imara.
Wakati huo huo nilisika harufu ya nyama kama zilizo kuwa zikibanikwa, vilevile kwa mbali kulisikika sauti za kutisha na ngurumo nzito.
Lakini pia, wakati mwingine nilisikia sauti za watu wakiimba lakini nyimbo zilizo imbwa zilikuwa za hovyo hovyo zisizo na mvuto katika masikio ya mtu yeyote ambaye angepata bahati ya kusikia aina zile za za nyimbo..
Hii nini hii? kwanini haya yanatokea? ndio kusema nipo kwa mashetani sijui ujinini? kwanini niwe mimi?na kosa letu ni lipi hasa dhidi ya hawa mashetani? na wenzangu wengine wako huku? na kama wako huku wazima ama ndio washakufa kama Mpemba? na kama hawapo huku watakuwa wapi? yote ni maswali yaliniandama akilini mwangu, sikupata aina yoyote ya majibu.
Hadi wakati huo niliona ni kama ndoto tu mbaya ya kutisha inayo nipitia nikiwa katika usingizi wa pono, haiwezekani hadithi za mazimwi nilizo wahi kusimuliwa, eti leo iwe ndio maisha halisi ninayo kutana nayo!
Nikiwa bado katika tafakuli mara kishindo kikubwa kilisikika umbali fulani umbali ambao nilikuwa napata kusikia zile sauti za ajabu ajabu na nyimbo zisizo eleweka, na hata kile kishindo kilipo sikika mara ghafla ukimya ulitawala eneo zima kama kwamba palikuwa hakuna makelele ya aina yoyote eneo lile.
Mara nilisikia nyayo za kitu kikiwa kinakuja usawa ambao mimi nilikuwa nipo. Mtembeaji alifika hadi katika geti la chumba nilicho kuwa nimefungiwa kisha nikasikia chakara chakara za kufungua geti, kiumbe huyo sikuweza kumwona kabisa kutokana na giza lililokuwapo mule ndani.
Mara nilihisi kuguswa kwa kiganja cha yule kiumbe kisha nikashikwa kwa nguvu na kuvutiwa kwake.
Nilijikojolea.
Yule kiumbe alinikamata mkono pasina kuongea neno lolote kisha akawa ananiburuta kunipeleaka nisipo paelewa.
Nikiwa navutwa na yule kiumbe, yeye mbele, mimi nyuma, hatua kama kumi na mbili, tulifika eneo lenye mwanga wa mioto, ilikuwa ni vigingi vya mioto iliyo washwa kama mwenge na kuwekwa pembezoni mwa ukuta ambapo kulikuwa na sehemu malumu ya kushikia vile vingingi.
Kitu nilicho kigundu eneo lile, ni kwamba pale nilipo pelekwa palikuwa ni pangoni, kutokana na mzingira niliyo yaona ila sikujua ni mapango ya eneo lipi, kwani pamoja na kwamba kuwa ni mzawa wa Kigoma sijawahi kusikia eneo fulani kuna mapango, hivyo sikujua kabisa nipo katika mapango yaliopo eneo gani.
Yule kiumbe alikatisha kona kama mbili kisha tukatokea katika eneo pana kidogo ambapo kulikuwa na mazingira kama ya jiko huku upande wa kushoto mwa eneo lile kulikuwa na binadamu wa kawaida na majiko makubwa yalikuwa yamebandikwa masufuria makubwa huku kuni zilizo kuwa zikichochowe na wapishi hao binadamu zikiwaka kwa kasi.
Kulia mwa eneo lile kulikuwa na meza kubwa iliyo kuwa imetapakaa damu na nzi wakiwa wengi, na mbele yangu kulikuwa na chumba kidogo kilicho fungwa kwa kigeti kidogo chenye nondo ngumu, pia kilikuwa kimefungwa kwa kufuli imara.
Macho yangu yalirejea kwa wale binadamu wenzangu, sura zote zilikuwa ngeni, lakini moyo wangu ulipata ahueni kidogo kwani matumaini ya kukutana na binadamu wenzangu, tumaini lilijijenga moyoni mwangu kuwa uhai upo, japo sikujua kivipi watu hawa wawe huku tena wanaishi na viumbe wa ajabu kama huyu aliye nishika mkono tena bila wasiwasi wowote.
Wale watu hawakuonyesha kunijali hata kidogo. “heloooo!” nilitoa sauti kwa wale watu kuwaita, walicha kidogo kuchochoe kuni wakanitizama, “jamani huku wapi ninyi?” niliuliza, uso wangu nikufanya wenye huruma mbele ya macho ya wale binadamu waliokuwa wamevalia nguo nyepe za kimapishi huku kichwani wakiwa na kofia nyeupe za duara, badala ya kunijibu wale watu miongoni mwao mmoja akamuuliza swali yule kiumbe, swali kwa rugha ya kiswahili, swali ambalo lilinikata maini, alisema, “vipi huyu nae binadamu jini kwani nyama yake siku hizi inaliwa?”
Ebwana weee! nilihisi wazimu unaniingia na kutoka! kama kuna siku mapigo yangu ya moyo yameenda kasi basi haishindi siku hii, kwani moyo ulinidunda kama mdundiko wa kizalamo!
Asalimia mia moja yule mpishi alihoji kuhusu mimi, japo katika baadhi ya maneno yake kuna neno ambalo sikujua nini maana yake ‘BINADAMU JINI’ yanii mimi ni mtu jini?.
Sikuelewa hapo.
Kwa mara ya kwanza nikasikia sauti ya yule kiumbe, asauti ilikuwa nzito haswaaa tena iliyo endana na mwonekano wake, jibu lake lilinifanya akili yangu ipoteze kabisa uimara kwa lugha ya kiswahili alimjibu hivi,
“Hapana, nyama yake hailiwi! huyu mchinjeni kisha mumbanike nyama yake itatumika kwa majaribio ya kutengeneza dawa ya ugonjwa wa Anofobia”
Nilianza kulia kama mtoto, nikawa nafurukuta kujinasua katika mikono ya kile kiumbe,lakini kiganja cha lile dubwasha kilinikamata imara kweli kweli. Alikuwa ni kama amekamata kifaranga cha kuku.
“Uwiiiiiii!..nakaufaaa mamaaa” nilipiga mayowe nikijinyonga na kulisuka suka lile jitu hata kwa kulivulumushia makonde, lakini ilikuwa ni kama namkuna tembo! Kwa jani la ufagio, haikutosha nikasogeza meno yangu katika mkono ule ulio nikamata kisha nikamuuma meno kwa nguvu.
Lakini wapi.
Ngozi ya lile jitu ilikuwa ngumu kama ya mamba!.
Nilivutwa kwa mvuto wa kawaida na yule kiumbe nilijibamiza katika vitu vilivyo kuwapo sakafuni kana kwamba nilivutwa kwa nguvu nyingi, kusema ukweli sijawahi kuona dude lenye miguvu kama lile!.
Nikakokotwa hadi katika chumba kilicho kuwa mbele yangu, kisha yule kiumbe akafungua akiniachia mkono, akawa anafungua kufuli la pale getini.
Nikakurupuka na kutoka ‘mkuku’ huku nikipamia vitu vilivyo kuwa ‘shabarabaghala’, ajabu ni kuwa hakuna mtu aliye hangaika na mimi, yanii naweza nikasema wale watu walikwisha zoea kuona purukushani za watu eneo lile, hakuna aliye jali mbio zangu, kila mtu aliendelea na shughuri yake, hata yule kiumbe pia, aliendelea na kufungua lile kufuli pale getini.
Nilichoropoka mule ndani, nikapita katika kona mbili tatu, kisha nikatokea katika kijinjia chembamba ambacho kilikuwa na mioto inayo waka kama mwenge, nikazidi kukimbia kwa kasi kuelekea mbele, kasi niliyo kuwa nayo bado niliona haitoshi kwani suruali yangu nayo ilikuwa inanisumbua ilikuwa inavuka.
Kama ingetokea bahati ya kuniona, ungeshuhudia namna nilivyo kuwa nikitweta hovyo, mkono wangu nikiwa nimekamatilia suruali yangu iliyo kuwa inanivuka, huku kila sekunde nikigeuza macho yangu nyuma kuona niko umbali gani dhidi ya adui aliye taka kunichinja na nyama yangu kuibanika!. eti nyama yangu itafanyiwa majaribio ya ugojwa wa anofobia, ugonjwa ambao sijawahi kuusikia hapa duniani.
Nilizidi kujisukuma kwa mbele, huku nikihema kwa pupa hofu ikiwa kwa kiwango cha mwisho kabisa.
Nikiwa umbali fulani mara nikawa nasikia zile sauti za ajabu ajabu na nyimbo zisizo eleweka, kile kinjia kilikuwa kirefu hata nisiweze kuona mwisho wake, na mita kama kumi niliona kuna kona upande wa kulia, nikaongeza kasi nifike katika kona ile ili niachane na ile njia iliyo nyooka, kwani kuendelea kukimbia nikiwa katika njia ya namna ile isiyo onekana mwisho ni hatari.
Vilevile kama mtu angesimama mwanzo wa ile njia basi lazma angeweza kuniona kwa mbali nikiwa nakimbia kiwazimu.
Nikaongeza kasi ya mbio kuifikia ile kona.
Ile nafika tu…!
Ghafla..
Nilijikuta nanyakuliwa kama kifaranga cha kuku!. Nilikuwa nimeshikwa na mkono, lakini mwenye mkono hakuonekana.!
Mkono ulikuwa mrefu kama kamba, ule mkono ukawa unanivuta kunipeleka mahali, na kadri ulivyo kuwa ukinivutia mahala ndivyo ulivyo kuwa ukipungua, ukisinyaa.
Ulikuwa mkono wa yule kiumbe..
Ule mkono ukanirejesha hadi mbele ya yule kiumbe wa ajabu.
Nilichoka.
Nilibaki nikitweta macho yangu yakiwa yametapakaa hofu.
Yule kiumbe alinisukumia katika kile chumba kisha akafunga geti paaa!.
Kumbe ndio maana hawa watu hawakuhangaika na mimi kunikimbiza uwezo wao ulitisha
Ndani ya chumba pweke, hapakuwa na kitu chochote mule ndani, chumba kilikuwa tupu, ni upande wa kulia tu kulikuwa na dirisha lililokuwa na urefu wa mita kama kumi na mbili kwenda juu ambalo lilikuwa likitizama huko nje ambako kuna wale wapishi wa kibinadamu walio kuwa wakipika.
Moshi wa kuni na vyakula vilivyo pikwa huko nje yote iliingia ndani kupitia lile dirisha, harufu kali na mbaya ya vitu vilivyo pikwa ilikuwa ni yakipekee kwani sikuwahi kuisikia mahala popote.
Niliegemea ukuta taratibu nikajikuta nachuchumaa huku nikiburuza mgongo wangu katika ukuta hadi chini miguu nikiwa nimeikunja sambamba na kifua changu.
Bado kichwa changu kilikabiliwa na vitendawili lukuki,
Kiasi cha kama dakika therathini na ushee zilikatika kukiwa na kimya kama kwamba hakuna kinacho endelea.
Je, nini kitaendelea?
Tukutane Jumatatu hapahapa.
Comments are closed.