The House of Favourite Newspapers

JINI MTU-05

Mapafu…mapafu yanauma…yanashindwa kufanya kazi? yanapata moto…pumzi..pumzi hakuna kabisa…..

 Oooh my god  kumbe hivi ndivyo inavyo kuwa roho inapo mtoka mtu?aah,pumzi jamani pumz, .yanii nipo kama kwenye…niko kwenye…MAJI

   Nilifumbua macho ghafla na kufunua mdomo wangu na kuvuta hewa nyingi ili niyape ahaueni  mapafu yangu, badala yake nilijikuta nikibwia maji mengi na kutapatapa kwa namna halisi ya mfa maji, nikahisi nikizidi kuzama zaidi katika kina kirefu cha maji nikiamini nimeangukia katika dimbwi kubwa la maji ama mtoni katika eneo lile la kishetani.

Kwa dakika za kuhesabu nilijikuta nimenasa katika  gogo kubwa lililokuwa limekaa umbo la ‘Y’  hakika hilo ndilo lililo nizuia nisizidi kupelekwa na maji yaliyo kuwa yanatiririka kwa kasi.

Niliinua uso wangu juu na kutizama kule niliko tokea ,lakini sikuona chochote zaidi ya miti mikubwa na mirefu iliyo funika anga,  eneo lote  lilisheheni giza, kikohozi cha mfululizo kilinishambulia  huku maji yakinitoka mdomoni na puani  pomoni “mmh maajabu ya Musa haya..huku niko wapi mimi Vegasi? hawa mashetani wananiondoa duniani, bloody coward.

Niliinamisha  kichwa na kujitizama katika lile jeraha la kisu, woga mkubwa ulinijaa pale nilipo ona maji katika ule mto yamebadilika rangi na kuwa nyekundu kutokana na damu iliyokuwa ikivuja katika lile jeraha la kisu.

Ooo!Yailah.. natokwa na damu nyingi ndio maana nguvu zinaniishia, nakufa mimi jamani.. nafaa!. Nilizidi kupambania rohoho yangu.

Kwa tabu nilijivuta katika lile gogo lenye muundo wa ‘Y’ ili nijaribu kujichomoa katika lile gogo na kujitupa pembeni ya mto ule.

Lilikuwa kosa, kwani hapo nililitikisa lile gogo  na nililichomoka na kuanza kusombwa na maji kwa kasi.. sikuwa najua kuogelea lakini zaidi sikuwa na nguvu kabisa, nilicho fanya nilijivuta karibu kabisa na lile gogo na kulikamatilia kwa nguvu  likiwa ndio kama boya langu katika ule mto mrefu kabisa.

Sasa nikawa napelekwa na maji kwa namna ile kwa umbali mrefu kabisa,  hata dalili ya maji kupungua haikuonekana, maumivu katika jeraha yalikuwa hayamithiliki.

Mara mbele yangu mita kama kumi na sita niliona ule mto ulikuwa ukiishia katika mpolomoko mkubwa mithili ya victoria fall..

Yanii ndio naenda kufia huko, niliwaza.

Nilijikuta napiga kelele na kujikuta nikizidi kulinga’nag’ania lile gogo lenye umbo la ‘Y’ nilivyo zidi kukaribia katika mpolomoko ule niliona mawe makubwa yaliyo kuwa ukingoni.

“Mungu fanya kitu sasa hapa..fanya kwa wakati usikawie  Mola wangu… nisaidie mja wako.. huku sasa ndio nakwenda kufa”    

    Nilizidi kunong’ona kiwazimu.

Akili moja ilinijia kuliongoza lile gogo katika yale mawe yaliyokuwa ukingoni mwa ule mto.. sasa nikawa nalisukuma kwa nguvu kidogo nilizo kuwa nazo lakini wapi, maji yalikuwa na kasi na nguvu kubwa kuliko mimi, sikukata tamaa nikaendelea kulisukuma lile gogo kwa nguvu zangu zote zilizo kuwa zimebakia.

lakini wapi..

Na wakati huo huo nilikuwa nimekwisha fika katika mpolomoko mrefu kabisa..”AAAAYAAAAAH” Nilipiga ukelele wa woga.

Nikajikuta napolomoka katika mpolomoko mwingine mkali kabisa ambao nafikiri ulikuwa na umbali wa mita kama mia na sabini kwenda juu, nilitumbukia  tena kwenda chini kabisa “pwaaaaaaaaa” nilifika chini na kujibamiza katika maji ambayo yalitoa kishindo kikubwa na kutawanyika,wakati huo huo nilijipiza kichwani katika jiwe  na hapo hapo niliona giza likitanda machoni mwangu..

****

Sikujua fahamu zilinirudia baada ya muda gani au baada ya siku ngapi kwani kichwani mwangu nilikuwa nikipitiwa na taswira nyingi za ajabu ambapo zilifuataiwa na vipindi virefu vya  kiza na utupu mrefu akilini,miongoni mwa yale yaliyo pita ni tukio la wachezaji wenzangu kuliwa nyama kama mishikaki na viumbe wa ajabu kabisa, jingine ni la wale viumbe kunisujudia  huku wakizungumza maneno nisiyo pata kuyaelewa.

Maumivu makali yaliutesa moyo wangu haswa pale nilipotaka kukumbuka hata jina langu lakini nikashindwa, niliishi maisha ya tabu sana katika siku za ukubwa wangu, kila kitu kwenye maisha yangu kilikuwa kipya kabisa, sikumfahamu yeyote katika eneo lile.

Sikukumbuka nilipokuwa wala nilifikaje, sikufahamu chochote kuhusu ulimwengu, kila kitu kilikuwa ni giza ndani ya maisha yangu, sikutamani kufa kwasababu sikujua nini maana ya kuishi na nini faida ya kufa kwa wakati huo, kwa kweli yalikuwa maisha ambayo sikuwahi kufikiri kama ningeishi.

Niligombea chakula na kunguru katika majalala maeneo mbalimbali ambapo sikujua ni wapi,.

Mwehu, kichaa,na chizi ndiyo yalikuwa majina niliyo itwa na watu, Kwangu ilikuwa ni mahala popote, chakula changu, ilikuwa ni kitu chochote ambacho nitaona kiumbe yoyote anakula awe mbwa,paka au binadamu.

Lakini hata hivyo, Sikupenda kukaa karibu na binadamu kwani niliwaogopa, niliishi peke yangu katika magofu na vichochoro,nilicheka peke yangu nilipojisikia kucheka, na niliongea peke yangu nilipo tamani kuongea,.

Niliupenda usiku kuliko mchana kwani usiku ulipo ingia na kulala usingizi sikuwa mimi niliye itwa MWEHU nilikuwa mtu mkubwa mwenye heshima kubwa kwa jamii fulani nisiyo pata kuifahamu.

Lakini kila kitu kilibadilika nilipostuka kutoka katika usingizi  na kufumbua macho yangu ni hapo ambapo kichwa changu kinagubikwa na giza zito na kuwa binadamu nisiye elewa lolote.

Hayo ndiyo yalikuwa maisha yangu kwa masiku mengi mno katika dunia hadi siku moja nilipo patwa na hali fulani ambayo nilishindwa kufahamu nini kilifanyika katika mwili wangu..

*** 

   Masikio yangu yalikuwa katika mkanganyiko mkubwa,mkanganyiko dhidi ya nzi waliokuwa wakicheza gwaride katika sikio langu na kusababisha misisimko  yenye karaha kubwa,.

Hali ile iliondoa utulivu kabisa kwangu

nilijaribu kutikisa kichwa changu lakini wapi! kichwa kilikuwa kizito ajabu!

Hata nilipojaribu kuinua mkono wangu ili niwaswage wale wadudu nilihisi mikono yangu ikizuiliwa kutenda agizo langu,.

Lakini hata hivyo atimae nilifumbua macho kivivu.

Macho yangu yakakutana na sura ya mwanadada aliyekuwa ameninamia huku akitabasamu ilihali kwa mbali nikisikia muziki wa heart break hotel wa Elvis Presley.. nimekufa na mungu ameniingiza peponi,niliwaza.

 Wakati huo macho yangu yalitua kwa yule mwanamke aliyekuwa akinitizama huku tabasamu zuri lilloacha mashavu yenye vishimo katikati likisafisha uvulivuli wa macho yangu.

     “Peponi kuna wadada wazuri hivi loh!

Niliendelea kuwaza.

Mkononi akiwa na kiredio kilicho kuwa kikilia nyimbo za Elvis Presley nikiwa shabiki nambari moja kwa huyo mwanamuziki.     “kumbe kwa Mungu huwa kuna miziki ya Elvis Presley?”  niliuliza kwa sauti iliyo kwaruza  na macho yaliyo regea  huku nikiendelea kumtizama yule mdada mwenye urembo uliotukuka.

Yule mrembo alizidi kutabasamu kabla ya tabasamu lake kupanda cheo na kuwa kicheko kidogo kilicho acha kinywa chake wazi na kumafanya azidi kuonekana mrembo haswaa, niliona meno mazuri meupe yaliyo pangana  vizuri na kuacha kijmwanya kidogo kizuri  katikati.

“Hapa ni nyumbani Katubuka Manguruweni Kigoma.. siyo mbinguni Vegas” alisema  huku akinitizama kwa macho yake malegevu tabasamu kubwa likichanua kinywani mwake.

Naitwa Nasra ndiye mtu ninayekusaidia  katika matibabu yako, ni mimi ambaye ndiye nakuwa na wewe muda wote kuangalia afya yako,”   aliongea huku akionekana kuangalia pembeni..nikamwona akipangusa machozi katika macho yake.

  “Kwanini unalia” nilimuuliza huku nikimgeuza ili aniangalie.

“Silii ni furaha tu kwakuwa umeamka leo

Alisema huku machozi yakiendela kumbubujika.

Kichwa changu kilikuwa kimejaa maswali mengi sana, lakini sikujua namna ya kuyauliza, kila kitu pale kilikuwa ni michoro kwangu isiyoashiria chochote, nilikuwa nimevurugwa akili na kila kitu kabisa.

Sikumfahamu yule mwanamke aliye jiita Nasra na wala sikujua yeye ni nani, sikujua anaposema nimeamkaje, nililala toka lini, na kwanini kuamka kwangu kuwe ni furaha kwake , kwanini alionyesha furahakuamka kwangu, yeye alikuwa nani kwangu, mimi nilikuwa na thamani gani kwake, hiyo yote ilikuwa ni kitendawili ndani ya kichwa changu.

Nilikuwa kama teja lililokuwa likihudhuria kliniki ya ukichaa.

   Binti yule mwenye kufanana na mwanamke wa urembo alinishika kichwa changu ba kukilaza katika kifua chake kilicho kuwa kimebeba matiti makubwa ya wastani yaliyo banwa vizuri kwa sidilia,”  unaishi na nani hapa?”  niliuliza huku nikijitoa katika katika kifua cha yule mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Nasra.

“Naishi mwenyewe lakini kwasasa nitakuwa nikiishi na VEGAS” aliongea hayo na kucheka, Kwa muda mfupi niliokuwa na Nasra nilikuwa nimegundua kuwa alikuwa mtu mwenye kupenda sana kucheka.

Alikuwa ni mtu mcheshi na anayependa utani muda mwingi.

Nilianza maisha haya ya kuishi kwa Nasra,.

   Nilimtizama sura yake nikiingiza katika ubongo wangu kidogo sura yake kama niliwahi kuiona mahala lakini sikumbuki ni wapi.

   “Ngoja nikutayarishie chakula Vegasi.”  Alisema tena  yule mwanamke mwenye kiuno chembamba kilicho jikata vizuri na kutengeneza umbo la namba nane kwenye mwili mwanamke yule..

    Ndani ya dakika hiyo hiyo  akaingia mtoto mdogo wa miaka mitatu..mtoto mzuri wa kike  mwenye kufanana na mwanamke wa yule..mtoto mzuri mchangamfu.

    Ooh kumbe mwanamke wa urembo ana mtoto

Niliwaza.

Nasra alimbeba mtoto wake huku akinitizama kwa mashaka kidogo na kutoka nje kwa minajili ya kwenda kunitayarishia chakula japo sikuwa na hamu na chakula chochote.

Mule ndani bado nilikuwa sijapata uimara katika akili yangu, tangu nimepata fahamu ubongo wangu ulikuwa tupu kabisa hakuna nililo kumbuka hata moja, nilitizama mazingira yale niliyo kuwapo, kilikuwa ni chumba kidogo kilicho kuwa na vitu vichache mule ndani vilivyo pangwa vizuri,

Meza ndogo ya kulia chakula mabegi ya nguo yaliyo kuwa katika kona ya kushoto ya chumba, kiruninga kidogo cha hitachi kilikuwa mbele ya kitanda nilicho lalia,

Macho yangu yalitua katika picha nyingi zilizo kuwa katika chumba kile,ni picha  kubwa ya mama mtu mzima akiwa katika tabasamu la huruma ndiyo iliyonivutia, niliitizama kwa kiasi cha dakika nne huku nikichekecha ubongo na moyo wangu uliokuwa ukipwita mbele ya picha ile

Nani huyu mwanamke..nilimwona wapi vile..nani vile…nani…

Sikupata jibu.

Japo niliendelea kupata shinikizo moyoni la kuitafakari ile picha ambayo ilitekenya ubongo wangu kwa dakika chache nilizo pata kuiona.

    “Nani vile huyu mtu… kama namfahamu,.lakini wapi nilimwona..nani vilee nani..mama yangu..yeah nimekupata mama yangu…… eeeh mama..oooh mama yangu..” Nilipagawa.

Ilikuwa ni picha ya mama yangu mzazi, mtu muhimu kabisa katika uhai wangu hapa duniani ni hapo macho yangu yalipotua mbele ya picha nyingine kubwa iliyokuwa amepiga binti wa urembo na kijana mwingine aliyekuwa katika mavazi mazuri ya vijana wa kileo. “Nasra…ooh..Nasra mpenzi wangu,..Nasra uuuuwii Nasra!.”    

    Nilipagawa kwa furaha nilihisi kuwakosa watu hawa japo sikujua ni muda gani umepita .. hivi hii ni ndoto au kweli..isije ikawa ni ndoto halafu nikajikuta niko..niko ..niko wapi vile..wapiii..KUZIMU.

Hapo Kila kitu kilijirudia katika akili yangu kama mkanda wa filamu, toka tukiwa katika sherehe pale kizota sherehe  ya kupanda daraja na kuingia katika ligi kuu kwa timu yetu ya Joy  football club kisha tukapata ajali ya basi tukiwa tunatoka katika sherehe na kujikuta nimeingia katika mikono ya wachawi na kushuhudia wenzangu wakiliwa nyama kabla ya mimi kuangukia katika mpolomoko mkali na giza kutanda katika macho yangu hadi muda huu ambapo nipo ndani ya chumba kidogo nikiwa hoi bin taabani.

Mara mlango wa chumba ukafunguliwa akaingia  Nasra mwanamke wa urembo,  mkononi akiwa na bakuli la uji mzito pamoja na sahani lililokuwa na futari ya ndizi kwa utumbo wa  ng’ombe  tabasamu lake lilikuwa bado limechanua kinywani mwake.

“Nasra”  nilimwita huku nikitizama macho ya mwanamke huyo..niliona namna alivyo patwa na mshangao mkubwa alibaki akiwa ameganda akinitumbulia macho ya mshangao mkubwa.

Kwanini ananishanga huyu malaika wa  mrembo,

“Nasra my love” niliita tena safari hii nikitoa sauti ya juu kidogo macho yetu yakiwa yanatizamana.

Alisogea na kuweka kile chakula katika meza kisha akinisogelea pale kitandani na kunikumbatia kwa nguvu huku akitokwa na machozi.

“Hii ni miujiza.. siku zote nilijua kuwa siku moja utazinduka katika usingizi mzito lakini sikuwahi kufikili kama fahamu zako zitarejea kwa wepesi kiasi hiki”

Alisema Nasra akilia katika kifua changu, “mama yangu yuko wapi?” niliuliza.

Nasra alijitoa kifuani kwangu ilihali machozi yakiwa bado yanamtoka machoni akizidi kunitizama kwa mshangao mkubwa,.

“Kila kitu utafahamu taratibu Vegas kwa sasa pumzika kwanza”

Siku hiyo nilipata kumbukumbu nyingi mno ambazo ndani yake zilitengeneza maswali mengi ambayo sikujua niyaulizeje.

*******

Baada ya chakula cha usiku Nasra alimbeba mtoto wake na kumlaza katika chumba kingine kilichokuwamo mule katika nyumba ile ndogo lakini nzuri, badae alirudi na kubadilisha nguo mule mule ndani nilipo kuwapo mimi.

Bado sikuwa katika hali ya kawaida  pamoja na kwamba nilikuwa nimemkosa binti huyo kwa miaka mingi lakini pia nilihitaji kujua mambo mengi yaliyopita katika kipindi ambacho nilikuwa sina fahamu nzuri,.

Nasra alinisogelea pale kitandani na kuanza kunipapasa katika maeneo mbalimbali katika mwili wangu huku akionekana yupo katika uhitaji mkubwa wa penzi langu.

“Hapana nahitaji kujua kwanza nini kilitokea…”

“Shiiii…najua nini unahitaji.. lakini mambo yaliyo pita ni mengi unahitaji utulize fikra zako kwanza,.” alinikatisha huku akitia kidole cha shahada katika mdomo wake,.

“lakini si mke wa mtu wewe kwa sasa?,.una mtoto Nasra ujue.”

“Wenye watoto wote ni wake za watu Vegasi?”

“Sasa vipi hii,.. aaagh mimi sijui,..lakini si ntakuwa naiba penzi la baba wa huyu mtoto?” niliweka hoja ambayo nilijua haina nguvu mbele ya mwanamke yule mrembo mwenye kuonekana kuhitaji penzi langu kwa hali na mali,.

Hakujishughulisha hata kunijibu kabisa isipokuwa aliendelea kunichezea katika sehemu tofauti katika mwili wangu.

Nikajikuta nasombwa na misisimko ya hali ya juu, mwisho nikazama katika penzi zito kabisa la bi Nasra mwanamke wa urembo.

Asubuhi ya siku iliyofuatia alikuwa ni Nasra aliye kuwa wa kwanza kumka aliniandalia stafutahi ya mkate na chai ya maziwa,.Baada ya kupata stafutahi ile  Nasra alitumia wasaa ule kunisimulia mambo yaliyopita wakati mimi nikiwa sina fahamu
Je, nini kitaendelea?
Tukutane Alhamisi.

Comments are closed.