The House of Favourite Newspapers

JINI MTU-07

Tayari maghalibi ilikuwa imeingia kwani mwanga hafifu wa njano ulipenya katika dirisha la lockup ya polisi na kuniangazia mahala nilipo kuwa nimelala baada ya kupoteza fahamu kwa masaa Zaidi ya matano pale kituo cha polisi hali iliyo tokana na kupokea mkong’oto wa haja.

Nilizinduka nikiangaza huku na kule mule ndani palikuwa na watu wengine kama sita walioingizwa pindi nikiwa katika mshike mshike na wale polisi kule katika chumba cha mateso aidha nikiwa sina fahamu.

Nilijaribu kujinyanyua lakini mbavu zilikuwa zinauma vibaya mno, nilipeleka mkono katika sehemu zangu na kugusa nyeti zangu ambazo nilihisi yule polisi baradhuli alinipasua nikagusa, nilipata maumivu makali mno yaliyo nifanya nishindwe kabisa kukaa kitako, nikabaki vile vile nimelala kifudifudi.

Sikuwa napumua vizuri nilikuwa navuta hewa kwa tabu,hewa chafu ya kinyesi cha binadamu iliyokuwa mule selo ilinifanya nipate tabu Zaidi.

Giza likawa linaumeza ule mwanga wahafifu wa maghalibi na kufanya giza mule ndani.. Muadhini akiwa ananadi swala kule musikitini kwa mbali nikawa nahisi macho yangu yanapoteza nguvu huku giza zito mno likiwa mbele yangu pumzi zikawa zinanoitoka na kuingia kwa tabu,.

“Anakufa huyu afande,.anakufa huyuu jamaniii”

Nilisikia kwa mbali sauti za wale jamaa waliokuwa mule ndani.,

Nikajaribu kuinuka wima lakini sikuwa na nguvu hata kidogo katika mikono na miguu yangu,.

Wakati huo huo nikasikia sauti fulani ambazo niliwahi kuzisikia miaka mingi ya nyuma, nikatuliza fikra zangu kidogo ili nipate kusikia kile kilicho kuwa nakisikia, zile sauti za nyimbo za hovyo hovyo za wale viumbe wa ajabu zikalindima masikioni mwangu vizuri.

   Oooh ndio narudi kwa wale viumbe wala nyama za watu mimi

Hata wakati najalazimisha kurudi katika fahamu zangu ndivyo nilivyo zidi kupotea kabisa katika ulimwengu mwingine wa ajabu.******

 

Nilikuwa mbele ya maelfu ya watu na viumbe wengine wenye maumbo makubwa na yakuogopesha kabisa, ilikuwa ni katika eneo la wazi katika usiku wa giza, palikuwa na mioto iliyowaka kama mwenge kuzunguka eneo lile la wazi, watu wengi wakiwa wamesujudu mbele yangu kwa heshima kubwa, sikuwa na hofu yoyote nilikuwa na hasira na donge zito rohoni,

Sababu ya kuwa vile sijui.

“SIMAMA” nilitoa amri na watu wote walisimama kwa unyenyekevu mkubwa.

Nilichukua kibuyu kilicho kuwa pembeni ya kiti cha kifalme nilicho kuwa nimekalia kisha nikachukua kisu kikali kisha nikajikata kidogo katika mkono wangu wa kulia, damu nyingi zilitoka nikakinga kibuyu kile,.

Damu ikatoka nyingi na kujaa kibuyu kile.

“Zakora” niliita kwa amri, na hapo mzee mmoja mwenye mvi nyingi alinijia kwa heshima na kumkabidhi kile kibuyu kilicho jaa damu yangu.

Watu wote wakapiga makelele ya furaha,mzee Zakora akiwa amenyanyua lile buyu lenye damu yangu.

Badae nikagusa katika lile jeraha na kuzungumza maneno fulani ya lugha isiyo pata kuwapo katika hii dunia na hapo hapo lile jeraha likafutika lote, pakawa kama kwamba hapakuwa na jeraha la aina yoyote eneo lile..nikasimama eneo lile la mbele huku macho yangu yakiwa si yenye kukapua hata kidogo nikaanza kuwahutubia wale maelfu ya watu waliokuwapo katika eneo lile la uwazi.

“Watu wataishi karne nyingi kwa damu yangu..,Anophobia huu ndio mwisho wake…,hatuta hitaji damu za viumbe wa duniani wala nyama zao tena…, kwa tone moja la damu yangu utapata misha marefu yasiyo hitaji kula wala kunywa,.jambo moja lazma mlifahamu ninyi ufalme Wajenzi huru, ninyi ni bora kuliko binadamu kwakuwa nimewafanya hivyo na kuwapa maisha yasiyo na ukomo.!”

Nilisema na watu wote wakapiga makelele ya furaha.

Nikaondoka katika lile eneo la wazi liliokuwa na mioto iliyo washwa kama mwenge nikiwa na mzee mwenye mvi nyingi kichwani.

Tulienda na yule mzee katika eneo jingine ambalo nilikuwa nalifahamu kabisa, ilikuwa ni katika eneo ambalo kuna wafungwa wa kibinadamu wengi ambao waliandaliwa kwa ajili ya kitoweo.

Palikuwa na watoto wengi walio valia mavazi ya kufanana, walikuwa ni wanafunzi..nilimgeukia mzee Zakora nikamtizama katika macho yake huku nikipitisha swali kwa njia ya mawazo pasina kuzungumza mmewatafuna wangapi hawa binadamu”

  Tisa mkuu.

   Sawa kuanzia leo ukomo wa kula watu umefika, kumbuka hawa ni nusu ndugu zangu vilevile.

   Sawa mkuu niliwatizama wale wanafunzi, walikuwa katika mashaka makubwa mno, hofu ya kuliwa nyama ilihali wakiwa hai..

     Mkuu kuna binadamu wanataka kukuona

Mzee Zakora aliniambia kwa mtindo ule ule wa mawazoni.

   Nani hao?

   Ni Ashimu Azizi na nduguze Moyo ulinipiga mkumbo nilipo sikia jina hilo.

Sikujua kwanini napatwa na joto la tumbo hata baada ya kutajiwa jina lile ambapo bila shaka mtu mwenye jina hilo alikuja kwa ajili ya kupata msaada kwangu,.

Nikaanza kuzipiga hatua kwenda kwa huyo binadamu mwenye kuitwa Hashimu Azizi ambaye kutajiwa tu jina lake nikapatwa na joto la tumbo huku moyo wangu ukipiga mkumbo.

******

“Mwaaaaaa” nilimwagiwa vitu vya baridi vilivyo leta unyevu nyevu katika mwili wangu,. nikafumbua macho yangu,

Nilikuwa nimelala katika sakafu huku kukiwa na watu wenye mavazi ya kipolisi wamenizunguka huku wakinitizama kwa jicho baya, mmoja akiwa ameshika ndoo ya maji niliyo mwagiwa mwilini mwangu na kunitoa katika usingizi wa kupoteza fahamu.

Nilitizama katika kile chumba nilicho kuwepo kumbukumbu zangu zikaanza kurejea taratibu,

Niliamka na kuketi kitako huku nikiwa na mawenge lukuki, nikajitizama mwili wangu nikajiona niko safi, sikuwa na maumivu eneo lolote..siyo katika korodani.

Katika mbavu wala kichwani nilikuwa safi kabisa kama kwamba ni mtu aliye kuwa amelala usiku kucha sasa ameamshwa asubuhi,.

“Nilikuwa wapi mimi?” niliuliza huku nikiwatizima wale polisi na wale washitakiwa wengine waliokuwa mule selo katika namna ya kupata jibu.

“Madawa ya kulevya siyo mazuri hata kidogo”

Alisema askari aliyekuwa amekamata ndoo ya maji.. “mtu anapata wazimu kirahisi kabisa”.

Alisema yule askari kauli iliyo nipa maana kwamba mimi nilikaribia kupata uchizi kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya,

“No no no afande…kuna mahala nilikuwa..ni kule pa siku ile jama..kule ambapo wenzangu waliliwa nyama.. yeah ndio kule afande hata huyo sijui vile mlikuwa mnataka niwatajie nimemjua afande niamini jamani aagh”

Nilisema haraka haraka huku macho yangu yakiwa yanapuyanga hovyo mule ndani, hakuna aliyenijibu zaidi ya kuchekwa huku wengine wakilaani matumizi ya madawa ya kulevya kwa vijana wa Tanzania.

Polisi waliondoka mule lockup na kukomea geti kubwa kwa kufuri imara kabisa.

Nilisimama wima nikajikagua mwili wangu wote sikuwa na hata chembe ya jeraha.

“Eti jamani mimi sikuwa mahali fulani hivi?”

Niliwauliza wale jamaa nilikuwa nao mule selo, hakuna aliye nijibu kila mtu alinichukulia kama chizi niliye athirika kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya.

Nilibaki najitafakari  kwa muda nikajikuta najiogopa mwenyewe. Mimi ni nani au inawezekan kweli nikawa na uwendawazimu katika akili yangu!.

“No mimi siyo mwehu, ninajitambua, ninacho kiona ndicho ninacho kizungumza,

Niliongea peke yangu maneno yaliyo sikika kwa wale jamaa nilio kuwa nao,  hapo nikaona jamaa wanapoteza kabisa Imani na mimi na kuniona ni binadamu niliye lukwa na akili kwa kiwango cha juu kabisa.

Nilifikilia mambo mengi kuhusu maisha yangu ya nyuma na familia yangu pamoja na ukoo wangu kwa ujumla.

Niliwahi kusikia kuwa kuna koo baadhi zinakuwa na mila na destuli zao katika mambo ya Matambiko na mizimu ya mababu wa kale, labda mimi nilikuwa miongoni mwa kijana mteule katika kusimamia mizimu ya koo yangu.

Hili kidogo liliingia katika akili yangu na kuleta kidogo maana ya matukioa yanayo nikabili.

Lakini mbona familia yangu ilikuwa ni familia ya kichamungu baba yangu kabla ya kufariki nikiwa na umri wa miaka kumi alikuwa ni shekhe mkuu wa musikiti wa Ibadhi kwa miaka mingi., pia mama yangu alikuwa ni ustadhati mzuri sana vilevile hata mimi nilikuwa mswalihina mzuri tu,.

Sasa vipi hii!.

Mara zote moyo wangu umejengwa katika Imani ya kuamini Mungu mmoja, ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa wala hana yeyote wa kufanana nae, ndiye mmilikiwa mbingu na ardhi na vitu vyote katika ulimwengu. Sasa vipi mimi nigeuke niwe Mungu wa jamii fulani.

Wajenzi Huru ndio ufalme wa wapi huo kama siyo mashetani tu haya”

Nilisema kwa sauti tena, wale jamaa mule selo wakazidi kunisikitikia namna ninvyo zidi kupagawa kiakili.

Niliamini kabisa hakuna mtu ambaye nitamweleza haya matukio yanayo tokea katika maisha yangu akanielewa.wajibu wa kutafuta majibu ya kitendawili hiki ninao mwenyewe.

Nahitaji kufanya kitu ili nipate majibu ya kitendawili hiki,

Ni kitu gani?.

Nahitaji kulala.

Niliketi chini katika sakafu nikatuliza akili huku nikijilazimisha kulala ili niingie katika ulimwengu mwingine pengine naweza nikapata majibu ya misamiati iliyopo katika maisha yangu nikiwa katika ulimwengu mwingine nipatapo usingizi.

Zaidi ya saa nzima usingizi uligoma sikuwa na lepe la usingizi macho yalikuwa makavu kabisa, taswira ya sura ya Nasra ilinitesa pia katika akili yangu, kila wakati binti huyo mwenye kufanana na mwanamke aliye shinda mashinadano ya urembo ilinijia.

Ilikuwa yapata kati ya saa saba ama saa nane za usiku bado sikupata usingizi kabisa sikuwa hata na dalili ya kusinzia.

Hadi inafika alfajili macho yalikuwa nimeyakodoa kodo sikufanikiwa kulala hata kidogo,

Tuliamshwa asubuhi na polisi walio ingia zamu ya asabuhi na kutakiwa kufanya usafi mule selo ikiwa ni pamoja na kumwaga kinyesi cha haja kubwa na ndogo kilichokuwa katika ndoo ambalo ndilo lililo tumika kwa kujisaidia, kisha tuka somwa majina ya watu wanne na kutakiwa kujianda kwa ajili ya kupelekwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa kesi zetu mbalimbali ambazo zilikuwa zinatukabili.

Saa moja kamili tulitolewa nje na kuingizwa katika gari la polisi tayari kwa kupelekwa mahakamani kisha gerezani kwa wale ambao hatuta pata dhamana.

Ni mimi peke yangu niliye pelekwa katika Mahakama ya wilaya huku wale jamaa wengine ambao sikujua walikuwa wanakabiliwa na makosa gani wakipelekwa katika mahakama ya mwanzo.

Mule mahakamani niliungana na mahabusu wengine walioletwa kutokea katika Gereza la Bangwe, ambao kesi zao zilikuwa bado hazija hukumiwa, tulikaa katika mabenchi tukimngoja hakimu mfawidhi wa Mahakama ya wilaya aliwasiri.

Nje na ndani ya Mahakama kulikuwa na ulinzi mkali wa askari wenye bunduki na mbwa.

Punde nilisikia sauti kali ikisema koooort na watu wote wakasimama kwa utii mbele yangu akaingia hakimu akiwa na watu wengine kama watatu.

Macho yangu yalipotua kwa yule mtu ambaye bila shaka ndiye alikuwa hakimu nilihisi mwili mzima ukinisisimka, jasho jembamba likanitoka nilimtizama tena kwa makini zaidi, macho yangu hayakuwa yananiongopea hata kidogo alikuwa ndiye haswaa,niliona dunia inageuka nje ndani na kujifinyanga huku mimi nikiwa ndani yake.

Alikuwa ni mzee ZAKORA.

Nilibaki nikiwa nimeduwaa bado nimesimama angali wenzangu wote walikwisha kaa chini.

“Wee kaa chini” nilistushwa na sauti ya amri ya askari magereza aliyekuwa karibu yangu, niliketi huku jicho la mshangao likiwa limenitoka pima.

  Mzee Zakora wazo lilipita katika akili yangu, mara hata baada ya wazo lile kupita kwa namna ya kutaja jina lake nilimwona yule mzee ama hakimu namna alivyo pata mstuko,alinyanyua kichwa chake uso wake uliokuwa umevishwa miwani ndogo ya macho haikuweza kuzuia nisiyone macho yake namna yalivyo patwa na mstuko ulio changanyikana na hofu kidogo, alikuwa akiangaza huku na kule akimtafuta mtu wa jamii yake ya kichawi aliye msemesha kwa namna ya ajabu kabisa.

Wee nani na uko wapi? alinijibu kwa namna ile ile ya mawazo na sauti yake ikapenya ndani kabisa ya masikio yangu,.yanii ilikuwa ni kama kwamba nimevaa visikilizio vya masikioni {earphone}  na kusikiliza mazungumzo ama kitu chochote katika santuli yoyote aidha simu ama Walkman ya CD.

Sikumjibu zaidi ya kutuliza mawazo yangu na kutowaza jambo lolote nilijitahidi kutoingiza kitu chochote katika akili yangu kwani kuendelea kuwaza ni kumpa mwanya yule mzee mwenye kuitwa Zakora nafasi ya kunigundua upesi, kitu ambacho sikuwa tayari kwa wakati huo,

Nilihamisha fikra zangu kwa marehemu Nasra.

Nilimwona yule hakimu kule mbele namna alivyokosa uimara kabisa, lakini hakuna aliyemgundua Zaidi yangu peke yangu.

Kesi zilikuwa nyingi siku ile, kesi yangu ilikuwa ya mwisho kuitwa na mwendesha mashtaka, nilisomewa mashtaka mawili moja la kuhusishwa na uuzaji wa madawa ya kulevya pili kusababisha vifo vya watu wawili, mbele ya yule hakimu mzee aliyekuwa anaandika andika katika mafaili vitu Fulani.. nilikana mashtaka yote mawili.

Sikutakiwa kujibu kitu kingine nikapangiwa tarehe nyingine ya kesi huku nikitakiwa kukaa mahabusu pasina kupata dhamana kutokana na aina ya kesi nilizo kuwa nazo.

Wakati naondoka nilitupa jicho katika kibao kidogo kilicho kuwa mbeleya meza kubwa ya hakimu kilisomeka kwa maandishi makubwa HAKIMU; CYMON MLWILO.

Niliondoka na kurudi mahala nilipokuwa nimekaa tukingojea kufungwa kwa mahakama kisha mahabusu wote tupelekwe gerezani.

   Hakimu; Cymon Mlwilo!. Nilijikuta nalitaja hilo jina katika hali ya kuwaza, na hapo yule mzee kule katika kiti, alistuka mno hadi nikaona maofisa waliokuwa wamekaa viti vya pembeni yake wakimsaili kutaka kujua amepatwa na nini.

Wewe ni nani? na kwanini unanichezea? unaita majina yangu bila kujibainisha mbele yangu, nani wewe.  Mzee aliunguruma kwa ghadhabu mno.

Sikumjibu, nilijikausha nikisubiri muda wa kupelekwa katika gereza.

Sikuwa na ndugu hata mmoja katika mji wa Kigoma kwa wakati huo kwani tangu nipotee na kuibuka siku tatu kabla ya kutokea kwa maswahibu haya sikuwa na taarifa na ndugu wala jamaa yoyote, hali hii pia ilimaanisha kwamba, matatizo yangu haya ni ya kwangu peke yangu!.

Mahakama ilifungwa saa kumi kasorobo watu tulingizwa katika basi la magereza na safari ya kupelekwa katika gereza la bagwe ikaanza.

Dakika ishirini na tano pekee zilitosha kutufikisha mbele ya geti la gereza kubwa la bangwe, tuliteremka katika gari na kuingizwa ndani ya gereza chini ya ulinzi mkali wa askari wenye bunduki na mbwa, huko tuliingizwa katika chumba kidogo kwa zamu ambacho kilitumika kuhifadhia vitu vya watu, palikuwa na askari magereza ambaye alifanya kazi ya kuandika kila kitu acha mahabusu ikiwa ni pamoja na hati ya shitaka lake.

Baada ya kukabidhi kila kitu katika ile ofisi ya magereza, tulitakiwa kula chakula kwani muda wa kufungiwa ulikuwa umewadia kwa mujibu wa jua ilikuwa ni kati ya saa tisa ama saa kumi kasoro.

Kwa mara ya kwanza nilihisi njaa kwani niligundua nilikuwa nimekaa kwa masiku mawili pasina kuweka kitu chochote mdomoni.

Tulipewa mabakuli makubwa ya shaba na kugawiwa ugali kwa harage bovu lililo tabasamu kama karanga.

Kwakuwa nilikuwa na njaa ilikuwa ni chakula kitamu kabisa kilicho jaza tumbo langu nikashushua na maji ya kunywa nikashiba kabisa.

Sasa kengele iligonga watu wote tukapanga foleni huku tukiwa tumechuchuma, katika miili yatu tukiwa vidali wazi ama tumbo wazi kama mwingine anavyo weza kusema na kuanza kuingia katika mabweni mmoja mmoja kwa namba.

Mule ndani hali ilikuwa tete sana kwani matandiko ya kulalia yalikuwa yamechakaa mno,vilevile kigodolo cha futi tatu kwa sita mlitakiwa kulala watu wanne, mtindo ulio tumika kulala ni kiubavu ubavu ili mjitosheleze hakuna kujigeuza upande wa pili, ukilala upande mmoja basi utalala hivyo hivyo hadi  kunakucha asubuhi yanii ni kama kwamba umezikwa katika mwana ndani kaburini.. kwa hakika hakuna mahala penye maisha magumu katika hii dunia kama jela za Tanzania huo ndio ukweli ninao uzungumza katika maandishi haya.

Kule hakuna haki za binadamu hata kidogo.

Kwakuwa siku hiyo nilikuwa nimechoka mno kutokna na usiku wa kuamkia siku hii sikuwa niliye lala usiku ,haikuchukua zaidi ya dakika kumi, tayari usingizi ulinipitia na kuingia katika ndoto yenye ukweli yakinifu ndani yake iliyo nitoa mule na jela kunipeleka katika mazingira mengine kabisa.

 

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Ijumaa hapahapa.

 

 

Comments are closed.