JINI MTU-11

Yapata saa saba za usiku nilikuwa mbele ya kitanda alicho lalila Nasra nikiwa kiumbe mwingine mwenye uwezo wa ajabu. Ni katika chumba kidogo ndani ya hospitali ya Lubengera  Mwanga.

Nitizama yale mazingira ndani ya ile wodi alikuwa yeye peke yake,kulikuwa na korido ndogo iliyotenganisha wodi ile na ofisi ya manesi.

Wagonjwa na wauguzi wote walikuwa wamelala. Nasra  nilimwita taratibu katika namna       ile ile ya  mawazoni.

   Nasra niliita tena, na mara hiyo hiyo alikurupuka kitandani macho ameyatoa mbele yangu kisha kilicho fuata hapo ilikuwa ni kizaa zaa,  “maamaaaaaa nakufaaaa!.” ukulele mkubwa wa hofu ulitoka kinywani mwa Nasra, alirusha mikono yake huku na kule, ilikuwa ni kama kwamba ameona jini.

Mara hiyo hiyo nikasikia vishindo vya nesi akija mule wodini, nilibaki nimepigwa na bumbuwazi akili yangu ikiwa imesimama kwa muda bila kufanya kazi yake sawasawa kwani ilikuwa ni taharuki ambayo sikuitegemea,kweli Nasra alikuwa ananiogopa lakini sikujua kama ni kwa kiwango kile.

Aliendelea kupiga mikelele, na mara nesi aliyekuwa amevaa mavazi meupe na kikofia kichwani aliigia kasi mule wodini.

Alifunga breki ghafla na kubaki akiwa anatutizama kwa zamu huku akiwa na viulizo vingi kichwani mwake.

Hali ile ya kuonekana kwa yule nesi haikuwa nzuri kwangu,ilikuwa ni lazma nifanye kitu ili nisiingie katika matatizo na kuleta kizaa zaa kingine katika jamii,vipi niwe gerezani wakati huo huo nionekane niko mtaani.

“Hei hei, wewe ni nani hapa muda huu?”  nesi aliuniuliza kwa wahka,huku ukulele wa Nasra ukipungua, na hapo aliruka pale kitandani na kutoka kasi hadi mahala alipo kuwa amesimama yule nesi na kuwa nyuma ya mgongo wa nesi.

Sasa ikawa wananitizama kwa namna ya hofu, nesi akinitizama kama muhalifu fulani niliye ibuka mule wodini kwa kumdhulu mgonjwa, Nasra yeye akinitizama kama jini ama mzimu niliye katika mwenekano wa Vegasi.

Akili yangu ilizunguka na mara hiyo hiyo tena aliingia daktari wa kiume na nesi mwingine ndani ya ile wodi wote wakawa usawa wa yule nesi wa awali pamoja na Nasra.

“Nini hapa, kuna nini?” aliuliza daktari.

“Huyu mtu kaingia wodini sasa hivi kuna jambo baya alitaka kulifanya kwa mgonjwa”. Alisema yule  nesi.

“Hey wewe ni nani ?” aliniuliza yule daktari. Lakini sikujibu, wala sikuona sababu ya kujibizana na wale watu muda ule kwani ni kuzidi kupoteza muda kwa kujibizana nao,maana yake ni kujiweka katika mazingira magumu na hatimae kuingia kizuizini.

Nilitizama pembeni mwa ile wodi kulikuwa na chumba kilicho tumika kama choo na bafu,  wazo la kukimbilia huko likanijia, kwani hiyo ndio nafsi niliyo bakiza.

Lakini kabla sijatekeleza wazo langu, Nasra aliachia ukulele. “Anataka kukimbilia bafuni huyoo”  alisoma mawazo.

Ooh hii ilikuwa mbaya kwangu, nilitoka kasi huku nikipamia baadhi ya vitu vilivyo kuwa mule wodini, kulisikika ukulele wa taharuki kwa wale manesi  na daktari wao akiwapo Nasra, niliufikia mlango wa bafu na kuubamiza  kwa msukumo wa nguvu kuingia ndani kisha baada ya kuingia nikaukomea kwa ndani.

Nilikuwa nikihema kwa kasi, bado ukulele kwa wale watu kule wodini ulizidi kuwa juu.

Nikasikia walinzi wa hosptali wakingia mule wodini ili kuweza kunidhibiti nisitoroke.

“Aiseee kuna muhalifu kajifungia chooni askari, fanyeni kila hali akamatwe asitoroke huyo mtu anaonekana kabisa siyo mwema” alisema daktari.

Walinzi walijaa mule wodini na kunitaka nijisalimishe kwani mikononi mwao walikuwa na bunduki na wangeweza kuvunja mlango na kunikamata kama nikileta ubishi.

Nilikuwa nikihema huku nikifikilia haraka haraka kitu gani cha kufanya, wakati huo huo nikasikia yule daktari akiwasiliana na afande mwita juu ya hali iliyopo pale wodini.

Nilitoa kidonge kidogo chenye ukubwa wa piritoni, kisha nikakitia mdomoni, kile kidonge hakikuwa ni chenye kuyeyuka  ilikuwa ni kidonge cha plastiki.

Kule nje wale walinzi walianza kunihesabia moja mpaka tano niwe nimejisalimisha vinginevyo wanabomoa mlango na kunikabili,

“moja…mbili…tatu…nne…”  walinihesabia, nilikuwa kimya,pembezoni mwa kona ya maliwato.

Kishindo kikubwa kilisikika na mlango wa choo ulipigwa kishindo kikubwa na kisha walinzi wenye bunduki wakajitoma ndani,

Ajabu hawakuniona.

Walingaza eneo lile dogo la maliwato hata katika dali , lakini wapi macho yao hayakuwa na uwezo wa kuniona katika ile kona niliyo kuwa nimesimama, japo mimi niliweza kuwaona vizuri sana.

Usiku ule kila mtu alibaki akiwa amebung’aa kwa tukio lile, vipi mtu akimbile maliwato,eneo ambalo kuna mlango mmoja wa kutokea kisha ayeyuke katika mazingira ya kutatanisha!.

Huu ni uchawi.

Hili ndilo lililokuwa akilini mwa watu usiku ule wa manane pale hospitali.

Kwa tukio lile, kwa kiasi fulani wauguzi na madaktari walianza kuamini madai ya  Nasra.

Nilitoka katika maliwato taratibu nikipishana na ulinzi mkali uliokuwa wasaa ule mazingira yale na kutokomea nje pasina kuonekan katika macho ya binadamu wa kawaida.

Nilingia mtaani na kuanza kuranda randa hovyo nikiwa sina mwelekeo mzuri,

Kile kidonge kidogo kama piritoni kiliendela kuwa mdomoni kwangu na kunifanya niendelee kutoonekana katika macho ya watu katika mitaa usiku ule.

Bila kuifanyia kitu akili ya Nasra kamwe

hawezi kunisiadiki kama mimi ndiye Vegasi, siku zote ataniona mimi kama jini mtu, lakini nimfanye nini huyu mwanamke ninae mpenda ili aweze kunielewa kwamba mimi ndiye?, nibadilishe akili yake na kuifanya ifanye kazi vile ninavyo taka mimi? Yanii nimfanye awe ndondocha katika hizi siku chache za uhai wake?

Ama nimchukue nimpeleke maili nyingi mbali  watu ili walau huko nimweke chini na kumweleza kinaganaga?  Hii kidogo ilikuwa nzuri japo sikutaka kumfanya mwanamke huyu ajione mateka kwangu. Sasa kumbe nifanye nini?

Sikupata jibu.

Kwa mujibu wa taratibu za miungu ya bahali Nasra alikuwa na siku mbili tu za kuishi kutoka siku hiyo.

Ndani ya usiku huo huo nikiwa katika mitaa nikirandaranda bila mwelekeo, kidonge kidogo kikiwa mdomoni mwangu.

Sasa nilihitaji kuonana na mzee Zakora ama hakimu Cyomon Mlwilo kama alivyo fahamika kwa binadamu.

Nilifumba macho kisha nikanuiza maneno ya kuwa mahali aliko mzee Zakora.

Hata nilivyo fumbua amcho tu nilikuwa mbele ya kitanda kizuri cha sita kwa sita ndani ya chumba nadhifu nyenye kila aina ya thamani  ju ya kitanda kile akiwa amelala mzee Zakora na mwanamke mwembamba mrembo haswaa.

Japo nilikuwa na uwezo wa kutumia nguvu za ajabu lakini hadi wakati huo bado nilikuwa na vitendawili vingi ndani ya akili yangu kuhusu mguvu hizo zilivyo kuja kimaajabu katika maisha yangu.

Vipi nijue kutumia uchawi kiasi hiki ilihali sina mwalimu wa kunifundisha uchawi huu!.

Maswali muhimu ambayo nilihitaji ufumbuzi wa majibu yake  “mimi ni nani katika ufalme ule wa ulimwengu wa ajabu ambao huwa nasujidiwa kama Mungu? na kwanini niwe mimi? Na huo ufalme uko wapi? Maswali yote haya niliamini mzee Zakora atakuwa na majibu yake.

Kabla sijamwamsha yule mzee niliisaili ile nyumba yote, alikuwa ni miongi mwa watu walioshi maisha ambayo binadamu anatakiwa aishi.

Nje ya nyumba katika wigo mpana kulikuwa na magari matatu ya kisasa, bustani nzuri ya nyasi za kijani kibichi na mauwa mazuri yaliyo tunzwa vizuri.

Upande wa mashaliki mwa gati kuu la kuingia katika nyumba ile kulikuwa na kibwawa kidogo cha kuogelea ukingoni kukiwa na viti vizuri vya kupumzikia ambavyo ungeweza kuvikuta katika beach na hotel kubwa kubwa, yalikuwa ni mazingira ambayo ni jamii ya watu wachache mno katika nchi za dunia ya tatu walio bahatika kuishi katika mazingira yale.

Katika geti kulikuwa na mlinzi kutoka katika kampuni ya ulinzi aliyekuwa akilinda na bunduki pamoja na mbwa,

Yule mbwa alikuwa akinibwekea huku akijivuta katika minyororo aliyo fungwa shingoni akitaka kunifuata huku yule mlinzi akiwa makini kufutilia kile kinacho mfanya yule mbwa abweke kiasi kile.

Haikuwa nzuri ile, nilinuia kurudi chumbani mwa mzee Zakora na sekunde hiyo hiyo nilikuwa mbele ya kitanda cha mzee Zakora aliyekuwa amelala na mwanamke wake wake.

  Mzee Zakora nilimwita, huku nikimgusa katika shavu lake

Alifumbua macho yake kama mzimu akiwa amekodoa bila kupepesa kope.

Aliingiza mkono mfukoni katika pajama la kulalia na kutoa kidonge kama kile nilicho kuwa nakimung’unya  mdomoni mwangu, kisha alitoka kitandani huku katika mwili wake kukiwa kama na viwiliwili pacha.

Alitoka kitandani na kupiga magoti mbele yangu huku kiwiliwili kingine kikibaki kikiwa kimelala bila fahamu.

Alikuwa mepiga magoti kwa utii mkubwa.

“Niko tayari kufuata lolote utakalo nielekeza bwana wangu” alisema kwa unyenyekevu na utii wa hali ya juu, kama ungepata bahati ya kumwona mtu yule,  katu usinge amini kama yule ndiye alikuwa  hakimu wa wilaya, mtu mwenye kuheshimika kabisa kutokana na wadhifa wake.

“Nataka majibu ya maswali nitakayo kuuliza upesi” nilisema kwa sauti ya kiburi na majivuno.

“Sawa bwana wangu”

“Mimi ni nani?” nilimuuliza  kwa ufupi.

“Nabii wangu wa mwisho katika imani yangu takatifu”

“Imani ipi? Na kwanini mimi niwe nabii wako”

Niliuliza ndita zikiwa zimejipinda katika paji langu la uso., mzee Zakora alinitizama kwa mashaka kidogo, huku akiwa na viulizo vingi kichwani mwake,

“Jibu upesi wewe mtu” nilistua na kumkazia macho.

“Kwakweli sijui, ninacho jua mimi ni hilo tu”

Alijibu, jibu lake lilinichanganya na kunizidishia maswali mengi.

“Wewe aliye kueleza kwamba mimi ni nabii wako wa mwisho ni nani?”

“Ni lody Kizy”

“Lody kizy?”

“Ndio mkuu”

“ Ndio nani?”

“Nabii kutoka ukoo wa majini.”

“Whaaat!.” nilishanga, zilikuwa ni habari za ajabu kabisa.

Nikiwa bado katika tafakuli mara ghafla kulisikia vishindo vikali katika geti huko nje, huku milio ya risasi ikilindima eneo lote ikifuatiwa na sauti kali ya maumivu kutoka kwa mlinzi na mbwa wake.

Ndani ya dakika za kuhesabu ilizuka kizaaa zaa kingine katika ile nyumba.

Ajabu pamoja na sinto fahamu iliyo ibuka mule ndani yule mzee alibaki akiwa ameniinamia vile vile katika namna ya kunisujuda.

Mwanamke aliye kuwa amelala na mzee Zakora alistuka katika usingizi kutokana na kizaa zaa kilicho zuka katika nyumba ile ikawa anamwamsha mzee Zakora, yanii kile kiwili wili kilicho bakia kitandani.

Lakini wapi, ule mwili usiyo na nafsi uliendela kulala vile vile kama maiti, binti aliingia katika mashaka makubwa, wakati huo huo sauti za mabinti kutokea katika vyumba vingine ndani ya nyumba ile zilisikika zikijitetea na kugumia maumivu makali ya kipigo kutoka kwa watu walio vamia mule ndani.

Yule mwanamke aliteremka katika kitanda akiwa na  hofu kubwa, ikawa anatafuta mahala pa kujificha, uvunguni mwa kitanda ikawa ndio sehemu aliyo ona inafaa kujitenga na kizaazaa kile.

Ndani ya sekunde kumi watu sita, wenye sura za kikatili na miili mikubwa yenye misuli imara, wakiwa na bunduki mikononi mwao walijitoma mule ndani wakiwa na mabinti wawili vigori, ambapo kwa mtazamo wa mara moja nilifahamu walikuwa ni watoto wa mzee Zakora.

Mtu mmoja ambaye alionekana ndiye kiongozi wa lile kundi la majambazi aliusogelea mwili wa mzee Zakora na kumshindilia ngumi kali ya korodani, ambayo aliamini lile pigo lazma litamwamsha yule mtu aliye onekana kulowea katika usingizi wa pono.

Lakini wapi.

Mzee Zakora hakuamka wala kuonekana kuingiwa na lile pigo, japo alikuwa akihema, hata wakati hayo yakitokea katu hakuna macho hata ya mtu mmoja aliye weza kutuona.

Ilikuwa ajabu kidogo kwa wale wavamizi lakini.jamaa alimshindilia teke kali tumboni..lakini kiwili wili cha mzee Zakora hakikutikisika kabisa.

“Kisha jifia kwa presha hili zee” kiongozi wa wale wavamizi alisema.

“Wapi pesa ninyi” aliongea tena mvamizi mkuu kwa sauti ya amri yenye dutu za vitisho.

Wakati huo huo jambazi jingine liliweza kugundua mahala alikojificha hawara wa mzee Zakora kule katika uvungu.

Alichomolewa

“Paaa” alipigwa kibao yule mwana mwali  wa mzee Zakoro, maumivu ya kibao kile ikawa yanafukuta  mwilini mwake, na hakuwa na ujasili wa kutosema wapi pesa zilipo mule ndani.

Ajabu ni kuwa  wakati yote hayo yatendeka mule ndani,  kwa upande wangu mimi ilikuwa ni aina ya utalii mzuri ndani ya nafsi yangu, kwa lugha nyepesi naweza nikasema, nilifurahia kila tukio lililokuwa likiendelea mule ndani.

Sikujisikuia huruma hata kidogo.

Wale wavamizi walivunja droo ndogo ya kabati na kutoa maburungutu mengi ya noti za shilingi elfu kumi kumi, kisha zote wakazisokomeza katika begi dogo la kuvaa mgongoni.

Nyuso zao zikawa  zenye kutoa tabasamu baya kabisa lisilo na mvuto hata kidogo katika macho ya mtu mwenye kupenda amani.

Haikutosha, waliwalazaimisha wale wanawake kuvua nguo zao zote!. Sasa walikwiba pesa na uroda pia walitaka.

Mzee Zakora alikuwa akilia miguuni mwangu huku akiniomba niisadie familia yake, lakini wapi macho na moyo wangu ulivutiwa na matukio yale yaliyo kuwa yanaendelea mule ndani.

Kiongozi wa wale watu alisogea katika kiwili wili cha mzee Zakora na kumimina risasi nyingi mno mwilini mwake, wale wanawake walitoa ukulele wa hofu huku macho yakiwa yamewachonyota vibaya mno.

Kwa hakika mabinti walikuwa katika wakati mgumu mno, fursa hiyo ikatumiwa na wale jamaa kuwataka wavue nguo zao zote na kubaki uchi kabisa, wakiwa na mashaka makubwa ya kupigwa risasi  ya kichwa na kufa, wote watatu walitii amri ya wavamizi, walivua nguo zao na kubaki kama walivyo kuja duniani.

Kubakwa kukawa nje nje, maumbile ya wale wanawake kamwe wale watu wasiweza kuwaacha hivi hivi tu bila kuwaonja vinginevyo wangekuwa na matatizo katika miili yao.

Naam, ndivyo ilivyo kuwa.

Sasa wavamizi sita wakawa wanawabaka wale mabinti watatu kwa nguvu na kwa zamu.

Mzee Zakaro aliendelea kulia miguuni mwangu akiniomba kwa maneno ya huruma kabisa kama  nisaidie ile kadhia kitendo cha wanawe kubakwa mbele yake lilikuwa ni tukio lililochoma mno moyo wake.

Lakini ilikuwa ni kama anapiga ngoma katika masikio ya mbuzi, mimi nilikuwa nikifaidi lile filamu kali kabisa tena adimu!.

Wavamizi waliwazini wale wanawake hadi miili yao ilipo sema basi, kisha katika hali ambayo hata mimi mwenyewe sikuitegemea wale jamaa waliwapiga risasi wanawake wote na kufa pale pale.

Mzee zakora alilia mno.

Roho ya binadamu ikisha kuwa mbaya, anageuka na kuwa kiumbe wa ajabu mno ambapo anaweza kutenda  dhambi hata ibirisi mwenyewe akabaki anashangaa!.

Maiti zilitapakaa mule ndani huku wimbi la damu likiwa jingi kabisa yote hayo yalichukua si zaidi ya dakika ishirini, jamaa waliondoka eneo lile,huku mule ndani nikiwa mimi na mzee Zakora ambao hatukuwa tunaonekan katika macho ya kawaida.

“Sasa mzee Zakora tunaendelea, naona tulipata bugudha kidogo” nilisema yanii kama kwamba lile tukio lililotokea pale lilikuwa kama la kuuwa kunguni kwa dawa.

Niliona namna mzee Zakora alivyo pata mafadhaiko kwa kauli yangu, kwani hadi wakati huo alikuwa katika matatizo makubwa mno ila ajabu  mimi niliayachukua kwa wepesi usiyo kawaida.

Walio kufa walikuwa watoto wake wa kuzaa pamoja na sasa vipi mimi nichukulie vifo vile kama maafa ya mbu ama kunguni.!

“Umenielewa wewe?” nilimstua nikimtoa katika mkanganyiko wa kuchanganyikiwa.

“Ndio bwana wangu” alinijbu kwa upole akifanya macho yake ya kizee kuwa ya huruma mbele yangu, lakini sikuwa na hisia hizo hata kidogo, ushetani ulikuwa umenienea mwilini mwangu.

“Umesema lody Kizy ni nabii kutoka ujinini?”

“Ndio bwana wangu”

“Kwa hiyo ni jini”

“Ndio bwana wangu”

“Nampataje huyo kiumbe?”

“Kwa kweli sijui bwana wangu lakini unaweza kutumia uwezo wako  ulio tunukiwa ukakutana naye”

Alisema yule mzee na mara nilisikia vingora vya magari ya polisi huko nje ya nyumba, sikuona la muhimu tena pale nilitembea kutokea katika kile chumba kilicho tapakaa damu na miili ya binadamu ambayo tayari ilikuwa maiti, niliruka ile miili na kutoka kwa kupitia katika sebule, nikipishana na polisi walio kuwa na bunduki wakingia katika nyumba ile kwa tahadhali kubwa.

Mzee Zakora alibaki mule ndani akilia kwa misiba ile huku akibaki katika hali ile ya kuto onekana tena kwani mwili wake tayari ulikuwa maiti nay eye alibaki nafsi tu.

Je, nini kitaendelea?
Tukutane kesho.

 

Toa comment