The House of Favourite Newspapers

JINI MTU-13

0

Mvua kubwa ya upepo na mawe ilinyesha zaidi ya masaa mawili..baada ya kutoka katika mapambano makali kule katika makabuli ya nazareti sasa nilikuwa  mbele ya nyumba ya afande Mwita, yapata saa nne kasoro za usiku, kiasi mvua ilikuwa imekatika, katika maeneo ya gungu, afande mwita alikuwa ikishi katika nyumba ya vyumba viwili na sebule.

Nyumba ilikuwa kimya, umeme wa tanesko ulikuwa umekwisha katika saa nyingi ikiwa ni kutokana na dhoruba ya mvua kubwa ya upepo iliyonyesha masaa mawili nyuma.

Nilipita hadi chumbani mwa afande Mwita, nyumba ilikuwa kimya giza lilikiwa zito mule ndani mwa Afande Mwita.

Mwita alikuwa amelala chali katika kitanda alicho kuwa amelala na mwanamke, ambaye alikuwa pia yuko macho akiwa anabofya bofya simu yake ya mkononi, huku kila mtu akionekena kuwa na hamsini zake usiku ile.

Niliketi katika sofa lililokuwa mule ndani, nikifikilia namna ya kuzungumza na yule afande juu ya kifo cha Nasra vile kilivyo tokea ghafla.

Na hata nikiwa katika fikra zile mwanamke aliyekuwa amelala ukutani mwa kitanda kile kikubwa alinyanyuka na kuelekea maliwatoni.

Nilisimama na kumfuata kule maliwato.

Mwanamke alipo maliza kujisaidia haja ndogo nilimgusa kichwani mwake, na lilikuwa ni tendao la haraka sana,kwani kitendo cha kumgusa tu aliregea na kuanguka chini,nilifumba macho nikanuia maneno fulani, na hapo kitu kama kivuli kutoka katika mwili wa yule mwanamke kilinizunguka na kuniingia mwilini mwangu, hata kilipo kuwa kikinivaa mwilini mwangu nilikuwa nikihisi kama namwagiwa maji ya uvuguvugu mwilini mwangu.

Nguo zangu ziliyeyuka kama unyoya unao ungua katika moto huku mavazi ya yule mwanamke yakijitengeneza katika mwili mwangu kwa namna ya ajabu kabisa, ambayo nashindwa kuelezea.

Kama ungebahatika kuniona ungeona nafanana kabisa na yule mwanamke aliye kuwa amelala pale chini akiwa hana fahamu, nilikuwa na kila kitu alicho kuwa nacho yule mwanamke isipo kuwa maungo ya uzazi tu, ndio yalibaki vile vile.

Nilitoka mule bafuni na kurudi chumbani alikokuwa Afande Mwita.

Nilipanda kitandani upande ule ule aliokuwa amelala yule mwanamke, nikijiweka sawa kwa ajili ya mahojiano na yule afande mwenye akili nyingi, lakini kabla sijasema lolote Mwita alijipindua upande wangu na kuanza kunishika shika.! na kunipiga mabusu mbalimbali mwilini mwangu.

Nilimsukuma na kusogea kando, “leo sijisikii kufanya chochote” nilisema. Huku nikijisikia vibaya sana kufanyiwa kitendo kile na mwanaume mwenzangu.

“Hee!. Makubwa siyo wewe uliye kuwa unanisumbu leo kutwa nzima jamani sasa vipi tena?”

“Nimeingia ghafla hedhini?”

“Mmh!. Wewe hedhi si ulimaliza juzi wewe? sasa hiyo hedhi ipi tena mke wangu mpenzi? eeh” alisema huku akipitisha ulimi wake katika shingo yangu yenye kuonekana katika macho yake kama ya mke wake.

“Aagh..bwana..wee nielewe tu” nilijibalaguza  nikiona uongo wangu, unaweza kumfanya yule polisi kuhisi kitu kisicho cha kawaida.

“Kama hutaki sawa, usiwe unanisumbua kwa meseji zako zisizo koma nikiwa kazini, hasa katika kipindi hiki ninacho kabiliwa na upelelezi wa kesi za ajabu ajabu,”

Alisema., na hapo hapo nikaona nimepata pa kuanzia.

“Kesi zipi za ajabu ajabu?” niliuliza nikijiweka sawa.

“Wee nae,. kila siku unaniliza swali moja.,si hii kesi ya mauwaji ya Nasra na mwanae”

“Ooh! hivi kitu gani kinaendelea?”

“Aagh nimechoka bhana,tutaongea kesho wee umaninyima uroda wako, basi lala, sitaki maswali” alisema katika namna ya utani huku akigeukia upande wa pili na kunipa mgongo,

“Nasikia Nasra amefariki” niliendelea kumuhoji bila kujali kama hizi taarifa alikuwa anajua mkewe kama anazifahamu ilihali anauliza tena.

Alinigeukia akiwa amebadilika sura, akinitizama katika namna ya mshangao, akiwa hategemei jambo fulani toka kwangu alilo lifahamu mwenyewe.

Nikahisi sasa nimegundulika kwa huyu afande.

Moyo wangu ukawa unapiga kwa kasi, nikaona nashindwa kupata kitu juu ya kile kilicho mfanya Nasra afe katika siku zisizo zake, huku nikishia kugundulika kwa yule polisi.

“Nasra yupi?” aliniuliza akiwa amenikazia macho ya mshangao hadi nikapata mashaka.

Si…huyu..huyu..mpya,. aliyefufuka!. nilijibu kwa kitetemeshi nikiwa tayari kwa makabiliano na yule polisi kama angeanzisha dhidi yangu.

Kauli hii pia ilizidi kumshangaza,akanyanyuka pale kitandani na kuketi kitako ikawa ananitizama katika nanma ya kuuliza maswali mengi ilihali akiwa hajui ayaulize vipi maswali yake.

“Wewe  haya mambo umejuaje kuwa kuna Nasra mpya ameibuka?” niligeuka kuwa mjibu maswali badala ya mimi kuwa muulizaji kama nilivyo kusudia.

“Kwani hayupo Nasra mpya aliyeibuka hvi karibuni?” na mimi nilimjibu kwa swali.

“Huyo mtu yupo ila nashanga wewe umejuaje, wakati hili, nilikuwa sijakueleza”

“Wewe hujanieleza, ila  mtaani haya mambo yanajulikna na ndiko niliko yasikia”

Nilimjbu katika namna ya kujishetua,vidole nikivichanua midomo nimeipinda  na macho nikiyazungusha vile wanawake wafanyavyo wakiwa wanapeana umbea ama udaku wa hapa na pale.

“Ooh!. Hili swala ni gumu mno, mara zote nilitaka liwe siri, linaweza kuleta taharuki kubwa mno katika jamii kama mambo haya yakianza kuvuja kwa mtindo huu, acutually ni kesi ambayo ndani yake kuna friction scence ya ajabu kabisa, ni kesi yenye mwendelezo wa matukio fulani ya siri mno, mambo ya secret society pia yanahusika ndani ya kesi hii”

“Kwani kilicho muua yule binti ni nini?”

“Hii ndio inanifanya kichwa kiume” alisema kwa fadhaa huku akilala chali macho ameyatupa juu ya dali, mikono ameivingilisha  chini ya kisigo chake juu ya mto alio weka kichwa chake, kisha akaendelea kusema.

“Kichwani mwa yule binti marehamu, kulikuwa kuna kitu kilikuwa kinatembea katika fikra zake, yanii kila wazo alilo weza kuwaza yule kiumbe aliweza kujua, lakini pia, kila wazo lililowazwa na kiumbe yule, pia binti aliweza kujua…awali haya maneno niliyachukulia kama hadithi..lakini  baada ya kufika hospitalini leo asabuhi na kupata uthibitisho wa kutoka kwa manesi na dokta Mathiasi juu ya kuonwa kwa yule kiumbe ndani ya wodi ya Nasra kabla ya kupotea kimiujiza katika maliwato, taarifa hizi ndio zilinifanya nilifuatilie swala hili kiundani zaidi bila kujua maisha ya yule binti naenda kuyatia doa.”

“Kivipi hapo” nilihoji huku nikimtizama Afande Mwita aliye kuwa amelala katika mtindo uleule.

Kiumbe anaye shutumiwa kuibuka kule hospitalini ni mahabusu aliyefungwa katika gereza la Bangwe hadi dakika hii, na siyo hilo tu huyo mtu ndiye muhusika anaye shutumiwa kwa kusababisha kifo cha binti huyu ambaye leo anaonekana yuko hai,.umeona hapo.”

“Ebwana wee! Eeh ikawaje?” nilijitia kustajabishwa na taarifa ile, katu Afande Mwita hakujua tena kama huyo kiumbe anae mwongelea ndiye mimi niliye pembeni ya kitanda chake nikiwa na wajihi wa mkewe.

“Hapo ilibidi akili itumike ili niweze kumtia hatiani yule muhalifu mwenye uwezo wa kutisha..yule binti  Nasra, kitaaluma ni mwalimu wa watu wasiyoweza kuongea mabubu {deaf professiyonal} kilicho fanyika binti alichukuliwa na kuingizwa katika chumba cha mawasiliano, ambapo tulitegesha vifaa vya mawasiliano, kisha binti alitakiwa kutoa taarifa zote za yule kiumbe kwa njia ya ishara, chochote anacho kiwaza, kwa kuzingatia kuwa yule kiumbe anaweza kusikia neno lolote atakalo lizungmza Nasra..hata kama akiwa maili elfu moja..Kwakuwa chochote ambacho anakiongea na kukiwaza yule kiumbe anasikia..basi ishara itumike kutoa taarifa zote pindi sisi tunapokuwa tunafanya mahojiano na huyo mahabusu anae sadikiwa kuwa ndiyo huyo kiumbe mwenyewe.

“Duh! Kweli hii njia kiboko nini kilitokea?” niliuliza kwa makini zaidi.

“Zoezi lilienda vizuri sana, lakini…”

“Lakini nini?” nilidakia,wahka ukiwa umenivaa usoni na moyoni,

“Pindi wakati hayo yakiendelea, binti aliomba chakula kwani njaa alikuwa ikimsumbua, ubwabwa na samaki ukaletwa, na..”

“Ooooh mungu wangu hapo ndipo mlipo mmaliza Nasra wanguuu!!…” nilijikuta nikilopoka, akili yangu ikiwa imekosa uimara kabisa.

Nilihisi mawenge mawenge katika akili yangu kwa zaidi ya nusu dakika nilibaki nimeduwaa    moyo wangu ukisombwa na simanzi iliyochanganyikana na aina fulani ya majuto,

Hata dakika moja ilipo kamilika ndipo nilipo jikuta nikitizamana macho kwa macho na mdomo wa bastola, uso wa afande mwita ukiwa katika taharuki isiyo mithilika, akiwa wima mwili unamtetemeka hovyo.

“U-Vegasi wewe?” aliniuliza akirudi hatua kadhaa nyuma na kukomea mlango kwa ndani,

Nilibaki nimeketi pale kitandani namtizama yule askari anaye taka tuonyeshane makeke mule ndani.

“Umepatwa na nini sweaty?”

“Kimya wewe, hakuna sweaty hapa..Vegasi najua wewe ni mwanga tu ambaye usha niibukia humu ndani kwa sura ya mke wangu,..na kunichimba,.. sasa nakwambia hivi..,leo nitacheza na wewe hadi mshindi apatikane,”  alisema afande Mwita, na hapo hapo risasi ilitoka katika bastola yake na kutoa mlipuko mkubwa mule ndani,.sekunde hiyo hiyo nikahisi chuma kigumu kikipenya katika bega langu la kulia  na kutokea upande wa pili huku maumivu makali yakisambaa katika mwili wangu kasi ya ajabu.

Jamaa ahakuwa na utani hata kidogo macho yake yalionyesha kuwa na uhakika kwa kile anacho kifanya na alidhamilia kufanya tukio jingine zaidi ya hili la kunipiga riasi ya begani.

Nilihema kwa tabu damu nyingi ikichafua mashuka ya kitanda kile.

“Unakosea sana wewe mtu, elewa wazi una uhalibu mwili wa mwanamke wako, na ukiendelea na ujuha huu, utamwua hawala yako kwa mkono wako mwenyewe”

“Unafikiri mimi ni mbumbumbu kiasi hicho Vegasi? Tulia hivyo hivyo vinginevyo risasi itakayo fuata nitaielekeza katika bichwa lako na kumwaga ubongo wako”

Alinong’ona kwa ukali mwili ukiwa bado una mtetemekea vibaya mno, jicho la chuki likinitizama kwa makini.

Tulibaki tunatizamana kama majogoo, nilikuwa nikimsoma dhamila ya yule mtu, alidhamilia kunitia mbaloni kwa hali yoyote itakavyo kuwa, sasa alikuwa akifikiria namna ya kunikabilia, japo alinipiga risasi ya bega lakini bado alikuwa na mashaka kidogo ya kunisogelea, hakuwa na imani na mimi hata kidogo.

“Umeingiaje humu ndani wewe?” hatimae aliniuliza.. “siyo muhimu kwako, muhumu kwako, ni kuacha ukinzani na mimi..wewe siyo saizi yangu hata kidogo Mwita,” nilisema kwa kiburi.

Na hapo nikaona kidole cha shahada kikivuta kifyatulio cha Kurusu risasi itoke katika ile bastola iliyo kuwa inanitizama..

Mlipuko mwingine ulisikika, na mara hiyo hiyo kipande kingine cha chuma kiliingia katika eneo la kiuno huku nikihisi kusukumwa kwa nguvu na nguvu ya risasi ile na kujibamiza katika ukuta na kujibwaga tena katika kitanda, kilicho geuka  kuwa bahali ya damu, sikuweza kusimama tena, damu zilinitoka kama bomba, hakika niliona nisipo kuwa makini naweza kushikwa au hata kuuwawa kizembe tena kwa mtu dhaifu kama huyu askari polisi.

Alinisogelea pale kitandani na kunishika mkono kisha akanivuta kwa nguvu na kujibwaga katika sakafu, huku macho yangu yakianza kukosa nguvu, na mwili kuwa dhaifu kabisa.

“Kwisha habari yako hayawani weee,”

alisema na kuanza kunipekua mwilini ni hapo alipo pata mshituko mkubwa baada ya kunigusa sehemu zangu za siri na kuona nina maungo ya kiume ilihali mwili wangu ni wakike, tena mwanamke mwenye wajihi wa hawala yake!.

“Looh! Mwanga mkubwa wewe..”

Alinitusi huku akichana nguo zile na kuniacha uchi. Mwili wa mtu wa ajabu ukawa mbele ya macho yake, wakati huo nilikuwa nikijitahidi kunuia maneno fulani ya kichawi ambayo niliamini ndio msaada kwangu kwa wasaa ule.

Aligutuka ghafla ikawa ni kama aliye pata kugundua jambo alitoka kasi na kuelelea maliwato,. “Uuuwiiiii!!” ukulele wa hofu ulimtoka afande Mwita baada ya kukukuta  kiwiliwili kingine cha hawala yake kilicho kuwa kimelala kule maliwato bila fahamu.,

Ndani ya dakika hizo hizo lundo la askari polisi wenye bunduki, likiongozwa na yule polisi mwenye kupenda kunipiga vibao lilingia mule ndani kwa kishindo, mkononi wakiwa bunduki ilihali ndani ya dakika hiyo hiyo afande Mwita alitoka kule bafuni akiwa amepagawa vibaya kwa yale mazingaombwe aliyo yashuhudia mule ndani wasaa ule, vile vile ilikuwa ndani ya dakika hiyo hiyo  nilikuwa nimekwisha kamilisha idadi ya sentesi za maneno yale ya kichawi niliyokuwa nikiyatamka.

Ilizuka taharuki ya aina yake.!

Yowe kubwa kutoka kwa wale maaskari akiwemo afande Mwita liliwatoka kwa pamoja baada ya kuhisi vitu vikali kama miiba vikiwachoma katika macho yao na hapo kukafuatiwa na miwasho mikali katika macho kama kwamba wamesilibwa kwa upupu.

Moshi fulani mwepesi ukuzuka mule ndani bila kuonekana unapo tokea,

Na hapo haikuwa macho tena, miili yao ilipatwa na miwasho ya hali ya juu mno,

Jamaa walizidi kujinyonga nyonga kwa miwasho mikali kabisa ya macho  milini mwao wote, huku akili zao zikihama kabisa dhidi ya kunikabili, ikawa kila mtu anahanagaika na kwa kujisuka suka hovyo.

Naam Ulikuwa ni wakati wa mimi kujiondoa mule ndani, sikuwa na nguvu za kusimama, nilijivuta kwa kutambaa na huku nikizongwa na maumivu makali kabisa damu zikiendelea kunivuja kama bomba,

Nilijiburuza kwa tumbo hadi mlango wa maliwato ambako kulikuwa na mwili wa hawala wa afande Mwita.

Nilizungumza maneno yangu ya kishetani tena, na hapa vitu fulani vyenye kufanana na unyoya mwembamba na laini mno vilitoka pia katika mwili wangu kupitia masikio macho na mdomo na kuingia katika kiwili wili cha yule binti aliye kuwa amelala sakafuni mule maliwato.

Na hapo ngozi yangu na viuongo vya mwili wangu vikawa vinayeyuka na kuja viungo vingine, vile ambavyo ni vyangu siku zote.

Naam ungepata bahati ya kuniona sasa ungeweza kuniona Vegasi yule yule halisi, nilisimama wima na kumtizima yule binti, jereha kubwa na baya lililokuwa kiunoni mwangu kabla ya kuhamia kwake likiwa linampa maumivu makali kabisa lile la beagani likimfanya atamani kufa kuliko kuendelea kuteseka kwa maumivu makali kiasi kile.

Nilitoka maliwato na kurejea mule ndani ambako nilikuta wale maafande wakiendelea kuhangaika na miili yao kwa kujikuna hovyo kutokana na miwasho mikali  milini mwao.

Nilimsogelea afande Mwita aliye kuwa akijikwaruza kwa nguvu kwa makucha yake katika mwili wake kutokana na miwasho mikali kabisa kwa sauti ya kunon’gona nikasema.

“Afande hizi ni salamu za awali kwako, nataka nikuonyeshe tu kuwa mimi siyo mtu wa kawaida, sasa basi kesho nahitaji niwe huru kule katika gereza vinginevyo uhai wako na wa hawa asakari wako na yule hawala yako aliye huku maliwato wote mtakufa kama kuku wa mdondo kama huamini endelea kutia ngumu pia napenda nikwambie kuwa jiandae kuchukua maiti ya kila mtu aliye husika na kifo cha awali cha Nasra na mwanae”

Nilisema na hapo hapoa nikayeyeuka kama moshi na kutoweka mule ndani.

******

Asubuhi ya siku ya pili nilistushwa na sauti kali ya muadhini, nilifumbua macho yangu na na kujikuta nipo katika kitanda cha zahanati ya gereza huku pingu zikiwa mikoni mwangu nimefungwa pamoja na chuma cha kitanda.

Nilijinyanyua na kuketi kitako kwa muda wa zaidi nusu saa nzima kabla ya nesi kuingia mule wodini ambako nililazwa peke yangu siku hiyo..

“Fahamu zimekureje eeeh…wewe kijana hawa polisi watakuja kukukorongoa meno kama utaendelea na tabia yako ya ujeuli ndani ya gereza..hii ni mara ya pili sasa unaletwa  humu ndani ukiwa umebamizwa hadi kupoteza fahamu.”

Alisema yule nesi na hapo nikakumbuka kipigo nilicho pigwa na afande Mwita jana mchana kabla ya kupoteza fahamu na kuingia katika ulimwengu wa pili, ulimwengu unao nifanya niwe zaidi ya binadamu.

Dakika kumi nyingine zilitosha kurudishwa ndani ya gereza afya yangu ikiwa  imerejea vema.

 

Je, nini kitaendelea?

Tukutane kesho.

Leave A Reply