JINI MTU-15

Miaka mingi iliyopita, Mama yako alikuwa mwanaume mwenye kuitwa Kalindimya, akafariki, ikaja siku akazaliwa upya akiwa mwanamke mwenye kuitwa bi Khajat au mama Vegasi kama alivyo kuja kuzoeleka!.enzi za usichana, Bi Khajat hakutakiwa kukutana kimwili na mwanaume hadi hapo atakapo fikisha miaka kumi na tisa, lakini siku moja kabla ya kutimiza miaka kumi na tisa, alibakwa na baba yako, lilikuwa ni kosa kubwa, alitakiwa kufa tena na azaliwe upya, mtu mmoja mwenye kuitwa Otumani Hilal ndiye aliye toa msaada mkubwa kwa mama yako na kuendelea kuwa hai,”

Alisema yule jini, kwa kiasi alizidisha taharuki kubwa ndani ya moyo wangu, alinipa taarifa za ajabu kabisa, taarifa ambazo sikuwahi kifikiri kama kuna matukio ya namna hiyo hapa duniani, tena yanayo tokea kwa watu wangu wa karibu kabisa, zilikuwa ni habari za siri ambazo sikuwahi kuzisikia katika maisha yangu ndani ya familia yangu.

Alikaa kimya kwa nukta chache ili yale maneno yaniingie vizuri kichwani mwangu, na kwa hakika yalipenya haswaa Kisha akaendelea kuzungumza.

Unaweza kujiuliza mama yako ni mtu wa aina gani? Jibu ni kuwa mama yako ni nusu jini nusu binadamu, mzee masele ambaye wewe ni kilembwe kwake, ndiye  mzazi wa Kalindimya ambaye alizaa na jini mtoto huyu mwenye kuitwa Kalindimya, miaka mingi badae huyu kijana alifariki katika ajali iliyo tokea bahalini, na mwili wake haukuonekana kabisa.

Kiasi cha miaka kadhaa kupita babu yako mzee masele alizaa mtoto mwingine na jini huyo mwenye kuitwa Shkira, Ndipo hapo alipo zaliwa mama yako, na katika makuzi yake ya utoto, alikuwa akieleza matukio mengi ya nyuma ambayo yalitokea angali yeye akiwa hajazaliwa kabisa, na kunawakati alisema yeye aliwahi kuishi akiwa mwanaume mwenye kuitwa kalindimya, hapo ndipo huyu jini Shakira alihitaji nguvu za kijini kumnusuru mwanae na fikra hizi.

Bi khajat asingweza kuwa na fikra hizi za kumbukumbu za nyuma hadi hapo ambapo angefikisha maika kumi na tisa bila kuingiliwa, kisha damu yake ya hedhi ingechukuliwa na kufanyiwa dawa na tatizo hilo lingekoma, kwa bahati siku moja kabla ya kufikisha miaka kumi na tisa alibakwa na baba yako na kushika mamba ambayo ulikuja kuzaliwa wewe, tatizo lake lilikuja kukomesha na huyu mtu ambaye ni adui yetu namba moja. Othuman Hilal”.

Hatimae Lody kenzy alimaliza kunipa mtiririko wa wa hadithi ya ukoo wangu ambao umetokan na majini.

Lakini bado nilikuwa na maswali kuhusu hujuma za Saaumya kohil au Hashim Azizi,  dhidi yangu,

Unajua vegasi kuna jambo moja ambalo   hilielielewi hapa, alisema  Lody kenzy huku akimalizia kabisa kile kinywaji cha damu yabinadamu iliyo kuwa imesalia katika chupa.

“Wewe pia ni nusu mtu nusu jini, ila umekuwa zaidi katika jamii za wanadamu, sasa kulikuwa na ulazima wa Saumya Kohili au Hashim Azizi kufanya kile alicho fanya, na halikuwa matakwa yake, isipokuwa matakwa yetu,” alisema akiwa anajiramba ramba midomo kama kwamba jambo alilokuwa analizungumza ni lakawaida sana kwake.. akaendelea kuzungumza.

“Punde baada ya kujulikana kuwa una sifa za kuwa kiongozi, ulingia katika kipindi kigumu cha mpito katika maisha yako ya duniani, nafikiri hadi sasa utakuwa  bado unapitia maisha magumu kabisa, hii yote ni kukufunza kuwa, lazma uelewe hasara za tabu na shida na ujue faida ya raha pia.”

Alisema yule jini.

“Hiyo tu, ndio sababu hata ya kifo cha mchumba wangu Nasra… ni  kwa sababu ya elimu hiyo tu… hadi ipelekee familia yangu kusambaratika, eeh?” niliuliza kwa ukali donge likiwa kooni mwangu.

Yule kiumbe alicheka tena katika namna ya masikhara kisha akasema, “kifo cha Nasra na mwanae ilikuwa nisadaka kwako, hakuna binadamu atakae tumikia jamii yetu bila kutoa sadaka, hilo liweke akilini mwako, na…”

“Kivipi Nasra awe sadaka kutoka kwangu?” Nilimkatiza kwa pupa.

“Ni sisi tulio kufanya uwe mikononi mwa Nasra kutoka huko Bunjumbura ulikokuwa ukishi kama mbwa koko,  ni sisi pia, tuliye mtwaa Nasra kupitia Hashim Azizi, japo wewe ulifanya jaribio la kumrejesha, isingewezekana Vegasi, na haijawahi kutokea kabisa, vilevile ni sisi tulio kwamisha jaribio lako la kuirejesha nafsi ya Nasra tena duniani… si uliona jaribio lako lilivyo feli kirahisi.. Labda nikwambie hivi, huwa tunapokea sadaka ya damu ya kile unacho kipenda lakini sambamba na hayo, ni jana usiku nyama ya Nasra imeliwa, na hii ni damu yake. Hayo ndiyo ninayo weza kukueleza ila kuhusu familia yako  sijui kilicho tokea.”

Ebwana wee!.

******

Nilifumbua macho yangu taratibu, kichwa kilikuwa kinaniuma vibaya mno, nililala zaidi ya masaa kumi mchana wa siku hiyo.

Vidonge vikali vya usingizi, ambavyo nimekuwa nikitumia vilinifanya nijisikiea mchovu sana, nilijinyanyua kivivu katika kitanda na kuketo kitako.

Nilikuwa nimeletewa chakula cha mchana, ilikuwa ni mkate na box kubwa la juic ya embe, nilishanga kidogo kwani haijawahi kutokea mahabusu ukatayarishiwa chakula kizuri kama kile.

Lakini wakati hayo yakipita kichwani mwangu, nilihisi kuwapo na mtu nyuma yangu, hii ilitokana na halufu nzuri ya manukato iliyo ibuka ghafla katika chumba kile.

Niligeuza macho yangu upesi huko nyuma.

Naaam, alikuwa ni yule jini  mwenye kuitwa Lody Kezy ambaye nilifanya nae mazungumzo muda mchache uliopita nikiwa usingizini

“Naona umenikimbia Vegasi na kurejea shimoni kwako,” alisema yule jini mwenye maneno mengi ya dhihaka.

Nilivuta pumzi na kuzishusha huku kifua kikipanda juu na kushuka, “ningewezaje kuendelea kuzungumza nawe ilihali nilikuwa katika ndoto na usingizi wangu ulifika kikomo”

“Ukomo wa maisha hayo ni leo usiku Vegasi…usiache kufika katika ibada takatifu ya kutawazwa kwako,”

Alisema Lody Kenzy, na mara hiyo hiyo aliyeyuka na kuacha moshi mwepesi wa rangi nyeupe ukielea katika anga.

Nilibaki katika mawazo mengi, matukio niliyo ambiwa na yule kiumbe hayakuwa matukio mepesi kiasi cha kutoweka kirahisi ndani ya kichwa changu.

Nilikaa katika kile chumba mpweke kwa masaa mengi mno nikifikiri mambo mengi katika maisha.

Kwa hakika nilikuwa ni mtu niliye kata tamaa kwa kiwango cha juu.

Miaka yote niliyo ishi duniani sikuwahi kujua kama mimi ni nusu jini nusu mtu, siku zote za uhai wangu, sikuwahi kufikiri kama siku moja nitakuja kuwa mkuu wa ulimwengu wa pili wa siri, wakati wote katika makuzi yangu, nilikuwa ni mtu mwenye matumaini makubwa ya kuona uzima wa mielele siku moja baada ya kufa, lakini sasa kila kitu kimehearibika, nipo upande wa shetani kwa karibu kabisa, niko mbali kabisa na Muumbaji wangu, na sasa natakiwa kutawazwa kwa ajili ya kumtumikia shetani rasmi. Siyo mbali.. ni leo siku..ndio usiku wa leo kuamkia kesho.

*******

Ilikuwa ni katika ukumbi mkubwa wenye kutengenzwa kwa vimto vya thamani, kulikuwa na mwanga hafifu wa taa za rangi nyekundu zilizo angaza eneo lile na kufanya wekundu mwingi kutapakaa eneo lile la ukumbi, zuria kubwa la rangi nyekundu na lenye manyoya mengi, na lundo kubwa la watu walio valia majoho mekundu yenye makofia  yaliyo funika nyuso zao, huku kukiwa na moshi usiyo weza kuumiza macho yako ama kifua alifuka eneo lile pasina kujulikana wapi chanzo cha moshi ule.

Nilikuwa kiti cha mbele nimeketi mbele ya lundo la watu wale kutoka nchi tofauti duniani, zaidi kukiwa na utitiri wa watu maarufu na matajiri katika dunia.

Macho yako yangepata bahati ya kuniona, ungeona joho kubwa jeusi liliokuwa mwilini mwangu huku kichwa changu na sehemu kubwa ya uso wangu ukifunikwa kwa kofia ya joho lile, katu usingeweza kunifahamu, katika namna nyingine  ungeweza kunifananisha na wale majambazi wa filamu za kibongo vile wanavyo vaa katika maigizo yao!.

Watu wengi.. wote walinisujudia.

Kwa kiasi kama dakika tatu, ulivuma upepo mkali na kuzima zile  taa nyekundu zilizo kuwa zikiwaka, kisha ule upepo ukavuma kuja usawa ule nilio kuwa nimekaa, kitu chenye kufanana na kimbunga kinacho vuma kwa kuzunguka kilitokea.

Upepo ulivuma kwa kasi na kufunua kofia la joho langu lakini mara hiyo hiyo nilifunikwa.

Niligeuza macho yangu kutizama nani aliye nikifunika macho yangu yalikutana na jini Lody Kenzy, alikuwa amesimama pembeni yangu huku na yeye akiwa mnyenyekevu mbele ya upepo huo.

Mara kilitokea kitu mbele ya kimbunga kile kilicho kuwa kikivuma kwa kasi, kimbunga kilichokuwa kikisindikizwa na upepo mkubwa.

Ilikuwa ni chupa yenye vimiminika vya rangi ya dhahabu, ile chupa ilikuwa ikielea angani huku ikiyumba yumba kulia na kushoto, bila kushikwa na kitu ama mtu yeyote.

Ile chupa ilinielekea mimi na kutakiwa kuichukua, nilisita kuipokea ile chupa, nikageuza macho yangu kwa halaiki kubwa ya watu kule mbele, maelfu ya watu walikuwa bado wamenisujudia kwa utii.

Nikarejea katika ile chupa iliyo nielekea kutoka katika kile kimbuga, nikitakiwa kuipokea, nikiwa bado sijajua nifanye nini dhidi ya tukio hilo, Lody Kenzy alininamia na kunitaka nipokee chupa hiyo kisha nifungue kiminika kile na kunywa yote mara moja.

Nilipokea ile chupa na kufanya kama nilivyo elekezwa na Lody Kezy, nilihisi tumbo zima likinichemka baada ya kugwida kile kimiminika.

Baada ya hapo Lody Kenzy aliniinamia tena na kusema, “sasa umekwisha pigwa muhuri wa shetani na kunywa damu yake, tayari u-mfuasi wake leo hadi milele”.

Ajabu ni kuwa sikuhisi uoga  wala aina yoyote ya mashaka ama huzuni.

Nilijsikia furaha tu, nilijona ni mtu huru, mwenye mamlaka makubwa, nilijiona ni zaidi ya kila kitu katika ulimwengu, naweza nikasema nilijisikia ni binadamu mwenye mafanikio makubwa mno.

Ule utitiri wa watu ulizidi kunisujuidia katika namna ya ajabu kabisa.

Lody Kenzy alinikabidhi kitabu kikubwa ambacho kiliandikwa kwa lugha ambayo sijawahi kuiona hapa ulimwenguni.

Kiasi cha masaa mawili ibada ile ilikamilika na mimi nilikuwa mfuasi mkuu wa ushetani.

Watu wote walitoka katika ule ukumbi na  kuondoka kuendelea na maisha yao kama kawaida.

Nilitumia wasaa ule kukutana na baadhi ya viongozi wachache katika utawala ule akiwemo mzee Zakora ama hakimu Cymon Mlwilo, ambaye imeaminika amekufa huko uraiani ilihali huku akiwa hai, tena kiongozi wa kuchinja watu walio takiwa kufa aidha kwa kafara, ama wafuasi wa wajenzi huru walio enda kinyume na maagizo ama matakwa ya jamii hii kwa upande wa nchi hii.

Lakini pia, nilikutana na Hashim Azizi au Saumya Kohili, ambaye alikuwa ni mtu mwenye kusimamia mienendo na taarifa zote za wafuasi wa wajenzi huru kwa upande wan chi hii.

Fauku ya hayo nilikutana na viongozi wengine wengi wa huko uraiani ambao mbele yangu hawakuwa si lolote, si chochote.

Hatimae baada ya taratibu nyingi, mimi na Lody Kenzy, tulitoweka eneo lile, na nukta chache badae tukawa ndani ya nyumba nadhifu, nyumba yenye kila aina ya kitu cha thamani unacho kifahamu,

“Hapa ndipo utaishi maisha yako yote, ni kwako hapa.” Alisema yule jini, Lody Kezy.

“Huku wapi huku?” niliuliza.

“Wanapaita komakoma.”

“Komakoma!!.” Niliuliza kwa mshangao kwani sikuwahi kusikia hilo jina katika masiha yangu

“Ndio, huku Mwananyamala komakoma”

“Ooh! Kwa hiyo hapa nipo Dar es Salama”

“Ndio., kwani muda wote ulikuwa hujajua hilo?”

Nilitikisa kichwa kumkubalia, akacheka kwa dhihaka kama kawaida yake kisha akasema.

“  Ulifikiri bado upo katika ardhi ya Kigoma.. wapi Kigoma kuwe na kasri la ibada la wajenzi huru? huku ndio kila kitu, na hata wewe utaishi huku miaka yote,”

“Na vipi kuhusu kule gerezani ninako ishi?., maana naamini hapa niko katika ndoto tu, muda si mrefu nitaamka na kujikuta niko kule shimoni”

Yule jini alicheka tena kwa nguvu, cheko ambalo sikuwa navutiwa nalo hata kidogo, japo niligundua kuwa kiumbe huyu hufurahi na kuona raha pale unapokuwa upo katika kitendawili fulani na kuhitaji masaada wake.

Hii siyo ndoto Vegasi, haya ni maisha  ya kweli yanayo endelea, kule kesi  ilikwisha futwa na file kufungwa. Wewe utakuwa huru na hakuna mtu yeyote atakae fungua mdomo kuhoji juu ya kesi yako na hatma yako..lakini hata hivyo kuna binadamu mwenye kuitwa Mwita alikuwa ni askari polisi kaacha kazi leo, na sasa yupo safarini ndani ya treni akija  Dar kukusaka wewe, kisha kulipiza kisasi kwa kifo cha mchumba wake anacho amini kuwa wewe ulisababisha., sina mashaka na huyo bwana mdogo isipo kuwa swali ninalo jiuliza ni kuwa kajuaje kuwa wewe sasa upo Dar?”

Alisema yule jini,niliketi katika sofa moja lililokuwa mule ndani nikitafakari tena yale maisha mapya huku nikimtafakari yule afande.

 

Je, nini kitaendelea?
Tukutane kesho hapa.


Loading...

Toa comment