The House of Favourite Newspapers

Jini Mweusi 54

0

 

Alijijengea heshima kubwa nchini Tanzania kutokana na utendaji kazi wake mkubwa aliokuwa akiufanya katika jeshi la polisi nchini Tanzania. Kutokana na umahiri wake, akajikuta akipandishwa vyeo na mwisho wa siku akajikuta akiwa Kamanda Mkuu Kanda ya Dar es Salaam, DCP.

Heshima yake inakuwa kubwa, kila anayemuona anamheshimu kutokana na utendaji wake mkubwa aliokuwa akiufanya. Pamoja na heshima zote hizo, mwanaume huyu aliyeitwa Dickson alikuwa mtu mwenye sura mbaya ambapo huko shuleni kipindi cha nyuma aliitwa kwa jina la Zinjathropus, yaani binadamu wa zamani.

Hakuwa na mchumba, hakuwa na mpenzi, alichokifanya ni kuanza kununua machangudoa. Alifanikiwa sana, alilala na wengi. Alipofika Dar es Salaam, akaendelea kulala nao ila kwa kila ambaye alimuona sura yake na kumgundua, alimuua, alitaka suala la kununua machangudoa liwe siri maisha yake yote.

Upande wa pili kuna mwanamke mrembo aitwaye Pamela, msichana huyu mwenye umbo matata amefika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi ya uchangudoa. Anapofika huko, kutokana na uzuri wake, anawapata wanaume wengi, anamtetemesha kila mtu, si wanaume tu, hata wanawake wenzake.

SONGA NAYO.

Unaweza kuja nyumbani leo?” ilisikika sauti ya Dickson kwenye simu.

“Mimi?”

“Kwani nazungumza na nani mpenzi? Ndiyo! Wewe hapo.”

“Mmh! Kwa leo sidhani, kuna msiba huku.”

“Nani amefariki?””Rafiki yangu, anaitwa Magreth!”

“Pole sana aiseee. Basi sawa, nitakucheki keshokutwa,” alisema Dickson na kukata simu.

Muda huo, mwili wake ulimuwaka moto, alikuwa na hamu ya kuwa na mwanamke hata kwa saa moja tu. Mtu pekee ambaye kila siku aliuridhisha moyo wake alikuwa msichana Pamela tu.

Alimpigia simu na kumwambia kwamba asingeweza kuja kwa kuwa alikuwa kwenye msiba wa rafiki yake. Hapo ndipo Dickson alipogundua kwamba kumbe Magreth alifahamiana na Pamela.

Hakutaka kukaa nyumbani, pepo la ngono alilokuwa nalo lilimchanganya mno, alichokifanya ni kuondoka nyumbani na kwenda Ambiance ambapo aliamini kwamba angepata msichana mzuri wa kulala naye usiku wa siku hiyo.

Kama kawaida yake akaingia ndani ya gari lake na kuanza safari ya kuelekea huko kwa ajili ya kumnunua changudoa na kulala naye usiku huo. Ndani ya gari, alijiona kuchelewa kufika huko alipokuwa akielekea, aliendesha kwa kasi kubwa na ndani ya dakika ishirini, akafika Ambiance ambapo pembeni kulikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakijiuza.

Hata kabla hajachagua yupi wa kumfuata, ghafla wasichana wanne wakasogea kule alipokuwa, walivalia mavazi tofauti, wengine taiti na wengine vimini vilivyoyaacha mapaja yao wazi.

“Ngoo… ngoo… ngoo…” kioo cha mlango wa gari kiligongwa na msichana mmoja. Akakishusha na kuwaangalia wasichana hao. Hakukuwa na aliyemfahamu kutokana na giza kubwa lililokuwa ndani ya gari.

“Karibu mpenzi…” alisema msichana mmoja huku akijinyonganyonga.

“Asante. Bei inakwendaje?”

“Kulala au show time?”

“Kulala!”

“Elfu sitini,” alisema msichana huyo.

“Nyingi sana. Mwingine?”

“Subiri kwanza kaka! Mbona hatujaelewana! Bei mazungumzo mpenzi!”

“Utapunguza hadi ngapi?” aliuliza Dickson.

Kilichokuwa kikiendelea mahali hapo ni kukubaliana kwa bei na changudoa huyo aliyesimama nje ya gari lake huku wale wengine wakiwa wamekwishaondoka kwani mwenzao huyo alichaguliwa hivyo ndiye aliyetakiwa kukubaliana bei na mteja huyo.

Baada ya dakika kadhaa, wakakubaliana na hivyo msichana huyo kutakiwa kuingia ndani ya gari na kuondoka mahali hapo, changudoa huyo akafanya hivyo.

Alivyoingia ndani ya gari, ndipo Dickson alipogundua uzuri wa changudoa huyo. Kimini alichokuwa nacho ambacho kiliishia mapajani, alipokaa kitini, kikajivuta kwa juu na kumfanya Dickson kuweweseka zaidi.

Hawakuchukua muda mrefu wakafika katika nyumba moja ya wageni iliyokuwa Manzese Midizini. Gari likasimamishwa hivyo kutakiwa kuteremka. Changudoa yule alibaki na mshangao, hakuamini kama safari yao ingeishia ndani ya nyumba hiyo.

Ilikuwa uswahilini mno ambapo bei yake isingeweza kuwa zaidi ya shilingi elfu tano. Mtu aliyekuwa amemnunua kutoka katika kiwanja chake, alionekana kuwa bwana wa haja, mwenye pesa lakini kitendo cha kupelekwa katika chumba kile, ilimshangaza.

“Tumefika!” alisema Dickson.

“Nidiyo humu?” aliuliza changudoa yule kwa mshangao.

“Ndiyo! Kwani tatizo nini?”

“Mbona unaonekana una pesa sana, au hata hili gari umeazima?”

“Hapana. Ni maamuzi tu. Unataka hela au unataka kulala kwenye kitanda cha gharama?” aliuliza Dickson, alionekana kuanza kukasirika.

“Nataka hela.”

“Kama unataka hela twendeni,” alisema Dickson.

Kwa sauti aliyoitoa, hata changudoa yule alihisi kwamba alimkosea Dickson kwa kumuoneshea ishara ambazo moja kwa moja zilionekana kama kudharauliwa, alitamani kumuomba msamaha lakini akashindwa kufanya hivyo, kama malipo yake, akaahidi kufanya kila liwezekanalo amchanganye chumbani tu.

Kofia yake haikutoka kichwani mwake, bado hakuhitaji kujulikana, kila kitu kilikuwa siri kubwa kwake, walipofika mapokezi, akalipia chumba na kwenda chumbani tayari kwa kufanya kile kilichowapeleka pale.

“Naruhusiwa kuweka masharti kama mteja?” aliuliza Dickson.

“Kama lipi?”

“Napenda kufanya gizani, sipendi taa.”

“Kweli?”

“Ndiyo!”

“Hata mimi napenda giza, hakuna tatizo,” alisema msichana huyo kwa furaha, tena huku akionekana kuchangamka sana, kwa muonekano wake tu, alionekana kuwa na kitu nyuma ya pazia, Dickson hakuelewa hilo.

Je, nini kitafuatia? Usikose riwaya hii ya kusisimua Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

Leave A Reply