The House of Favourite Newspapers

Jinsi Ya Kudhibiti Kupanda Kwa Shinikizo La Damu

Shinikizo la damu ni msukumo wa damu kwenye kuta za mishipa. Shinikizo la damu laweza kupimwa kwa ukanda wa mpira unaoweza kujazwa hewa. Ukanda huo hufungwa kwenye sehemu ya juu ya mkono na kuunganishwa na kifaa cha kurekodi shinikizo. Kifaa hicho hurekodi vipimo viwili. Kwa mfano, chaweza kurekodi kipimo cha 120/80. Nambari ya kwanza huonesha kipimo cha shinikizo la damu wakati moyo unapopiga (systole).

Nambari ya pili huonesha kipimo cha shinikizo la damu katikati ya mapigo ya moyo (diastole). Shinikizo la damu hupimwa kulingana na milimeta za zebaki. Madaktari husema kwamba shinikizo la damu ya mgonjwa limepanda wakati kipimo kinapozidi 140/90. Nini hupandisha shinikizo la damu? Hebu wazia unamwagilia shamba lako

maji. Unapofungua mfereji au unapopunguza ukubwa wa shimo la mfereji, unaongeza shinikizo la maji. Ndivyo ilivyo pia na shinikizo la damu. Shinikizo la damu hupanda wakati damu nyingi inapopita mshipani au wakati mshipa unapokuwa mwembamba. Mtu hupataje ugonjwa huo? Mambo mengi yanahusika.

MAMBO USIYOWEZA KUEPUKA

Watafiti wamegundua kwamba iwapo mtu ana watu wa familia wenye tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu, basi anakabiliwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huo. Takwimuzinaonesha kwamba mapacha wanaofanana hupata ugonjwa huo zaidi ya mapacha wasiofanana. Uchunguzi mmoja ulizungumza juu ya “kuchunguza habari

zinazopatikana katika chembe za urithi ambazo husababisha tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu.” Hiyo inathibitisha kwamba kuna chembe za urithi zinazosababisha tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu. Inasemekana kwamba uwezekano wa kupata tatizo hilo huongezeka mtu anapozidi kuzeeka na kwamba wanaume weusi wanakabili uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ugonjwa huo.

MAMBO UNAYOWEZA KUEPUKA

Tilia maanani lishe bora! Shinikizo la damu ya watu fulani linaweza kupanda wanapokula chumvi (sodiamu). Hiyo inahusu hasa wagonjwa wa kisukari, watu ambao shinikizo la damu yao

hupanda sana, wazee na watu fulani weusi. Mafuta mengi katika damu yanaweza kufanyiza utando wa kolesteroli kwenye kuta za ndani za mishipa. Hivyo, mishipa huwa myembamba na shinikizo la damu huongezeka. Watu ambao ni wazito kupita kiasi kwa asilimia 30 wanaweza kupata tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu.

Comments are closed.