The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya kuepuka maumivu ya tumbo la hedhi (period pains)

MAUMIVU ya tumbo la hedhi au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo.

Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana.

Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija kitaalamu fallopian tubes na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa mzunguko wa yai yaani Ovulation.

Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili.

Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba.

Aina hii ya maumivu ni ya kawaida na mwanamke huyapata sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.

Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.

Karibu nusu ya wasichana na wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi na karibu asilimia 15 wanasema kuwa hupata maumivu makali. Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.

Sababu hizo ni kuwa na umri wa chini ya miaka 20, kuvunja ungo ukiwa na umri wa miaka 11 au chini ya miaka hiyo, kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi, suala hilo linaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali ya kitiba.

Wanawake ambao hawajawahi kuzaa husababisha mtu kupatwa na maumivu ya tumbo la hedhi wengine ni kwa sababu ya magonjwa ambayo ni:

Adenomyosis: Huu ni ugonjwa wa wanawake ambapo tezi au uvimbe (tumors) zinaota katika mfuko wa uzazi.

PID au ugonjwa wa uvimbe katika nyonga. Magonjwa ya zinaa yanayotokana na bakteria au magonjwa ya kuambukiza ya zinaa na mlango wa uzazi unapokuwa mdogo kiasi kwamba unazuia damu ya hedhi isitoke kwa urahisi.

Hebu sasa na tuzijue tumbo la mwezi linaumaje?

Tumbo la mwezi mara nyingi maumivu huwa siyo makali kwani maumivu huja na kuondoka, na kwa kiwango tofauti (spasmodic).

Maumivu ya mwezi ya tumbo la hedhi huja sehemu ya chini ya tumbo au huchanganyika na maumivu ya sehemu ya chini ya mgongoni ambayo husambaa mpaka mapajani.

dalili zake ni kujihisi kutapika, kichefuchefu na wakati mwingine hata kutokwa jasho.

Dalili nyingine ni kupata choo kilaini au hata kuharisha au kufunga choo, tumbo kuwa kubwa au kuwa gumu na kuhisi maumivu ya kichwa na kutojihisi vizuri au kujisikia kuchoka.

Inapasa kujua kuwa, kiwango cha maumivu ya tumbo la hedhi na mchanganyiko wa dalili inategemea hali ya mtu, mtu mwingine anaweza akawa anapata karibu dalili zote nilizozitaja hapo juu na mwingine ni baadhi tu.

Wanawake wengi hutambua wanapopata tumbo la hedhi bila hata msaada wa daktari.

VIPIMO

Wanawake wanashauri iwapo watapata maumivu makali sana ni bora wakamuone daktari ili wafanye vipimo kama vile Ultrasound, CT na CT-Scan, MRI na vinginevyo ili kufahamu iwapo kama matatizo mengine ya kitibabu yanayosababisha maumivu hayo kuwa makali.

MATIBABU

Matibabu ya maumivu ya tumbo la hedhi huweza kutibika kwa kutumia vidonge vya kupunguza maumivu, kama vile Ibuprofen, naproxen au aina nyinginezo za vidonge visivyokuwa na steroids (NSAIDS).

Pia kuna wakati madaktari wanaweza kumshauri mgonjwa kutumia vidonge vya kuzuia mimba. Vidonge hivyo huzuia mzunguko wa yai au Ovulation na kupunguza ukali wa maumivu ya tumbo la hedhi.

Kuna baadhi ya tiba za mitishamba herbal ambazo husadia kupunguza muamivu ya tumbo la hedhi. Wachina ni watalamu wazuri katika ujuzi huo.

Wanawake washauriwa kuoga maji moto, kutumia hot bottle na hata kuweka kitambaa chenye joto katika sehemu ya chini ya tumbo wasikiapo maumivu.

Kuna baadhi husaidia kwa kufanya mazoezi, tiba ya sindano (Acupunture), au kushituliwa mishipa ya fahamu. Vilevile kutumia vidonge vya vitamin E, Thiamine na Omega 3 husaidia katika suala hilo. Wanawake wanaopatwa na matatizo kama hayo ni bora wapumzike vyema na kupata usingizi wa kutosha.

Tunaweza kujiepusha na kupatwa na maumivu ya tumbo la mwezi kwa kula matunda, mbogamboga na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi, pombe, cofeini, Sodium na sukari.

Comments are closed.