The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya Kukabiliana na Tatizo la Kukosa Hisia za Tendo la Ndoa

0

TATIZO hili huwatokea wanaume na wanawake. Ni tatizo linaloathiri hali ya kisaikolojia na kimwili. Hamu na hisia za tendo la ndoa kitaalamu huitwa Libido au Sex drive, ndivyo humsukuma binadamu ashiriki tendo hili. Libido au sex drive hutofautiana kiwango kati ya mtu na mtu. Wapo wanaume wenye kiwango kikubwa na wapo wenye kiwango kidogo na wenye kiwango cha wastani.

 

Hali hii hivyohivyo ipo kwa wanawake. Mwanaume mwenye kiwango kidogo cha libido au sex drive huhisi amepungukiwa nguvu za kiume, kumbe yupo vizuri ila tatizo ni kwamba hana hamu na hisia. Mtu mwenye kiwango cha juu cha libido na sex drive, awe mwanaume au mwanamke huwa hawatulii na hawatosheki, huhangaika huku na kule. Kama ni mwanaume hutamani kila mwanamke anayemuona na kama ni mwanamke hivyohivyo, haangalii kila mwanaume humuona anafaa.

 

Ingawa ongezeko wengi huliona zuri kuliko mapungufu, lakini ongezeko la libido au sex drive huleta madhara ya kupata magonjwa ya kuambukiza, migogoro ya kimapenzi na hata kuvunjika kwa mahusiano. Mapungufu yake pia huumiza kwani mwanaume hawezi kushiriki tendo la ndoa na mwanamke hupata maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa ujumla, hisia na hamu ya tendo la ndoa huongozwa na mifumo ya kibaolojia, kisaikolojia na kijamii.

 

Kibaolojia tunahusisha zaidi vichocheo au homoni, aina nyingine za kemikali zipatikanazo mwilini ziitwazo Neurotransmitters, hasa vichocheo vya Testosterone na Dopamine ambavyo vina kazi kubwa katika utengamano wa libido mwilini mwa binadamu. Matatizo ya kijamii yanayoathiri hamu na hisia za tendo la ndoa ni majukumu ya kikazi na kifamilia, matatizo ya kisaikolojia ni yote yanayokusibu na kuumiza akili yako, mfano hali ya kujikataa mwenyewe na kukata tamaa, msongo wa mawazo, haya yote huathiri hamu ya tendo la ndoa.

 

Hisia au sex drive vinaweza kuathiriwa na uwepo wa magonjwa makali kama kisukari, magonjwa ya moyo, maumivu ya mwili, kansa, HIV, matumizi ya dawa kwa muda mrefu na baadhi ya madawa kama ya moyo, kansa, TB na mengineyo. Hali ya maisha na mahusiano kama sio mazuri pia huathiri kuwa vizuri katika hamu na hisia za tendo la ndoa. Umri huathiri hamu na hisia hasa katika kipindi cha balehe, mara nyingi hamu na hisia za kushiriki ngono huongezeka miongoni mwa vijana wengi.

 

Mtu yeyote awe mwanamke au mwanaume mwenye hamu na hisia kubwa za kushiriki ngono kitaalamu huitwa Hypersexuality na yule mwenye kiwango kidogo tunaita Hyposexuality. Huwa inatokea mtu akawa na hamu sana ya kuhitaji kushiriki ngono, lakini mazingira hayamruhusu au sheria fulanifulani zinambana kutokana na misingi au taratibu mbalimbali, mfano za kidini au kijamii au kimaadili, basi endapo itatokea atashindwa kujidhibiti au kudhibitiwa na akaipata fursa hiyo, basi huanza kushiriki kwa fujo bila kuangalia anayemfuatilia na kushiriki naye ni mtu wa aina gani, kwa hiyo wakati mwingine mtu anaweza kujikuta amedumbukia katika dimbwi la ngono bila kujijua alianza vipi kumbe ni kushindwa kudhibiti hali ya hisia zake na hamu. Itaendelea toleo lijalo
Haja na utashi wa kushiriki tendo la kujamiiana, au sexual desire miongoni mwa binadamu husaidia kuimarisha maelewano mazuri endapo wawili hao watakuwa na mawasiliano mazuri.

Leave A Reply