The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya kukabiliana na tatizo la kulegea kwa misuli ya uke-2

0

Diagnose-Vaginal-Discharge

Tumekwishaona katika makala iliyopita jinsi tatizo hili la kulegea kwa misuli ya uke linavyotokea. Tatizo husababishwa na kuzaa kwa njia ya kawaida iwe mtoto mmoja au zaidi na hasa pale mwanamke anapoongezewa njia au kuchanika na utaratibu wa kuirekebisha hautafanyika kitaalam.

Chanzo kingine ni umri mkubwa kwa mwanamke, kadiri umri unavyozidi hasa kichocheo au homoni za kike hupungua hivyo husababisha mvutiko wa misuli kupungua na uke unakuwa mkavu.

Pamoja na yote lakini tatizo hili halina watu maalum, mwanamke yeyote aliye katika umri wa kuzaa anaweza kulipata. Mwanamke mwenye tatizo hili pamoja na matatizo mengi ya kiafya yanayoweza kumpata mwanamke kama matatizo katika haja ndogo na kubwa, maumivu chini ya tumbo, maumivu ya kiuno na nyonga, maumivu wakati wa tendo la ndoa na kukosa au kupoteza hamu ya tendo la ndoa vyote humkabili mwanamke mwenye tatizo hili.

Mwanamke mwenye tatizo hili pamoja na kupoteza au kupungua kwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa, vilevile huwa hafiki kileleni, yaani hafurahii tendo hata mara moja.

JINSI YA KUGUNDUA TATIZO

Pamoja na matatizo makubwa yanayompata mwanamke mwenye tatizo hili ambayo tayari tumeshakwishayaona, zipo dalili za awali ambazo mwanamke anazihisi, akichelewa ndipo tatizo linakuwa kubwa, mambo haya yapo matano;

Kwanza ni kuhisi kubanwa sana na mkojo na kukimbilia chooni, kama choo kipo mbali au kuna mtu, mkojo unaweza kumtoka. Akienda kukojoa anahisi mkojo hauishi wote na baada ya muda anarudi tena.

Mwanamke mwenye tatizo atapimwa kisukari hakuna, lakini atakuja kutibiwa kama yutiai kumbe siyo. Wakati mwingine akicheka sana au kukohoa pia matone ya mkojo humdondoka.

Hatua ya pili ili kugundua kama uke wake umepwaya ni kwa kutumia vidole. Inatakiwa vidole viwili tu ndivyo vipenye ukeni na kuhisi vimebanwa, vidole hivi ni kile cha kati na cha shahada. Endapo utaingiza vidole hivyo na usihisi vimebanwa hadi ukaongeza na kidole cha pete aidha ukahisi umebanwa kidogo au hujabanwa, basi ujue una tatizo la kupwaya au kulegea kwa misuli ya ukeni. Zoezi hili unatakiwa ulifanye mwenyewe, mwanamke kwa kutumia mkono wako wa kushoto.

Hatua ya tatu ni kujikuta humalizi tendo la ndoa kwa kufurahia na kutoa majimaji tofauti na hapo awali. Mwanamke mwenye tatizo hili hulalamika kutokufurahia tendo la ndoa, anakuwa na hamu kama kawaida lakini wakati wa tendo hafurahii kama zamani. Tatizo hili huwapata hasa wanawake waliokeketwa.

Hatua ya nne ni pale mwanamke ili afike kileleni wakati wa tendo la ndoa, ni hadi abane miguu yake ili kuongeza msuguano ukeni au atumie staili ambayo uume utabanwa ili apate hisia za msuguano.

Hatua ya tano ni ya mwanamke kukata tamaa na tendo la ndoa, yaani hana hamu tena ya kufanya tendo la ndoa, ana uwezo wa kukaa hata zaidi ya mwezi hana hamu, hili ni tatizo la kisaikolojia kutokana na matatizo anayoyapata kwa athari ya kulegea kwa misuli ya uke, mfano maumivu sugu chini ya tumbo, ukeni, kiuno na nyonga na athari nyingine zote.

NINI CHA KUFANYA?

Mwanamke hana sababu ya kukata tamaa, awaone madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama katika hospitali za mikoa kwa uchunguzi na tiba.

Leave A Reply