The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya kupata mtoto wa kiume au kike

0

WANANDOA au hata wasio na ndoa hujiuliza maswali haya. Nini nifanye ili nipate mtoto wa kike au kiume? Je, kuna dawa au vyakula vya kusaidia kupata mtoto ninayemtaka? Siku gani nikikutana na mwenzangu naweza kupata mtoto wa kiume au kike?

Jinsia ya mtoto
Mtoto hutengenezwa pale mbegu ya kiume inapokutana na yai la kike. Mbegu ya kiume hubeba vinasaba vya X na Y, wakati yai la mwanamke likiwa na vinasaba vya X peke.

kikutana na mbegu ya kiume yenye kinasaba cha X na yai la kike (yenyewe yana vinasaba vya X peke yake) mtoto wa kike hutungwa. Mbegu ya kiume yenye kinasaba cha Y ikikutana na yai la kike, mtoto wa kiume hutungwa.
Mbegu ya kiume Y + Yai la kike X = Mtoto wa Kiume.
Mbegu ya kiume X + Yai la kike X = Mtoto wa Kike.

Njia za Kupata Mtoto Wa Jinsia Uipendayo
Mbegu za kiume zenye vinasaba vya Y huwa ni nyepesi, husafiri kwa haraka katika via vya uzazi vya mwanamke na huishi kwa muda mfupi ukilinganisha na mbegu zenye vinasaba X. Zenye vinasaba X huwa nzito zaidi, huenda polepole na huishi kwa muda mrefu zaidi.

Hivyo, kinadharia ili kupata mtoto wa kiume unaweza ukakutana na mwenza wako siku ambayo yai la uzazi linatoka (ovulation), kwani mbegu Y itasafiri haraka na kukutana na yai ili kulirutubisha kuwa mtoto wa kiume.

Mtoto wa kike, kutana na mwenzi wako siku 2 au 3 kabla ya yai kutoka. Kwa sababu mbegu Y huishi kwa muda mfupi, nyingi zitakufa wakati zinasubiri yai huku mbegu X zikiwa kwa wingi mpaka siku yai linatoka. Yai likitoka mbegu X zitakuwa kwa wingi kuungana na yai kutunga mtoto wa kike.
Kiuhalisia, siyo rahisi kufanikisha hilo.

Njia Nyingine
Kuna njia mbalimbali zinazosemekana zinaongeza uwezekano wa kupata mtoto wa kiume au kike. Njia hizi inajumuisha kula vyakula vya aina fulani, mikao maalum ya kimapenzi, kuweka vitu sehemu za siri na nyingine nyingi bado haziwezi kutatua tatizo hili.
Mpaka sasa na maendeleo yote ya kiteknolojia hatujaweza kupata njia ya kuwezesha kupata jinsia ya mtoto unayoitaka. Ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu!

Leave A Reply