Jinsi ya kupika chapati za maji

Natumaini hujambo mpenzi msomaji wa safu hii ya Mahanjumati na unaendelea vizuri na majukumu ya kujenga taifa. Leo kama ilivyo ada tutajifunza jinsi ya kupika chapati za maji.

MAHITAJI
Unga wa ngano nusu kilo
Mayai 2
Sukari robo kikombe cha chai
Chumvi kijiko kimoja cha chai
Hiliki nusu kijiko cha chai
Maji ya uvuguvugu kiasi
Mafuta ya kupikia
MATAYARISHO NA KUPIKA
Chukua bakuli kavu weka unga, kisha sukari, chumvi, hiliki na maji kiasi.
Koroga mpaka mchanganyiko wako uwe mzito.
Baada ya hapo weka mayai na ukoroge tena.
Mchanganyiko wako usiwe mzito sana au mwepesi sana.
Baada ya hapo onja kama kila kitu kimekolea.
Bandika chuma cha kupikia chapati (fry-pan) jikoni huku moto ukiwa wa wastani.
Weka nusu kijiko cha chakula cha mafuta ndani ya fry-pan kisha yatandaze.
Hakikisha chuma kinapata moto na mafuta yamechemka halafu weka upawa mmoja uji wa chapati na uutandaze mpaka uwe flati.
Subiri mpaka chapati ikauke juu kisha igeuze upande wa pili weka mafuta kijiko kimoja kikubwa cha chakula kwa upande wa chini na wa juu kisha uanze kuikandamiza kwa juu na kijiko ili iweze kuiva vizuri kwa chini.
Endelea kugeuza ukiona imebadilika rangi na kuwa ya brown itoe na uweke kwenye sahani, endelea kufanya hivyo mpaka umalize na hapo chapati zako zitakuwa tayari kuliwa.

Loading...

Toa comment