The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya Kupika Futari ya Mihogo na Samaki

LEO kwenye mapishi tutaona jinsi ya kupika futari ambayo ni tamu sana ya mihogo na samaki.

Mahitaji:

-Mihogo.

-Nazi.

-Chumvi.

-Samaki.

-Limao/ndimu.

-Mafuta.

-Pilipili-manga.

-Kitunguu swaumu.

-Tangawizi.

Maandalizi:

Menya mihogo, katakata vipande vidogovidogo, injika jikoni. Acha kwenye moto kwa dakika 10 kama unatumia gesi.Kuna nazi, chuja kisha mimina nazi kwenye mihogo ikiwa bado inachemka. Tia chumvi kidogo, acha vitokote kwa dakika 10 nyingine ili nazi ichemke. Bonyeza kwa mwiko uone kama umelainika. Kama umelainika epua, kama bado ongeza maji kidogo ili uive.

Samaki:

Andaa samaki wako kwa kuwaparua na kuwaosha vizuri.Wakate mstari kila upande, pakaa chumvi na limao au ndimu. Pakaa viungo vingine kama pilipili-manga, vitunguu swaumu na tangawizi (ukipenda).

Weka mafuta kwenye kikaangio. Injika mafuta kwenye moto yachemke, kaanga samaki mpaka wawe na rangi ya kahawia kisha ipua.

Waweza kuipamba sahani uliyopakulia chakula chako kwa kachumbari na limao au ndimu kwa ajili ya kuongeza ladha zaidi wakati wa kula

 

Na Hamida

Comments are closed.