The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya kupika Katlesi za  nyama

0

Mambo vipi mpenzi msomaji wa safu hii, Leo ni Jumamosi nyingine tunakutana ambapo tunajifunza jinsi ya kupika kitafunwa aina ya Katlesi za nyama kama wengi mlivyoomba.

 

MAHITAJI

Viazi mviringo kiasi chako

Chumvi

Pilipili

Vitunguu swaumu

Vitunguu maji

Karoti

Nyama

Unga wa ngano au sembe

Mayai

 

KUANDAA NA KUPIKA

Chukua nyama kisha ioshe halafu kata vipande vidogo.

Kata vitunguu maji vipande vidogovidogo, karoti kisha ponda vitunguu swaumu.

Weka viungo kwenye nyama, yaani vitunguu swaumu, chumvi na pilipili.

Bandika jikoni acha mpaka iive vizuri na uhakikishe maji yamekauka. Ikishaiva epua weka pembeni.

Chukua viazi vichemshe kisha vipondeponde na uchanganye na nyama.

Tengeneza madonge kisha gonga mayai  mawili na uyakoroge vizuri.

Chukua madonge uliyoyatengeneza chovya kwenye mayai halafu nyunyizia unga wa ngano au sembe.

Bandika mafuta ya kupikia jikoni, yakishachemka weka madonge yako ambayo tayari umeshachovya kwenye mayai na kunyunyizia unga.

Yaache yaive vizuri huku ukigeuza. Baada ya kubadilika rangi toa na weka pembeni.

Hapo kitafunwa chako kitakuwa tayari kwa kula.

Leave A Reply