The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya kupika wali wa maharage na nazi

0

wali maharage (1)
Leo tunajifunza kupika wali na maharage ya nazi.

MAHITAJI

Mchele kilo moja

Maharage nusu

Mafuta ya kupikia

Iliki pakiti moja

Nazi moja

Chumvi

Karoti moja

Kitunguu maji kimoja

wali maharage (2)KUPIKA MAHARAGE

Chambua maharage  yako vizuri,  yaoshe halafu weka kwenye  sufuria safi, weka maji kiasi kisha yachemshe mpaka yaive.

Yakishaiva ipua, chukua sufuria safi bandika jikoni likishakauka maji mimina mafuta ya kula yaache yapate moto.

Baada ya hapo weka vitunguu maji ambavyo umevikatakata vipande vidogovidogo, kaanga mpaka vibadilike rangi na kuwa vya kahawia (brown), weka karoti ambazo umekata vipande vidogovidogo.

Vikishaiva weka maharage uliyochemsha na chumvi kiasi, vikishachanganyikana weka tui la nazi subiri lichemke kwa dakika tano na hapo mboga yako itakuwa tayari.

WALI WA ILIKI

Pepeta mchele wako vizuri ili kutoa uchafu.

Chukua sufuria safi, weka maji yanayotosha kupika wali wako kisha yabandike jikoni huku ukiweka chumvi, mafuta ya kupikia na iliki halafu funika.

Yaache yachemke, baada ya hapo weka mchele ambao tayari umeshauosha kisha koroga huku ukiangalia kama                    chumvi imekolea.

Baada ya hapo funika subiri maji yakikaukia geuza ili uive pande zote.

Funika kisha subiri kwa dakika kadhaa geuza tena kwa mara ya pili ukiona maji yamekauka kabisa, hapo wali wako utakuwa tayari kwa kula.

Leave A Reply