The House of Favourite Newspapers

Jinsi ya kutengeneza kachori

0

0000150_kachoriMambo vipi mpenzi msomaji wa safu hii ya Mahanjumati, kama kawaida tunaandika kutokana na maombi yenu ambapo tunajifunza kutengeneza kachori, karibu tuwe pamoja.

MAHITAJI

Viazi

Kitunguu swaumu

Chumvi                                                                 

Pilipili ya kusaga                                                 

Ndimu                                                                 

Mafuta ya kupikia

Unga wa dengu au ngano

KUTAYARISHA NA KUPIKA

Chemsha viazi mpaka viive kisha vitoe maganda na uviweka kwenye bakuli.

Vipondeponde kwa mkono mpaka viwe laini.

Saga vitunguu swaumu na tangawizi kisha changanya na viazi .

Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga kisha uonje, unaweza kuongeza viungo hivi kwa kadiri unavyotaka.

Tengeneza madonge ya duara uyapange katika trei.

Changanya unga  wa dengu au ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo.

Weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto.

Chovya madonge kwenye unga na uyaweke kwenye mafuta ya moto.

Acha kachori zibadilike rangi ziwe za njano na uzitoe kwenye mafuta.

Ziweke kachori kwenye sahani zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Leave A Reply