Jinsi ya kutengeneza kachori
Mambo vipi mpenzi msomaji wa safu hii ya Mahanjumati, kama kawaida tunaandika kutokana na maombi yenu ambapo tunajifunza kutengeneza kachori, karibu tuwe pamoja.
MAHITAJI
Viazi
Kitunguu swaumu
Chumvi
Pilipili ya kusaga
Ndimu
Mafuta ya kupikia
Unga wa dengu au ngano
KUTAYARISHA NA KUPIKA
Chemsha viazi mpaka viive kisha vitoe maganda na uviweka kwenye bakuli.
Vipondeponde kwa mkono mpaka viwe laini.
Saga vitunguu swaumu na tangawizi kisha changanya na viazi .
Weka chumvi, ndimu na pilipili ya unga kisha uonje, unaweza kuongeza viungo hivi kwa kadiri unavyotaka.
Tengeneza madonge ya duara uyapange katika trei.
Changanya unga wa dengu au ngano kwa maji uwe mwepesi kidogo.
Weka mafuta ya kupikia ndani ya karai na uliweke kwenye moto.
Chovya madonge kwenye unga na uyaweke kwenye mafuta ya moto.
Acha kachori zibadilike rangi ziwe za njano na uzitoe kwenye mafuta.
Ziweke kachori kwenye sahani zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa.