JIONEE! Magari Yote Haya, Kompyuta Kuuzwa ‘Bure’ Dar – Video

MAGARI ya bure kuuzwa Dar! Hivi ndivyo unavyoweza kusema kufuatia Kampuni ya Udalali ya Tambaza Auction Mart and General Brockers Ltd iliyopewa mamlaka na TRA ya kupiga nada mali zilizotelekzwa bandarini ama ambazo wateja wake wameshindwa kuzilipia kodi/tozo.

Wiki hii tambaza watakuwa na mnada mwingine mkubwa wa hadhara ukihusisha magari na vitu vingine kibao, utakaofanyika katika Bandari Kavu ya Dar es Salaam, Jumamosi hii, Juni 15, 2019.

Magari hayo ni yale yaliyoingizwa nchini kisha wenye nayo wakashindwa kuyalipia kodi hivyo yakataifishwa na Serikali kwa mujibu wa sheria hivyo yanauzwa katika mnada wa wazi baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.

 

Akizungumza na Global TV Online, Ofisa wa Tambaza Auction Mart, Krotida Mlimila amesema wananchi wote wanaruhusiwa kwenda kukagua bidhaa zote zitakazouzwa kwenye LCDs zilizopo ofisi za LW9, Bandarini, nyuma ya Police Central kuanzia kuanzia Alhamisi ili siku ya mnada wanunue kirahisi.

Amesma baadhi ya vifaa vitakavyopigwa mnada Jumamosi ni pamoja na magari ya kisasa, vifaa vya kilimo, ujenzi nondo, tiles, mitumba na vitu kibao.

Mbali na hivyo, pia kutakuwa na kompyuta, viatu, mabegi, makontena ya nguo, ndondo, rangi za nyumba, mataili ya gari, baiskeli za watoto na vitu vingine kibao.

Mnada huo wa aina yake utaanza Jumamosi saa 4:00, Ubungo

(Kwa Mawasiliano piga 0713 327 989 au 0715 683 777 au 0713 508 158 au nenda ofisini kwao, Sinza Mori ama jengo la RITA, Ghorofa ya 18, Posta Dar).

 

 

 

 

TAZAMA VIDEO HAPA

Loading...

Toa comment