The House of Favourite Newspapers

JKT Queen Bado Haikamatiki Ligi Ya Wanawake

LIGI Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, moto wake unazidi kushika kasi kwa timu shiriki kupambana kwa kiasi kikubwa kuwania ubingwa wa ligi hiyo ambao upo mikononi mwa JKT Queens.

 

Kwenye ligi hiyo, ni timu ya JKT Queens pekee ambayo haijawahi kuonja ladha ya kipigo hadi kufikia mzunguko wa tisa ambao timu zote zimecheza mechi zake.

Ligi hiyo inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Lite, imekuwa na msisimko wa namna yake na suala kubwa ni jinsi timu shiriki zinavyobebeshana mizigo ya mabao tofauti na ile ligi ya wanaume. Si ajabu kufika katika Ligi ya Wanawake kuona timu ikifungwa mabao 7-0 ama zaidi ya hapo. Makala h a y a y a n a k u c h a m b u l i a juu ya mwenendo wa ligi hiyo namna inavyoenda hadi sasa.

WAJEDA HAWANA MASIHARA

Hadi sasa, staa wa JKT Queens, Fatuma Mustapha hakamatiki hata kidogo kwenye suala la kupachika mabao kwani ndiye kinara wao akiwa na mabao 18 katika mechi tisa ambazo timu yake na nyingine zimecheza. Fatuma ambaye ni muajiriwa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), anafuatiwa na mshambuliaji mwenzake wa kikosi hicho, Asha
Rashid ‘Mwalala’ aliyefunga mabao 17.

 

SIMBA QUEENS MAJI YA SHINGO Wiki chache nyuma, Simba Queens walikuwa moto kwelikweli na wakawa wanawafukuzia kwa ukaribu sana vinara JKT Queens, lakini sasa mambo yamekwenda tofauti kwani wamepitwa pointi 11 na JKT. S i m b a wamepoteza pointi sita kwenye mechi mbili zilizopita wakiwa mkoani ambapo walifungwa na Panama ya Iringa na Baobab ya Dodoma.

 

HAWA MAMBO MAGUMU KWAO

Hadi sasa, timu za Evergreen ya Dar es Salaam na Mapinduzi ya Njombe, ziko taabani kweli kwani ndizo zinakamata nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi hiyo. Timu zote hizo katika mechi tisa, zimeambulia pointi mbili tu kila moja. Kitu cha ajabu kwenye mechi zao zote walizocheza hadi sasa hawajashinda mechi yoyote ile, wamefungwa saba na kuambulia sare mbili tu.

Kikosi cha  JKT Queens. 

JKT QUEENS WAWEKA REKODI YA AJABU JKT

licha ya kuwa watawala wa ligi hiyo, pia ndiyo timu ambayo imeweka rekodi ya aina yake kwani hadi sasa hawajafungwa hata mechi moja ikiwa ndiyo timu p  ekee haijapoteza wala haina sare. Imevuna mabao 59 baada ya mechi tisa tu.

YANGA PRINCESS WAFUFUKA

Kikosi hiki kinachonolewa na kocha Khamis Kinonda, kuna wakati kilipepesuka na kujikuta kikipoteza mechi zake mfululizo ikiwemo ile ya dabi dhidi ya Simba Queens ambapo kilipokea kichapo cha mabao 7-0, lakini kwa sasa kimerudi relini. Yanga Princess imevuna pointi sita kwenye mechi mbili zilizopita, huku ikionyesha uwezo wa hali ya juu tofauti na ilivyokuwa mwanzoni mwa ligi hii.

MIKOA NANE, VIWANJA TISA

Nyasi za viwanja tisa zimekuwa zikiwaka moto kwa ajili ya ligi hii. Viwanja hivyo ni Meja Generali Isamuhyo unaotumiwa na JKT Queens, Karume (Yanga Princess, Simba Queens na Evergreen), Mabatini (Mlandizi Queens), Nyamagana (Alliance Girls na Marsh Queens) na Sheikh Amri Abeid (Tanzanite FC).

 

Vingine ni Samora (Panama), Lake Tanganyika (Sisterz) na Jam hur i (Baobab). Pia mikoa nane ndiyo timu zake zinashiriki ligi hiyo ambayo ni Dar wenye timu za Yanga, Simba, JKT Queens na Evergreen, Pwani ipo Mlandizi Queens, Mwanza kuna Alliance na Marsh Queens. Njombe inawakilishwa na Mapinduzi Queens, w a k a t i Arusha wanayo T a n zanite, Kigoma inabebwa na Sisterz, N j o m b e kuna Mapinduzi na Dodoma ipo Baobab Queens.

 

MSIMAMO ULIVYO J K T Queens n d i y o mama lao kwenye ligi wakiwa vinara baada ya
kuku-sanya alama 27, wakifuatiwa na Sisterz FC wenye alama 20, Mlandizi Queens wapo nafasi ya tatu na alama 19, Alliance wenyewe wamefunga nne bora wakiwa na alama 17.

 

Simba Queens wanakamata nafasi ya tano na pointi 16 sawa na Panama w e n y e pointi 16, kisha Yanga Princess wao wanakuja wakiwa na pointi 12 wanaokimbizwa na Tanzanite wenye pointi tisa sawa na Baobab. Marsh wao wana pointi sita wakiwa nafasi ya tatu toka mkiani huku Evergreen na Mapinduzi wenyewe wanaburuza mkia wakiwa na pointi mbili tu.

Comments are closed.