JKT Queens: Tumebakiza mechi 3 tupewe kombe

KOCHA Mkuu wa JKT Queens, Ally Ally amesema kuwa amebakiza mechi tatu kushinda ili atangazwe kuwa bingwa wa ligi ya wanawake Tanzania inayodhaminiwa na bia ya Serengeti.

 

Akizungumza na SportXtra, Ally alisema; “Kwa sasa nimebakiza mechi tatu kucheza kisha nitangazwe kuwa bingwa ninajiamini na ninawaamini wachezaji wangu tutashinda mechi zote na kuurejesha ubingwa.”

“Hakuna anayetutisha kwa sasa ndio maana ukiangalia idadi ya mabao ambayo tumefungwa haitishi
kama idadi ya mabao ambayo tumefunga, tumefunga mabao 82 na kufungwa mabao matatu pekee,” alisema Ally.

 

JKT Queens wamejikusanyia pointi 42 wakiwa ni vinara wa ligi huku anayefuatia ni Mlandizi Quuens mwenye pointi 29, wote wakiwa wamecheza michezo 14.


Loading...

Toa comment