The House of Favourite Newspapers

Joakim Low Aachia Ngazi Ujerumani

0

BAADA ya Ujerumani kutupwa nje kwenye Michuano ya Euro 2020 kufuatia kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Uingereza katika hatua ya 16 bora, kocha wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Joakim Low ameachia ngazi, Low ameiongoza timu hiyo kwa miaka 15 na kufanikiwa kutwaa Kombe la Dunia 2014.

 

Alichokisema Joakim Low baada ya kuachia ngazi; “Imekuwa miaka 15 mirefu na yenye wakati mzuri sana, kwa kweli, lakini kuna baadhi ni ya kukatisha tamaa.

 

“Timu na wachezaji wana hatma nzuri mbele yao. Bahati nzuri kwa Hansi Flick (kocha mpya), namtakia kila la heri, moyo wangu unaendelea kudunda kwenye rangi nyeusi, nyekundu na dhahabu.”

Stori: Sifael Paul

Leave A Reply